Nadhani Kuna umuhimu wa Watanzania kuwa imara,kusoma na kuelewa. Naibu katibu mkuu alichoeleza na kipo kwa maeneno na maandishi ni mabadiliko yaliyofanywa kuondoa wanafunzi wanaopanga kwenda kusomea ualimu ngazi ya cheti kwa mwaka unaoanza wa masomo.
Kwa wale ambao wamemaluza cheti na wapo uraiani au wameajiriwa watatakiwa kwa muda wao kujiendeleza wapate diploma itakayowawezesha kujiunga ngazi ya degree.
Muda wakusoma ni miaka ambapo hiki kwa uelewa wangu si kitu kipya ni kitu kinafanya kazi. Mfano Kama mnakumbuka wanafunzi aliwahi kuwaita kilaza waliokuwa wanasoma UDOM wakaondolewa, Hawa wanafunzi walimaliza kidato Cha nne wakapelekwa kusoma diploma miaka mitatu na wapo mtaani.
Sijaelewa tunaposema Rais amekataza mnatuaminisha amekataza kipi? Amekataza watu wanaomaliza kidato Cha nne kuendelea kusoma diploma miaka mitatu Kama utaratibu ulivyo Sasa au amefuta mfumo wa kusomea cheti ambao tulishaachana nao?
Lakini pia haya Mambo unapoyakataa huoni Kama unapingana na sera ya elimu ya nchi?
Nadhani kwenye elimu tukiendelea kutumia siasa wanayofanya chama Cha walimu tunakwenda kuitumbukiza shimoni hii taaluma. Tujiulize hiyo simu iliyopigwa kwenye kikao kwanini ipigwe leo? Kwanini tangazo litoke leo? Kwamba Naibu Katibu Mkuu anaweza kutangaza Jambo Kama hili bila Baraza la Mawaziri kufahamu?
Elimu yetu ikiendelea kuendeshwa kwa matamko tutarudi walipotutumbukiza akina Mungai kufuta michezo na Mlongo kuunganisha physics na chemistry