Dodoma: Tundu Lissu afuata gari lake lililoshambuliwa ofisini kwa RPC Muroto. Ashangaa hadi sasa hajahojiwa yeye na Dereva wake

Wanaweza kumjibu? Wao kila swali wanaloulizwa wanajibu "esijiara, sitigilazi, zahanati 400, ndege na flayiova" huo ndiyo wimbo wanaoimbia kila mtu. Swali lolote wanaloulizwa majibu ndiyo hayo
Selikali iko busy kuhudumia wanachi, haiwezi kupoteza muda jujibizana na kina Lisu.
Lisu atajibiwa na polepole ambae nae kwa bahati mbaya yuko busy kupanga mikakati ya ushindi huko field.

So Lisu mwache abwabwaje pekeake akichoka ataacha.
 
Hahahah huyu mgonjwa amekuwa kitukp kweli sasa kajipeleka ana shangaa hawajamuhoji wakati hakuwepo na alisha sema kuwa wao ndio walimshambulia sasa sijui anataka wamuhoji nini wakati majibu anayo mkononi hahahaha mgonjwa bwana

acha kumuita mwenzio hivo mkuu,maisha hujayamaliza bado be humble,umemuita β€œmgonjwa” sio kwa nia nzuri bali kama kumsimanga hivi au kumkejeli,unaweza ukapata ajali kesho ukawa kiwete
 
Polisi hawana time ya kumpa kiki Lisu maana wanajua kura atakazopata Lisu hazitazidi kwa Hashimu Rungwe
 
Mh.Lissu kamanda usiye choka..
~Kamanda unayepigana hadi tone la mwisho
~Kamanda wa haki
~Kamanda unayesubiri kuapishwa kuwa Amiri Jeshi na rais wa nchi

nakuomba kama itakupendeza na hasa ukishaapishwa unipe hilo gari! Amina

*mlio karibu naye Mh.TAL mfikishieni ombi langu.
 
Hahahah huyu mgonjwa amekuwa kitukp kweli sasa kajipeleka ana shangaa hawajamuhoji wakati hakuwepo na alisha sema kuwa wao ndio walimshambulia sasa sijui anataka wamuhoji nini wakati majibu anayo mkononi hahahaha mgonjwa bwana
Msije mkamwacha mwuaji wenu akayakabili Mateso peke yake maana huku kwenye mitandao mnajifanya mnamkingia kifua, msiojulikana mtajulikana pumbavu
 
Huna lolote we Mamluki
angalia hii
 
Lissu km Lissu...... Watamtambua huyu nabii alyeteuliwa na Mungu kulikomboa Tanzania inayoangamia
 
Hii kesi ina moto!! Robert katishia kuwaomba UN waje kupeleleza pamoja na mambo mengine ya waliopotea na wengine kutekwa.

Kinachosubiriwa ni trigger tu ili mambo yaanze rasmi.

Hii si habari nzuri!!
UN ipi?? Unaelewa ulichokiandika?
 
..afande Sirro alisema wapelelezi wake wanamtafuta TL lakini hawajampata.

..sasa leo TL kaenda mpaka kituoni kilichowashinda kumkamata na kumhoji ni nini?
Tunampa hadhi ya juu,mgombea wa urais Kwa tiketi ya chama cha chadema,au yeye atambui nafasi anayo wania.,....
Na aonyeshe tabia kama mgombea wa kiti cha uraisi...
Aache sasa kuonyesha tabia za uharakati..
Sisi tutaendelea kumjali kumpa stahiki kama mgombea mwingine wa chama kingine na yeye mshaurini aonyeshe tabia inayoendana na nafasi anayo gombania
 
Kalifuata au kaenda kuliangalia?!
Hahahah huyu mgonjwa amekuwa kitukp kweli sasa kajipeleka ana shangaa hawajamuhoji wakati hakuwepo na alisha sema kuwa wao ndio walimshambulia sasa sijui anataka wamuhoji nini wakati majibu anayo mkononi hahahaha mgonjwa bwana
Kila kitengo hujiendesha Kwa kanuni na taratibu zake, haiwezekani mtu kutoka anakokujua Yeye atake matakwa yake Yeye yafuatwe!! Utakuwa upumbavu

Honestly, nyie watatu ingalau πŸ‘† πŸ‘†πŸ‘†πŸ‘† kuna shida ya ufahamu ktk bongo zetu....

Nimejaribu kupata logic ya hoja zenu, nimeshindwa kuona kama zina connection na mada zaidi tu kwamba ni maandishi tu yasiyo na substance ndani yake....

Kwa sababu mantiki iliyo ktk maelezo ya msingi ya mada hii ni:

βˆšβ€’ Jamaa (yeye mwenyewe - Tundu Lissu), baada ya kuona hakuna uchunguzi unaoendelea kwenye ishu hii ameamua kwenda kuomba apewe gari lake ili maisha yaendelee....

βˆšβ€’ Tena ni baada ya "..utaratibu wa kawaida kulipata kwa njia zingine " kushindikana. Kwa statement hii inaonesha wazi kuwa kumbe kulikuwa na mawasiliano yanaendelea kati ya muathirika wa unyama ule na jeshi la polisi)....

βˆšβ€’ In response, SACP Muroto akajibu kusema, jeshi linahitaji muda zaidi kujiandaa kumkabidhi gari hilo kwake....

