MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 305
- 728
Spika wa Bunge Job Ndugai, amemuagiza Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika, kuandika barua ambayo ataambatanisha na katiba ya chama chake pamoja muhtasari wa kikao kilichofanya maamuzi ya kuwafukuza uanachama wabunge 19 wa chama hicho.
"Aandike barua aambatanishe na katiba ya chama chake, aniambatanishie na muhtasari wa hicho kikao kilichofanya hayo maamuzi, inawezekana huyo Katibu Mkuu kaamka tu kaandika halafu na mimi nakurupuka nachukua hatua, nitakua ni Spika au kitu cha ajabu, hivyo andika ili ile barua niwape watalam waangalie, halafu namuuliza msajili wa chama hawa wajumbe walioorodheshwa ndiyo wajumbe halisi?", amesema Spika Ndugai
"Pia naangalia kwenye muhtasari ule je hawa wabunge wanaotuhumiwa kufukuzwa walipata nafasi hata ya kujieleza na walisikilizwa?, nifukuze watu ambao hawakusikilizwa popote, yaani mbunge hujawahi kusikilizwa wanandika tu fukuza hawa, viko vyama vimejaa mfumo dume, kundi la wanaume wamekaa wanafukuza wanawake 19 kwa mpigo hata kama barua hiyo inatoka CCM lazima nitawaambia 'stop' kwanza taratibu", ameongeza Spika Ndugai.