Dodoma ndio Jiji lenye modern real estate kwa Tanzania

Hapo juu ni baadhi ya mji unaopatikana Dodoma, eneo linaitwa NCC Link au Tambukareli ilipo Makao Makuu ya Mahakama- Judiciary square
Watu wengi ambao hawajafika Dodoma huwa wanafikiri mji wa serikali upo Mtumba pekeyake😀😀Kiuhalisia Tambukareli ,Medeli,Njedengwa huko kote serikali imetapakaa mashirika,idara,taasisi
 
Huo ndio ukweli mkuu! Na Mwanza nayo inaenda kuwa hub ya great lakes. Dodoma bado atasubiri! Nikikuwa sijawahi kuruka kwa mwewe kwenda au kutokea Dodoma, leo jana na leo nilibahatika duh, ule mji bado sana!
 
Endelea kujifariji tu aiseee😀😀Mwanza hiihii mnayolalamika kuwa imetengwa kimaendeleo na Serikali au Mwanza nyingine😀😀
Wenzenu Dodoma kilasiku wanapendelewa kujengewa miradi mipya mfano mdogo tu Uwanja wa ndege wa kimataifa Msalato unaotarajiwa kufunguliwa mwakahuu mwishoni wakati huko Mwanza upanuzi wa uwanja wa ndege kilasiku ni stori tu tangu enzi za Magufuli 🤣🤣🤣
 
Huo ndio ukweli mkuu! Na Mwanza nayo inaenda kuwa hub ya great lakes. Dodoma bado atasubiri! Nikikuwa sijawahi kuruka kwa mwewe kwenda au kutokea Dodoma, leo jana na leo nilibahatika duh, ule mji bado sana!
Endelea kujipa false hopes
 
Eeh mkuu nipo Dodoma Kwa zaidi ya miaka 15, nilikuwa kampuni flani kama salesman kote huko nimrvuluga,yalikuwa mapori sana,jioni ikifika mafisi balaa!Nala,Vikonje,Nkuhungu,Kizota,Zuzu,Mailimbili,Chang'ombe,Area A,CD ,Ng'ong'ona,Iyumbu nk!
Mkuu nije uniuzie kiwanja?
Au ulikua unaona ni maporini tu hakutabadilika
 
Niko pale!
Kwa kukusaidia tu mradi wa Magufuli City Mtumba ndio kwanza upo awamu ya kwanza bado kuna awamu mbili zinakuja,bado kuna balozi hazijajengwa,bado kuna idara na taasisi nyingine zilizopo Dar hazijahamia Dom,bado kuna mashirika ya kimataifa hayajahamishia ofisi zao Dom.
Kwakifupi "future projects" zinazoenda Dom ni nyingi sana na kilasiku wanaongezewa mfano ujenzi wa Uwanja wa Mpira n.k
 
Unafikiri balozi zitahamia Dodoma? Hio issue labda Magu angekuwepo. Sana sana serikali na taasisi zake ndio watahamia huko ila kampuni za kimataifa sahau. Yaani waache commercial hub Dar wahamie kijiji kikubwa cha Dodoma kwa biashara ipi? Dodoma itakua ila sio kwa namna mnavyoota.
 
Balozi kuhumia Dar kuna husiana vipi na Biashara?
 
Kwa kifupi Dodoma haikwepeki saivi
 
Mpaka sasa balozi tano zimeshahamia Dodoma..ikiwepo ubalozi mdogo wa Ujerumani,Uingereza,China,Ufaransa. Uganda,Zimbabwe na Zambia wameshaanza ujenzi wa balozi.Ofisi za UN na mashirika yake mfano WFP,IOM,UN-HABITAT,FAO nk yalishahamia zamani.
Ni suala la muda tu taasisi zote za UN na balozi zote zitakua zimehamia Dodoma hata ROMA haikujengwa sikumoja
 
Watu wengi ambao hawajafika Dodoma huwa wanafikiri mji wa serikali upo Mtumba pekeyake😀😀Kiuhalisia Tambukareli ,Medeli,Njedengwa huko kote serikali imetapakaa mashirika,idara,taasisi
Dodoma ikifika 2040 huko utakua mji mzuri sana. Mji umepangwa vizuri hakuna slums wala sijui mambo ya Mkurabita. Vijana wenye kupenda kuishi miji mizuri tafuteni plots Dodoma. 👊🏿
 
Mtakubali tuu hata kabla ya Sasa mlikuwa mnasema hivyo hivyo ila Hadi mda huu hakuna Cha Mwanza Wala Arusha wa kusogeza pua.

Kadiri Dom inavyo mature ndivyo inazidi kuvuta fursa.

Dom ndio Jiji la kisasa zaidi hapa Tanzania bila kujalisha ni commercial au administrative , uwekezaji unazidi kumiminika 👇

View: https://www.instagram.com/p/DbIaYLyjL-5/?igsh=amx3MTk5M2Jyajc1
 
Wataweka ofisi zao ndogo huko no doubt.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…