Dodoma ndio Jiji lenye modern real estate kwa Tanzania

Dodoma ndio Jiji lenye modern real estate kwa Tanzania

Mkuu ulifika kweli Dom au uliishia Nyerere Square tu...😂😂😂unajua idadi ya maghorofa yaliyopo
-Magufuli City Mtumba,
-Tambukareli Government City,
-UDOM
-Medeli
-Uzunguni(kwa Waheshimiwa)
-Njedengwa Investment Area
-Kisasa

N.k
Uko ni nje, hapo nimesoma, nimepiga harakati, ukitoka Dom hotel Kuna jengo gan hapo la mana hapo town
 
Hii ni kwa waliofika mitaa ya ushuani Dodoma kwa hivi karibuni.

Naishi dsm, lakini nimeishi dodoma 5 years back, nimekaa Arusha na Mwanza pia.

Sikatai Dar ndio baba lao kwa Tz kwenye vitu vizuri hasa Makazi.
Kama umefika Dodoma hivi karibuni au hata kuangalia insta, Tiktok utaona real estate ya Dodoma inakuja kwa kasi mno hata Dar ikasome kuanzia Apartments, hotels, AirbnB etc

Hizi ni baadhi ya sehemu ambazo ukitembelea utakubaliana na mimi.

1. Itega - ianshika namba moja kwa Dodoma, wanaishi wazito huu mtaa uliopo chini ya mlima kama unaenda gereza la isanga. Sharti la kujenga ni kuanzia ghorofa moja, kiwanja kuuzwa 1 billion sio jambo la kushangazwa kutokana na value ya eneo na kumepangwa kweli kweli hiyo Mijengo Mbweni JKT akasome.

2. Njedengwa- naipa namba mbili, huu mtaa upo chini ya mlima kama unaenda iyumbu kule Udom. Kuna makazi ya watu, taasisi za umma na binafsi kama Tume ya Uchaguzi HQ. Huku kuna balaa watu wamejenga hadi unasema pesa wamepata wapi. Kwa kuongezea kuna Hotel Mbili za Nyota tano zinajengwa, ile ya Bunge la Afrika kushirikiana na Bunge Tz pamoja na ile ya NSSSF ili kuendana na kasi ya Jiji lakini kuhost diplomats, UN guests and high profile foreigners watakao kuwa dodoma msalato international airport ikikamilika.

3. Mkalama/ Makulu Oyster bay
Huu mtaa una washua balaa, kina Biteko etc wameshusha vitu na apartments zile za modern luxury zinajengwa na zingine zipo tayari.

4. Ilazo - kumenyooka huku hamna slums ni vitu fulani hivi vya kishua na barabara kiwango cha lami kwenye mitaa yake.

5. Medeli - Huku ndio kuna shopping malls, restaurants, ofisi za umma na bifnafsi na hotels za kisasa, in short panakuwa kwa kasi sana. Kiwanja kuuzwa 2 billion sio maajabu huu mtaa.

6. Kisasa- huku ni kama Sinza ya Dar, kumechangamka sana yaani ni mtaa unajitosheleza karibia kila kitu, tofauti na sinza huku hamna slums, kumepangwa vizuri barabara za mtaa almost zote zina lami.

7. Mlimwa C - huku ndio kule kwa Waziri Mkuu, chini ya mlima watu wanashusha mansion kama uyoga ndipo kuna royal village.

8. Mtumba City - kwasasa kuna modern state of art ministerial offices, ila kwa baadae patakuwa kufuru kutokana na modern hotels, restaurants and apartments ambazo zipo underway.

Sehemu zingine kuna Iyumbu, Ntyuka, Tambuka reli street etc

Dodoma Uncle magu angekuwepo sijui tungekuwa tunaongea nini.

Kwasasa ndio Jiji la tatu linalokuja kwa kasi baada ya Dar na Mwanza, hivyo Mwanza kaa tayari kushika namba tatu by 2030
Jengeni mji wenu lakini tuachieni jina la Oysterbay yetu jamani.

Unakuwaje na Oysterbay bila bahari?

Huu ushamba gani huu?
 
