Dodoma: Mzee Mangula ulichomfanyia Dkt. Kikwete, Mungu anakuona

wakatanta

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2018
Posts
2,594
Reaction score
3,158
Hakika huyu mzee wa Cardinal rules ni kiboko. Ameendesha kikao kibabe sana. Wakati Jakaya Kikwete akiwa na kalamu na karatasi akiandaa nondo za kutema kwenye mkutano huo akiamini atapewa nafasi, hakuipata.

Kilichotokea ni kuitwa Mizengo Pinda, tena bila ya Mangula kugeuka nyuma akisema kuna mtu hapa nyuma ana neno, akaita Mizengo. Baada ya Mizengo kumuombea kura Samia kilichofuata ni kuanza kupiga kura.

Naona aliona huyu ataanza kujitetea na maneno kibao huku akiomba maji ya kunywa kama ilivyokuwa kwenye mazishi ya Magufuli Chato.

Hakika siasa ni mchezo mtamu tena wenye timing nyingi sana. Leo mla timing (Jakaya) kaliwa timing kwelikweli.
 
Kwani alikuwa kwenye ratiba kwamba ataongea akaondolewa?.
 
Ni mpumbavu Pekee anayeamini kuwa Jk ana uwezo wa kupotezewa na Mangula ndani ya CCM.
Sisi tunaomfahamu mzee kikwete tunaamini kwa Sasa hakuna mwana Siasa mashuhuri aliyesalia ndani ya nchi Kama JKM,yote yaliyotokea mpaka Samia kawa raisi yeye amehusika kwa kiasi kikubwa,hapendi kujionesha.

Utawala wa mama Samia is like the reborn of JKM's Regime!utaamini hili after few years to come.
 
Jk huyu jamaa ni Nguli wa Siasa
 
Mama hajapata100%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…