Dodoma: Serikali yakiri Watu kushangilia Kifo cha Ndugai, ila yasema itawaeleza vijana kwamba hilo si jambo zuri

Dodoma: Serikali yakiri Watu kushangilia Kifo cha Ndugai, ila yasema itawaeleza vijana kwamba hilo si jambo zuri

Jibu Ni rahisi Sana. Ni ishara ya uadui wa wazi na utengano uliopo Kati ya viongozi wa serikali na wananchi. Tumezoea kushuhudia haya kwa Siri Sana kwa watu labda wachawi, majambazi nk. Inapofikia kwa kiongozi mkubwa wa Kariba yake Ni ishara mbaya Sana kwa mustakabali wa taifa.
 
Hivi ndivyo alivyoeleza Mkuu wa Wilaya ya Kongwa.

Zaidi huyu hapa

Swali letu ni hili, unadhani kwanini kifo cha Ndugai kimeshangiliwa badala ya kuwa Huzuni kama Marehemu wengine wanapofariki akiwemo Maalim Seif na Ally Kibao?
======================

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Saimon Mayeka, amekemea baadhi ya watu kushangilia kifo cha Spika mstaafu Job Ndugai kilichotokea jana Agosti 06, 2025.

Soma Pia: Wananchi wakutana kushangilia kifo cha Ndugai!

DC Saimon amesema baada ya msiba, atazungumza na vijana hao ili kuwarekebisha huku akiwaomba wazazi kukemea tabia hiyo.

Eti wazazi wawakemee! Laiti angejua wazazi ndiyo waliamrisha watoto wakashangilie ...
 
Na hyo n advertise tu
Wakumbuke mwishon n kama marehemu alijaribu kutubu
Sasa saa inakuja ambapo Kuna atakayeanguka na shangwe lake litakuwa si la kawaida
Nb Mimi sio muumin wa hizi shangwe wakat wa msiba ila viongozi wetu mnatakiwa kujitafakari wapi mlipokosea
 
Jibu Ni rahisi Sana. Ni ishara ya uadui wa wazi na utengano uliopo Kati ya viongozi wa serikali na wananchi. Tumezoea kushuhudia haya kwa Siri Sana kwa watu labda wachawi, majambazi nk. Inapofikia kwa kiongozi mkubwa wa Kariba yake Ni ishara mbaya Sana kwa mustakabali wa taifa.
Nakuapia asilimia 80 ya wabunge wa sasa wakipatwa na jambo kama hilo watu watashangilia. Siyo wabunge tu, ila ni viongozi wote wa kiserekali na chama. Sijui hawaoni hii hali warekebishe mambo....
 
Huyu mjinga anasema hakuna uadui wa hivyo? Yaani mnatuteka mnatuua halafu mkifa mnataka tulie.
Nyie ni maadui wetu,vifo vyenu ni furaha Kwa wanyonge mnaowanyanyasa na hawawezi kujitetea
 
Back
Top Bottom