Uko ni nje, hapo nimesoma, nimepiga harakati, ukitoka Dom hotel Kuna jengo gan hapo la mana hapo town
nina wasiwasi hujawahi fika Dom utakua umesimuliwa tu 😅😅😅...ndiomana hujui Dodoma CBD inaishia wapi.
Kwa kukusaidia tu idadi ya maghorofa UDOM pekeyake yanakaribia 200,Magufuli City yanakaribia 100,Tambukareli zaidi ya 50,Njedengwa zaidi ya 50 na hapo bado sijakutajia ya Medeli,Miyuji Proper,Uzunguni,City Centre,Mji Mpya,Kisasa,Ilazo n.k
 
Mimi kama mkazi wa Dodoma napenda kushirikisha wadau mbalimbali juu ya fursa zilizopo.
Ujenzi kwa sasa unafanyika sana hivyo kama unajiweza kwenye kuuza vifaa vya ujenzi karibu sana Dodoma.

Sekta ingine ni Vipuri vya magari na ufundi, magari kwa sasa Dodoma ni Mengi sana nadhani kwenye top 4 Dodoma haiwezi kosekana kwa idadi kubwa ya vyombo vya usafiri ila Bajaj hatuwafikii mbeya city (kidding 😂), hivyo basi kama unajiamini katika hizo nyanja mbili dodoma kuna fursa.

Na niwashauri wafanyabiashara wapya kufanikiwa sio kuweka ma faida makubwa bali huduma nzuri zenye uendelevuuu.

Karibuni iDodomya
 
nina wasiwasi hujawahi fika Dom utakua umesimuliwa tu 😅😅😅...ndiomana hujui Dodoma CBD inaishia wapi.
Kwa kukusaidia tu idadi ya maghorofa UDOM pekeyake yanakaribia 200,Magufuli City yanakaribia 100,Tambukareli zaidi ya 50,Njedengwa zaidi ya 50 na hapo bado sijakutajia ya Medeli,Miyuji Proper,Uzunguni,City Centre,Mji Mpya,Kisasa,Ilazo n.k
Unashid wewe Hadi udom unahesabu
 
Jengeni mji wenu lakini tuachieni jina la Oysterbay yetu jamani.

Unakuwaje na Oysterbay bila bahari?

Huu ushamba gani huu?
Ushamba mwingi sana! Halafu unakuta li Mkurugenzi lipolipo tu mpaka watu wanalazimisha kuita Oysterbay Dodoma mara huko Kahama nako eti! Ujinga tu!
 
Mkuu ulifika kweli Dom au uliishia Nyerere Square tu...😂😂😂unajua idadi ya maghorofa yaliyopo
-Magufuli City Mtumba,
-Tambukareli Government City,
-UDOM
-Medeli
-Uzunguni(kwa Waheshimiwa)
-Njedengwa Investment Area
-Kisasa

N.k
Ndio nimemdokeza hapo, watu wanajua city centre Dodoma ni nyerere square 😂
Ila hapo Tambukareli NIC link 🙌
 
Ushamba mwingi sana! Halafu unakuta li Mkurugenzi lipolipo tu mpaka watu wanalazimisha kuita Oysterbay Dodoma mara huko Kahama nako eti! Ujinga tu!
Inashangaza ila bongo tunapenda inspiration kukuta hotel inaitwa Las Vegas au mtaa unaitwa Morocco, Argentina, etc ni kawaida.
 
Acha kukariri next 20 years Dodoma. ndo itakuwa habari ya mjini..Dara hataona ndani.

Dodoma inakuwa kwa kasi kuliko mji wowote hapa Tanzania. japo Wazaramo akina Kikwete wanaihujumu kwa kutopeleka miradi ya maana.

Aisee Kama.una hela kanunie hata pori 50KM from cty centre utanishukuru baadae.mimi sipo Dom ila ushauri wangu ndo huo
Dodoma sio rahisi kuipiku dar es salaam hata kidogo . Dar es salaam ndio business hub ya Tanzania na Africa mashariki . Mji wenye bandari, airport , viwanda na ni gateway ya eat and central Africa.
 
nina wasiwasi hujawahi fika Dom utakua umesimuliwa tu 😅😅😅...ndiomana hujui Dodoma CBD inaishia wapi.
Kwa kukusaidia tu idadi ya maghorofa UDOM pekeyake yanakaribia 200,Magufuli City yanakaribia 100,Tambukareli zaidi ya 50,Njedengwa zaidi ya 50 na hapo bado sijakutajia ya Medeli,Miyuji Proper,Uzunguni,City Centre,Mji Mpya,Kisasa,Ilazo n.k
Dodoma ukiishia Nyerere square ni kweli utaona hamna jipya.
Sasa sogea hapo NICC link City- Tambukareli, nenda Medeli unganisha Njedengwa pitia Kisasa nyoosha Ilazo endelea Magufuli city afu malizia na Itega 🙌 hapo utapata picha future of dodoma city.
 
Back
Top Bottom