Maelezo mazuri mkuu.
Tukiendelea hivi JF itakuwa na manufaa zaidi kwa wengi.
Na ili ieleweke vizuri zaidi, pamoja na IAA kushirikiana na TMA kuandaa mtaala (pamoja na kufundisha?); huo mtaala unahusu masomo ya "Military Science" na siyo ya uhasibu, au siyo?
Bado ninatatizwa kidogo na uhusiano wa masomo ya kijeshi na Uhasibu.
Ninaelewa vyema sana kuwepo kwa uhitaji kijeshi kwa baadhi ya masomo ya kiuhasibu, lakini mtaala ambao sehemu kubwa ni uhasibu kwa masomo ya kijeshi, hapo ninatatizwa.
Labda itabidi tutafute ni kipi hasa kinachofahamika kuwa "Military Science", ikilazimu tutafanya hivyo.
Naomba nikueleze kitu kimoja ambacho kimebadilika sana kwenye vyuo vingi sana nchini
IFM,TIA,IAA vilikua ni vyuo vya uhasibu zaidi ila sasa hivi wanatoa digrii nyingine nyingi pia tofauti na uhasibu japokua wamejikita zaidi kwenye uhasibu
Hata SUA chenyewe tunachojua ni cha kilimo kina degree nyingine hata hazihusiani na kilimo/ufugaji
Sasa kwa jinsi ninavyodhani mimi(Sina uhakika)
1. Kwanza walichukulia kutafuta partner ambaye yuko karibu kieneo(Geographically) kwahiyo wakajikuta na IAA tu pale Arusha
2. Nadhani pia katika kuandaa modules sana sana watakua na sheria humo, DS ,Utawala,ICT, Hesabu,Lugha nk nk na hawa wakufunzi wanapatikana IAA(kwakua kuna haya masomo pale)
3. Wakufunzi wa TMA wenyewe wanabakia kukazia katika masomo yao ya medani kama Commanding/Leadership, Shooting,navigation, endurance no nk(Hapa nadhani na hawa wakufunzi pia walikula semina za kiraia/Za kule NDC au hata nje nchi) ili kuwa na kiwango cha kutoa hadhi ya BSc
Sidhani kwa vyovyote vile kama inahusiana na Uhasibu hata kidogo(Chuo cha Uhasibu kimabaki jina tu)
Nje ya mada: Hata mkuu wa chuo cha IAA yule Sedo aliyeongea jana pale Chamwino na ndio amesifiwa kwa kukibadilisha sana hiki chuo sio Muhasibu hata kidogo. Nimesoma nae Computer Science miaka mingi iliyopiata(Advance Diploma) na mpaka kaenda nje kufanya PhD ya IT ila ndo mkuu wa chuo cha "Uhasibu"
Kuna jamaa humu alisoma Bsc Military Science Pretoria ngoja nimuombe aje kabla sijamtag atuambie