Dodoma: Mume adaiwa kumuua mke wake kwa shoka kisa wivu wa mapenzi

Dodoma: Mume adaiwa kumuua mke wake kwa shoka kisa wivu wa mapenzi

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Tukio la mauaji linalodaiwa kusababishwa na wivu wa mapenzi limetikisa Kijiji cha Mapinduzi, Kata ya Kigwe, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma, baada ya mwanamke mwenye umri wa miaka 58, Clementine Pius, kudaiwa kuuawa na mumewe, Raphael Ulanga kwa kushambuliwa kwa shoka kichwani.

Tukio hilo limetokea Octoba 14, 2026 majira ya saa 4 usiku, ambapo Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu wamesema mtuhumiwa Raphael Ulanga baada ya kutekeleza shambulio hilo alijisalimisha mwenyewe katika kituo cha polisi.

Ndugu wamesema kifo cha Marehemu kimewaacha katika majonzi makubwa, huku wakihimiza wanandoa wenye migogoro kutafuta suluhu kupitia mazungumzo, usuluhishi na msaada wa kisheria badala ya kutumia nguvu.

Akizungumzia tukio hilo, Diwani wa Kata ya Kigwe, Adon Mabalwe, ameeleza kusikitishwa na mauaji hayo na kutoa wito kwa wanandoa na familia zinazokabiliwa na migogoro kutafuta msaada kutoka kwa viongozi na vyombo husika kabla tofauti zao hazijafikia hatua ya kusababisha madhara makubwa.

Soma Pia: Dodoma: Adaiwa Kumuua Mkewe kwa kumchoma kitu chenye ncha kali shingoni

Aidha Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi na hatua nyingine za kisheria, huku mtuhumiwa akishikiliwa kwa ajili ya hatua za kisheria

Chanzo: Jambo Tv


​
 
1792078272420.jpeg
SAMBAZA UJUMBE, ... HALI NI MBAYA!
 
Imezidi sasa kuna changamoto gani aisee?

Mboni wengine tunaishi nao na hatuwazi kuwauwa nyie wengine mnakwama wapi hadi kubebelea vishoka kuwauwa?
 
Akina mama wanachepuka sana waziwazi akiona haitoshi anakuita,kibamia,mwanaume suruali,kimoja chali huku mume anajua kabisa anamegewa sishabikii ila huyu jamaa anaonekana alidhamiria akaona bora akifie jela
Wanawake wangekuwa na subira na kuwaza kabla ya kufungua vinywa ndoa nyingi zingeponywa ila bahati mbaya hawawezi hii wanaiweza wanaume tu.
 
Ila wanaume wengine bana, unaendekezaje wivu kwa mwanamke wa miaka 58🤔
😂😂😂😂🤣🤣🤣😅😆😆😆😆😁😁😁😁😄😄😃😃😃😆😁😁😄😄😅😅🥰
 
Kibaya zaidi ni kwamba hao wanaofanya hivyo wanaonekana mashujaa huku kwenye mitandao,
Hali inayochochea wengine pia kuona kumbe inawezekana tu kufanya.
Hii ni hali mbaya. Mungu atusaidie
 
Back
Top Bottom