Mbona unajilisha upepo ndugu bila sababu yoyote? Mbona una argue mambo kwa hisia (emotions) zako badala ya uhalisia...?
Kama wewe unaona "karaha" kutoka kwenye baadhi ya maoni (comments) ya watu humu kwa kuwa ziko "hasi" na "interests" zako, basi tatizo siyo comments hizo bali tatizo halisi ni wewe mwenyewe...!
Hebu nikuulize maswali kadhaa na ukiweza kuyajibu kwa usahihi bila kuidhulumu nafsi yako, itapendeza na kukusaidia sana;
Tuambie, una maana gani kusema unaweza kuleta comments "hasi" na zenye "karaha" na "matusi" za wana CHADEMA 200?..
Umetumia kipimo gani tusichokijua sisi kuwatambua members wote wa JF kwa "nembo" zao za vyama vyao vya siasa?
Au ni lini na kwa kutumia vigezo gani hasa umeweza kuwa - classify members wa JF wote kuwa huyu ni CHADEMA , huyu ni CCM, huyu CUF, huyu ACT Wazalendo, huyu CHAUMA, huyu TLP na huyu hana chama nk nk?
Hebu tuambie umewezaje ndugu? Umetumia vigezo gani?...
Je, kwa kutumia kigezo hiki unachosema; "comments au maoni HASI na yenye KARAHA na yenye MATUSI " dhidi ya CCM na Magufuli?
Kipimo na tafsiri ya jumla (si yako wewe peke yako) ya; u - HASI, u- KARAHA na u - MATUSI ni ipi?
Kama utajibu maswali haya kwa uaminifu na kwa dhati ya moyo wako bila kuidhulumu nafsi yako haki yake, utagundua kuwa "arguments" zako zinatawaliwa mapenzi na hisia mbaya na mbovu za kisiasa zilizovuka mipaka ya ustaarabu pasipo kuwa na uhalisia...!!
Nikuambie kitu kimoja tu kwa nia ya kukuelimisha kuhusu jambo moja muhimu sana ktk uhalisia wa maisha ya binadamu...
Kwamba, kutofautiana kimitazamo ni jambo la kawaida miongoni mwa wanajamii iwe ndani ya familia moja, kati ya wanandoa, wafanyakazi kwenye shirika ama kampuni moja na wanachama wenyewe ndani ya chama cha siasa...
Mfano, ndani ya CCM kwenyewe huwa kuna kutofautiana kimawazo. Lakini haiondoi ukweli kuwa wote hao bado wanakuwa wanachama wa chama kimoja...
Kama utakereka kwa kuwa tu mawazo yako hajaungwa mkono na wenzako, kama nilivyosema tangu awali kuwa, tatizo linakuwa siyo mawazo hasi ama yenye karaha ya wenzako. Tatizo halisi unakuwa ni wewe...!!
Mara nyingi watu wa dizaini yako, wasio na "kifua" cha kupokea mawazo ya kuwakosoa ama kuwapinga ama yaliyo kinyume na matakwa yao huwa ni wabinafsi (selfish) na mtu mbinafsi mara nyingi "option" yake ya mwisho akishindwa kwa hoja, ni kumdhuru mpinzani wake na kama ana uwezo atamuua kabisa...!
Hawa watu hawana sifa ya kuwa viongozi ktk jamii. Wanapaswa kuwa viongozi wa kujiongoza wao wenyewe tu....!
Kwa hiyo kama mnatumia kigezo hiki kupiga watu risasi ama kuwateka na kuwapoteza na kuwajeruhi wengine kama ilivyotokea kwa Mh. Freeman Mbowe leo, mnafanya vibaya na mnaonea watu bila sababu....