βˆšβ€’ Sambamba na hilo, SACP Muroto akachomokea na ishu ya kutaka maelezo ya mwathirika (Tundu Lissu) kuhusu shambulio hilo (miaka mitatu iliyopita!!) something very ridiculous, right?

βˆšβ€’ In response, Tundu Lissu akamwambia, hakuna shida. Yuko tayari kutoa maelezo yake polisi kwa trh na muda mwafaka kwa pande zote.....

βˆšβ€’ Lakini wakati huohuo TL akaonesha mshangao wake kwa jeshi hilo kupitia SACP Muroto kwa kushindwa kumhoji yeye na dereva wake kwa miaka mitatu sasa baada ya shambulio licha ya Jeshi hilo kuwa limewataarifu Lissu na dereva wake kuwa wangeenda kuwahoji na kuchukua maelezo yao walipokuwa Nairobi Hospital - Kenya....

Lakini in very surprising circumstances, Polisi wakaingia mitini na baada ya hapo zikafuata mfululizo wa kauli za kisiasa kwa polisi wetu hawa huku wakiitupa sheria kule....

BAADA YA MAELEZO HAYA....

Hebu nyie watatu tuambieni hoja zenu ni nini? Mimi nawaona kama vile nyie siyo watu mnaotumia akili kufikiri. Ni kama maroboti fulani hivi....

Yaani mmeshindwa hata kung'amua kuwa hii "move" ya Tundu Lissu ina lengo maalumu la kuliweka Jeshi la polisi kwenye target yake.....

Na polisi wapende au wasipende wataingia tu (na ofcoz walishaingia wenyewe kwa hiari yao kitambo tu)...

Kwa sababu Polisi wanapoacha kufanya kazi yao au kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria badala yake wanafuata maelekezo ya kisiasa yasiyozingatia sheria zinazoongoza utendaji kazi wao kutoka kwa mabosi wao "raia" baki kabisa kina Makonda ama Magufuli, tayari ni KUPOTEA KWA KIWANGO CHA JUU SANA....!!
 
Najaribu kufikiria mazungumzo kati ya Lissu na Afande

Lissu : Afande habari za kazi

Afande: Nzuri karibu

Lissu :Nimeelezwa gari yangu namba XYZ ipo hapa kituoni kwako toka tarehe ABC mwaka 2017 kweli si kweli

Afande : Sahihi kabisa, gari hilo tunalo

Lissu : Kwa nini liko hapa?

Afande: Mm tulilichukua kutoka na tukio la uhalifu la mmiliki wake kushambuliwa tarehe hiyo akiwa ndani yake, tumelishikilia kwa ajili ya uchunguzi

Lissu : Uchunguzi umefikia wapi?

Afande : Kimya, Anazuga kumuita Afande Manywele

Lissu : Labda hukunisikia, nauliza tena uchunguzi umefikia wapi?

Afande : Tupo kwenye mchakato wa kuchunguza, tulikuwa tunangoja urudi tuchunguze

Lissu : Ningekufa je ina maana msingechunguza

Afande : Kimya

Lissu : Afande mbona hunijibu

Afande : Hayo mambo ya kufa achana nayo, maadamu hukufa ni jambo jema

Lissu : Nahitaji kutoa maelezo ya shambulizi dhidi yangu ili yasaidie uchunguzi

Afande : Kigugumizi, anashika hiki mara anashika kile, anatoa leso anajifuta..
mmh eeh mhhh mheshimiwa subiri kidogo tua... tuanda.. tuandae utaratibu mzuri wa jambo hilo

Lissu : Si ni jukumu la raia kutoa taarifa za uhalifu kwa mujibu wa katiba ibara ya XYZ na sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kifungu namba PQR?

Afande : Ni kweli mheshimiwa

Lissu : Sasa mbona unajivutavuta mimi kutimiza wajibu wangu wa kisheria wa kuripoti tukio la kihalifu dhidi yangu?

Mara simu kutoka mamlaka za juu inaita, Afande anaenda kuisikiiza, kisha anarudi

Afande : Mheshimiwa haya mambo unayoyauliza kwa kweli yako nje ya uwezo wangu

Lissu : Gari naweza kulichukua lini?

Afande : Muda wowote tutakuandalia utaratibu

Lissu : Hata kama uchunguzi haujakamilia naweza kulichukua?

Afande : Kimya

Lissu anamwambia Salum Mwalimu : Makamu wa rais turudi kwenye ofisi za chama chetu tukajiandae na kampeni, Safari hii CCM wamekwisha, tukajadili namna ya kuboresha maslahi ya watumishi wa umma, ajira kwa vijana wetu, kueta katiba mpya na bora, kupambana na ufisadi kwa dhati, Maslahi ya mkulima, utawala bora, kuondoa tatizo la TRA kubambikizia wafanyabiashara kodi, kurejesha na kupanua demokrasia, kuwalipa kifuta machozi waliobomolewa nyumba kikatili, kuheshimu na kuwezesha wanawake, kuboresha mpango wa gesi, kusaidia wavuvi, kupunguza rate ya marejesho bodi ya mikopo, kuboresha diplomasia yetu, kuondoa tatizo la lishe duni kwa watoto wetu.

Salum Mwalimu : Nimekuelewa mheshimiwa rais, twende tukapange mipango ya kuomba ridhaa kwa wananchi, Tafadhali usisahau Zanzibar yenye mamlaka kamili.

Lissu : Hilo tutalishughulikia kwenye katiba mpya

Lissu na Mwalimu wanatokomea zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…