Ndugai hajielewi kabisa, anajidai kuwafundisha Chadema nini cha kufanya kama vile hiyo ndio mara ya kwanza jambo kama hilo kutokea.
Lakini ukimsoma mbele zaidi anadai hawezi kufukuza watu ambao hawakupewa nafasi ya kujitetea, sasa kama waliitwa wakagoma kwenda alitaka wabebwe mgongoni?
Anaonesha wazi alivyoamua kuwalinda hao wanawake kwa gharama yoyote, ila ajue kwa hiki alichofanya anajiondolea heshima.
Amejidhalilisha mwenyewe, amelidhalilisha bunge kama taasisi inayotunga sheria, zaidi ameonesha hizo sheria wanazotunga bungeni hazina maana, pia kaidharau Katiba ya nchi, ni bora ajiuluzu ili kulirudishia bunge letu na yeye mwenyewe heshima yake.