Dodoma ndio Jiji lenye modern real estate kwa Tanzania

Dodoma ndio Jiji lenye modern real estate kwa Tanzania

Ukiwa Itega mji unauona kwa chini. Hakuna mpangilio wowote sijui ni kitongoji gani kile.
Washua ndio location zao hizo kuna limited accessibility kufika, unaogopa kufika maana hamna exit tofauti na mainroad.

Kuhusu kupangwa, nakupinga, Itega imepangwa kama mtu alichora na pencil hii unaona hata kwa drone aerial photograph, plots zote zipo well coordinated labda kama una personal biases.

Sasa mji upo mlimani ulitaka chini pasionekane?😂
 
Kwa Dar mkuu wako sahihi, imeitwa hivyo tangu enzi za ukoloni! Baada ya kuona kwenye hiyo Ghuba kuna makombe mengi!
Hawapo sahihi, tulishindwa kubadili jina baada ya ukoloni? Hii ina maana tunaishi ukoloni mambo leo
 
Area A ni mjini hapo kabisa karibu na Airport, nyuma ya Machinga au tuseme mkabala na Bahi Road au basi mkabala na Chinangali Park.
Lissu alipigiwa risasi Area D kwenye makazi ya wabunge.
Bahi road si kizota?
Hizo Area zinanichanganya zipo hadi Area E?
 
Bahi road si kizota?
Hizo Area zinanichanganya zipo hadi Area E?
Kizota ni mbali mzee, barabara ya kwenda Singida. Bahi Road ni nyuma ya Machinga sasahivi ndo niliona kuna soko dogo limejengwa la Mavunde. Hizo Area what what kweli zinachanganya inatakiwa upate wenyeji wakuelekeze vizuri. Mi napopafahamu kwa uhakika ni Area A, C na D.
 
Washua ndio location zao hizo kuna limited accessibility kufika, unaogopa kufika maana hamna exit tofauti na mainroad.

Kuhusu kupangwa, nakupinga, Itega imepangwa kama mtu alichora na pencil hii unaona hata kwa drone aerial photograph, plots zote zipo well coordinated labda kama una personal biases.

Sasa mji upo mlimani ulitaka chini pasionekane?😂
Acha ushabiki. Nineandika hivi ukiwa Itega kuna kitongoji unakiona kwa chiniji hakijapangika sijui kinaitwaje.
 
Acha ushabiki. Nineandika hivi ukiwa Itega kuna kitongoji unakiona kwa chiniji hakijapangika sijui kinaitwaje.
Ushabiki kivip?
Kwa upande wa nyuma chini kuna sehemu inaitwa Michese ndio unamaanisha?
Itega na Mbweni JKT haina tofauti kubwa.
 
Kizota ni mbali mzee, barabara ya kwenda Singida. Bahi Road ni nyuma ya Machinga sasahivi ndo niliona kuna soko dogo limejengwa la Mavunde. Hizo Area what what kweli zinachanganya inatakiwa upate wenyeji wakuelekeze vizuri. Mi napopafahamu kwa uhakika ni Area A, C na D.
Hapo nimekuelewa kuna intersection zinachanganya maana ukisogea bahi road kuna road ya Chinangali ambayo unatokea Wajenzi kama sikosei
 
Hata Dar es Salaam tu ni jina la kigeni tunatakiwa tulibadili,ziwa Victoria, Mlima Livingstone, jiwe la Bismarck etc. Majina ya kikoloni tunayo mengi.
Ni kweli, lingeitwa Ziwa Nyanza tu.
Victoria huyu malkia tunampa legacy ya kitumwa mbona kwao hukuti sehemu inaitwa Milambo, Mkwawa au Kinjiktile?
Nashukuru mlima Kilimanjaro haukupewa colonial name ni aibu we need reforms.
 
Hapo nimekuelewa kuna intersection zinachanganya maana ukisogea bahi road kuna road ya Chinangali ambayo unatokea Wajenzi kama sikosei
Hapo umenipata,sasa ukiwa unapita hiyo road ya Chinangali kuelekea Wajenzi,kushoto kwako ndo kuna Area A na Chamwino. Siku moja utembee kwa miguu ukipata nafasi,nyumba zimepangika ila zimechoka haswaa, ni za urithi warangi wanaishi humo tangu enzi.
 
