Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Yani hata Mbowe akipigwa na wakina Lijua likali au Lwakatare basi inasingiziwa CCM jamani kwani mbowe hana maadui ukizingatia sekeseke lililomo ndani ya chama saizi
Ina maana mkuu huwa hujasoma kabisa dictatorial regimes na jinsi zinavyooperate???????
 
Amka peke yako.
Tuache sie bado tumelala usingizi mtamu kwenye nchi yetu.
Di*k head
Akili ni nywele ndiyo maana wakati wewe unashinda na njaa sisi wenzako tunakula bata lkn bado hatuna mipango na ccm.
 
Ni magufuli aliyemshambulia?
Mkuu try to think beyond the box! Hii serikali inaongozwa na Magufuli na kwa cheo chake kama amiri jeshi wa nchi vyombo vyote vya dola vipo chini yake, hivyo kunapotokea hali ya kutowepo na AMANI kwa wananchi, yeye hawezi kujitenga na lawama!

Pia ni Mwenyekiti wa CCM taifa , hivyo kama mipango hii miovu inapangwa na CCM , hapa anachomokaje! Tunajuwa hawezi kuhusika moja kwa moja lakini kwa nyadhifa zake ndiye anapaswa kujenga mazingira ya kuhakikisha matukio kama haya hayatokei au yanakomeshwa!
 
Huo ndiyo ukweli
Huu ndio ushahidi kwa nini watu wanatunga sheria za kujilinda.

Pia swala la Lissu ni mwiba sana kwa sababu hakua asiye jua muhusika.

Kufuta habari za Lissu wameamua kuleta haya majanga.

Ipo siku CCM mtalazimishwa kunywa damu za watu. Waulizeni wacongo chini ya mabutu.
 
Mjadala kuhusu Tundu Lissu kutia nia ya kugombea uraisi wa JMT umekuwa moto mkali ndani na nje ya nchi.

Ili kuondoa umaarufu huo, mzee wa master mind ameamua ku-divert attention hiyo kwa kumvamia na kumjeruhi mh. Freeman Mbowe.

Sasa anaye-trend siyo Lissu tena bali ni Mbowe.

Screenshot_20200609-082549.png


Screenshot_20200609-083701.png
 
View attachment 1472626
View attachment 1472650

Salaam,

Taarifa nilizozipata hivi punde toka chanzo changu kinanihabarisha kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman A. Mbowe amevamiwa na kikundi cha watu wasiojulikana akielekea nyumbani kwake usiku huu na kupigwa na wamemuumiza.

Tukio hili limetokea majira ya saa 6-7 usiku.

Mhe. Mbowe amekimbizwa Hospitali ya Ntyuka iliyopo jijini Dodoma.

Kamanda Muroto amesema wamepata taarifa kuwa kavunjwa mguu wa kulia na amelazwa Wodi namba 4 hospitalini hapo. Amesema taarifa zaidi zitafuata

MAONI YANGU:
Mh. Mbowe kuvamiwa na kupigwa eneo la Area D, jijini Dodoma, Mtaa wa Sengia; linalotajwa kuwa na ulinzi wa kutosha, kama ilivyotokea kwa Lissu kunaacha maswali mengi, je, hili linaweza kuwa limechochewa na Lissu kutangaza nia ya kugombea Urais wa JMT October 2020? Ni hasira au kitu gani? No one knows.

Bado najiuliza; hivi kama Taifa kwa tabia hizi za kihuni tunaelekea wapi? Hawa wanaojichukulia sheria mikononi kila siku wanafanya hivyo kwa kutumwa na nani? Matendo haya yataendelea kwa viongozi wa upinzani mpaka lini?

We need to wake up, better late than never.
 
Back
Top Bottom