Kuna kitu kinaitwa precedence. Kama kila wakati ulikuwa unafanyia kazi barua bila kudai viambatisho hivyo, ukija vidai kwa mtu mwingine ni dhahiri utaonekana una lake jambo.
Na taratibu ni kuwa unapopokea barua kama hiyo ambayo unaona imekosa viambatisho ni kuwa unamwandikia aliyekuandikia ile barua kuwa hauwezi kuifanyia kazi kwa sababu ina mapungufu kadha wa kadha. Kukaa kimya bila kuijibu maana yake ni kuwa umeipokea na umeridhika kuwa imekamilika. Hii kuamka bungeni na kutoa sababu zisizo na kichwa wale mbele ni kutaka kuonyesha ubabe tu. Hawasaidii wakina Halima bali anazidi kuwafukia
Aidha, haya majibu yanatakiwa yatoke NEC sio kwake. NEC ndio wanaomtangaza mtu kuwa mbunge au la. Yeye alitakiwa awaambie NEC na hao ndio waseme kuwa wanawatambua wakina Halima kuwa wabunge halalali kwa sababu kadha wa kadha.
Amandla...