Dodoma: NEMC Kanda ya kati, kufanyia kazi Malalamiko kuhusu athari za sauti. Imekagua na kutembelea miradi 603 ya uwekezaji

Dodoma: NEMC Kanda ya kati, kufanyia kazi Malalamiko kuhusu athari za sauti. Imekagua na kutembelea miradi 603 ya uwekezaji

pantheraleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
692
Reaction score
880
Dodoma: BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Kanda ya Kati kwa kipindi cha Julai, 2024 hadi Januari, 2025, limekagua na kutembelea miradi 603 ya uwekezaji katika Mikoa ya Dodoma, Iringa na Singida ikiwa ni asilimia 75 ya makadirio kwa mwaka 2024/25.
IMG-20250204-WA0014.jpg

Kaimu Meneja wa NEMC Kanda ya Kati, Novatus Mushi ameyasema hayo jijini hapa alipokuwa akizungumzia shughuli zilizofanywa na ofisi hiyo kwa kipindi cha Julai 2024 hadi Januari 2025.

Amesema miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na miradi sita ya kimkakati ambayo Baraza limekagua na kufanya tathmini shirikishi za kufuatilia uzingatiaji wa sheria ya mazingira.

Ametaja miradi hiyo sita ni pamoja na Mradi wa Mwendokasi (SGR), Mji wa Serikali – Mtumba, Barabara ya mzunguko – Dodoma, miradi ya kilimo ya BBT,ujenzi wa bwawa la Maji-Farkwa na uwanja wa kimataifa wa ndege Msalato.

Kuhusu Tathimini ya Athari kwa Mazingira (TAM), amesema kwa hicho Ofisi ya Kanda ya Kati imesajili miradi ya maendeleo 105 na kati ya hiyo 51 imefanyiwa mapitio na kuwasilishwa kwa ajili ya kupewa vyeti vya mazingira.

Aidha, amesema vyeti 30 vilitolewa sawa na asilimia 59 ya miradi iliyowasilishwa na kufanyiwa tathmini kwa ajili ya kupewa vyeti vya mazingira.

Akizungumzia shughuli za uchimbaji wa madini, amesema uwapo wa mahitaji makubwa ya madini ujenzi katika miradi ya serikali na miradi binafsi kwa Jiji la Dodoma, umechimbaji wa madini hayo umeshamiri katika maeneo mbalimbali ya Jiji na pembezoni na hivyo kuhatarisha ustawi na jamii na mazingira.

Amesema pamoja na umuhimu wa shughuli hizo kwa uchumi wa jamii, zipo changamoto za kimazingira na kiafya zinazojitokeza kutokana na shughuli za uchimbaji ikiwemo vifo vya watu na mifugo.

Kutokana na hali hiyo, amesema NEMC imefanya ukaguzi katika maeneo ya Jiji la Dodoam na pembezoni ili kuhakikisha madhara kwa mazingira yanadhibitiwa.

Vilevile, katika Mkoa wa Singida, Ofisi ya Kanda kwa kushirikiana na kurugenzi ya utafiti chini ya Mradi wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki, imesimamia shughuli za kurejesha maeneo yaliyoharibiwa kutokana uchimbaji wa dhahabu uliofanyika katika Kijji cha Murumbi, Kata ya Mangonyi, Wilaya ya Ikungi, Mkoa wa Singida na zaidi mashimo 96 yalifukiwa.

Katika hatua nyingine, Mushi amesema asilimia 58 ya malalamiko ya kelele chafuzi yaliyopokelewa na kushughulikiwa kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2024 yanatokana na uendeshaji wa maeneo ya starehe, viwanda na nyumba za ibada.

Amesema idadi ya malalamiko yaliyosajiliwa na kufanyiwa kazi Ofisi ya Kanda kwa kipindi cha Julai -Desemba, 2024, ilipokea malalamiko 24 na kuyapatia ufumbuzi ambayo yalihusu sauti zilizozidi kiwango.

Amefafanua kuwa kati ya malalamiko yaliyowasilishwa, malalamiko yaliyohusu kelele chafuzi yalikuwa ni 14 sawa na asilimia 58 ya malalamiko yote ni ya kelele chafuzi yalihusu kelele zinazotokana na uendeshaji wa maeneo ya starehe, viwanda na nyumba za ibada na mengine 10 yalihusiana na uchafuzi na uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya Mikoa ya Dodoma, Singida na Iringa.

Hata hivyo, amesema Baraza limebaini ongezeko la kelele katika Jiji la Dodoma kutokana na kasi ya kukua kwa shughuli za kiuchumi.

“Malalamiko kuhusu athari za sauti hizo yamekuwa yakiongezeka na kwa kuzingatia afya na usalama wa wakazi wanaoishi karibu na maeneo hayo Baraza limekuwa likiainisha maeneo yaliyo katika hatari ya kupata athari zitokanazo na viwango vikubwa vya sauti ili kushauri namna bora ya kuyasimamia na kuyafuatilia.”amesema.
IMG-20250204-WA0018.jpg
IMG-20250204-WA0015.jpg
IMG-20250204-WA0016.jpg
IMG-20250204-WA0020.jpg
IMG-20250204-WA0019.jpg
IMG-20250204-WA0017.jpg
 
Back
Top Bottom