Sehemu pekee tanzania nikifika najihisi kuburudika nafsi ni DODOMA. Dodoma ukipanda Treni ya SGR ndio mkoa pekee sgr inapopita ukiwa unaingia Dodoma unapata view nzuri. Ukiwa unaingia Dar na SGR Yale majengo ya Kipawa na Vingunguti unaweza kusema uko Mitaa ya Islamabad.


Dodoma nadhani ndio sehemu nitaweka uzee wangu
 
Mimi kama mkazi wa Dodoma napenda kushirikisha wadau mbalimbali juu ya fursa zilizopo.
Ujenzi kwa sasa unafanyika sana hivyo kama unajiweza kwenye kuuza vifaa vya ujenzi karibu sana Dodoma.

Sekta ingine ni Vipuri vya magari na ufundi, magari kwa sasa Dodoma ni Mengi sana nadhani kwenye top 4 Dodoma haiwezi kosekana kwa idadi kubwa ya vyombo vya usafiri ila Bajaj hatuwafikii mbeya city (kidding 😂), hivyo basi kama unajiamini katika hizo nyanja mbili dodoma kuna fursa.

Na niwashauri wafanyabiashara wapya kufanikiwa sio kuweka ma faida makubwa bali huduma nzuri zenye uendelevuuu.

Karibuni iDodomya

Mkuu mtatuzidi vyoote ila sio bajaji 😂

Kwa bajaji mbeya Tunaongoza.
 
Huo ushamba ni common disease kote Tanzania.
Ni kama Dar, unakuta hotel inaitwa Miami, Las Vegas etc just inspirational.
Hapana, huu ni zaidi.

Naona hujaelewa hoja.

Sehemu nyingi duniani kuna majina ya kuiga.

Marekani kuna Paris, kuna London, kuna Berlin, kuna Rome, kuna Athens, kuna Dublin, kuna Vienna, kuna mpaka Cairo.

Yote majina ya kuiga hayo.

Hapo sioni tatizo kwa sababu hayo ni majina ya miji tu.

Tatizo linakuja unapoita jina lenye maana mahususi, Oyster Bay, maana yake ni Ghuba ya Chaza. Sehemu yenye ghuba panapopatikana chaza, baharini.

Sasa unachukua jina la "Ghuba ya Chaza" unalipeleka Dodoma, sehemu ambayo haina ghuba wala chaza.

Huo ndio ushamba, si kuiga jina la sehemu.
 
Sehemu pekee tanzania nikifika najihisi kuburudika nafsi ni DODOMA. Dodoma ukipanda Treni ya SGR ndio mkoa pekee sgr inapopita ukiwa unaingia Dodoma unapata view nzuri. Ukiwa unaingia Dar na SGR Yale majengo ya Kipawa na Vingunguti unaweza kusema uko Mitaa ya Islamabad.


Dodoma nadhani ndio sehemu nitaweka uzee wangu
Kamalizie uzee Mwanza utakuja kunishukuru! Sato unaweza kuagiza akaja kufia kwenye chungu. Ni wewe tu!
 
Haiwezi kuipiku Mwanza hata kwa dawa! Miaka 10nijayo Mwanza inaenda kuungana na Misungwi pamoja na Magu! Sasa hivi inaelekea kuungana na Kayenze! Magorofa sasa yanavyoporomoshwa usiombe!
Kitu pekee ambacho labda Dodoma haitaipiku Mwanza ni population tu manake Wasukuma wanazaliana sana+hawanaga uzazi wa mpango😅😅 lakini vigezo vingine vyote mfano ubora wa mipangomiji, ubora wa miundombinu,ubora wa huduma za kijamii ,vyuo vikuu,maghorofa+majengo ya serikali ,mtandao mpana wa lami,uwepo wa taasisi nyingi za serikali,balozi ,mashirika ya kimataifa,makao makuu ya chama+serikali n.k MWANZA ndio ikajifunze Dodoma huo ndio ukweli mchungu
 
Back
Top Bottom