Dodoma: Rais Magufuli apiga simu mubashara kwenye Kongamano la CWT na kukanusha kufutwa kwa Ualimu Ngazi ya Cheti

Dodoma: Rais Magufuli apiga simu mubashara kwenye Kongamano la CWT na kukanusha kufutwa kwa Ualimu Ngazi ya Cheti

Unamuita daktari mpumbavu? jamani? unafuta kwa kauli tu? hapana si sawa!! mamlaka zikanushe kwa tangazo na waweke saini kama alivyofanya Dkt Ave
Ilianza kwa Kabudi kuitwa mpumbavu sasa aona ameota mapembe juzi kati kawatukana Tunduma naona atakuja kututukana Watanzania wote Wasengerema hapo ni malezi aliyo kulia kutikana nduguzake wa kuzaliwa haswa marehemu dada yake.
 
Yaani Naibu waziri siku zote tangu ateuliwe hakuwahi kuliona hili la walimu wenye daraja la cheti? maana kuna muda kama kuna watu huwa wanatolewa kafara ili mambo yaende sawia.

Wiki kama mbili zilizopita ilitolewa taarifa juu ya walimu watakaosomea ngazi hiyo ya cheti na kutangazwa kutokuendelea kutolewa elimu hiyo. Yaani swali hapa ni jinsi haya matukio yanavyoendana kwasababu baada ya wiki kuna maadhimisho ya walimu.

Yaani watu wametolewa kwenye mstari wa kudai maslahi yao muhimu na yote ni baada ya kukutoa katika mstari na kuanza kukufikirisha mengine kabisa juu ya elimu ya cheti.

Mimi naamini haya matukio ni planned from the beggining, na wala sio coincidence. kama kuna tukio lingine sio mbaya ukishare nasi.
 
Kawa dhalilisha mama Janet na Majaliwa kwa vyeti walivyo dumaa navyo pasipo kujiendeleza
 
Yaani Naibu waziri siku zote tangu ateuliwe hakuwahi kuliona hili la walimu wenye daraja la cheti? maana kuna muda kama kuna watu huwa wanatolewa kafara ili mambo yaende sawia...
Najiuliza kosa lake ni tamko alilotoa?

Kama ni tamko, je alitoka nalo nyumbani kwake au lilikuwa ni tamko la wizara?

Kama ni wizara je yuko peke yake? au kuna kitu hakutamka sawasawa?
 
Maskini Naibu Katibu Mkuu. Kama ulikuwa kwenye nyumba ya Serikali, Anza mipango fasta ya kuhama!?
Uzuri wa nyumba zao unatoka kama unakwenda kusalimu ndugu, ni wewe na nguo zako.
 
Ukiangalia kwa jicho la tatu sio uamuzi wa kipumbavu kama alivyosema yeye, ingekuza kiwango cha elimu lakini imekuwa wazo la kipumbavu kwake kwa maana yupo kwenye kampeni na atakosa kura ndo maana kapiga simu live.

Ingawa wengi watakosa ajira lakini siyo wazo la kipumbavu angetumia maneno ya busara kidogo.
Busara na jiwe wapi na wapi?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Yaani Naibu waziri siku zote tangu ateuliwe hakuwahi kuliona hili la walimu wenye daraja la cheti? maana kuna muda kama kuna watu huwa wanatolewa kafara ili mambo yaende sawia...
Na wale wakufunzi walikuwa kwenye refresher course 350 kutoka vyuo 18 waliwapeleka kwa ajili ya nini?
 
Kama ni barua niliyoiona mtandaoni basi nimeshangaa kwamba kulikuwa na taharuki ya walimu. Mbona iko wazi kuwa ajira zao bado zitatambuliwa? Kuna shida gani hapo? Tuelimishane jamani
 
Kuna sababu ya msingi kwanini leo kuna wajinga wengi kuliko mia ya nyuma!! Ubora wa elimu umezidi kushuka.

Badala ya kuongeza vigezo na viwango vya waalimu, tunavishusha au tukivibakiza palepale - huku tukiiacha technolojia iende zake!!!

Tunakosea sana na waathirika wa hilo ni watoto wa wanyonge! Wazazi wanaopeleka watoto shule binafsi wanaweza kutambua hili!
 
Kwani Raisi wa Malawi huyu mpya alitangazwa na tume ipi??? Si ile ile ya Mutharika!! Nguvu ya umma haijawai kufeli duniani
Tanzania hamna kitu km hicho, box la kura haliwezi leta mabadiliko yoyote katika uchaguz
 
Back
Top Bottom