Najaribu kufikiria mazungumzo kati ya Lissu na Afande
Lissu : Afande habari za kazi
Afande: Nzuri karibu
Lissu :Nimeelezwa gari yangu namba XYZ ipo hapa kituoni kwako toka tarehe ABC mwaka 2017 kweli si kweli
Afande : Sahihi kabisa, gari hilo tunalo
Lissu : Kwa nini liko hapa?
Afande: Mm tulilichukua kutoka na tukio la uhalifu la mmiliki wake kushambuliwa tarehe hiyo akiwa ndani yake, tumelishiilia kwa ajili ya uchunguzi
Lissu : Uchunguzi umefikia wapi?
Afande : Kimya, Anazuga kumuita Afande Manywele
Lissu : Labda hukunisikia, nauliza tena uchunguzi umefikia wapi?
Afande : Tupo kwenye mchakato wa kuchunguza, tulikuwa tunangoja urudi tuchunguze
Lissu : Ningekufa je ina maana msingechunguza
Afande : Kimya
Lissu : Afande mbona hunijibu
Afande : Hayo mambo ya kufa achana nayo, maadamu hukufa ni jambo jema
Lissu : Nahitaji kutoa maelezo ya shambulizi dhidi yangu ili yasaidie uchunguzi
Afande : Kigugumizi, anashika hiki mara anashika kile, anatoa leso anajifuta..
mmh eeh mhhh mheshimiwa subiri kidogo tua... tuanda.. tuandae utaratibu mzuri wa jambo hilo
Lissu : Si ni jukumu la raia kutoa taarifa za uhalifu kwa mujibu wa katiba ibara ya XYZ na sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kifungu namba PQR?
Afande : Ni kweli mheshimiwa
Lissu : Sasa mbona unajivutavuta mimi kutimiza wajibu wangu wa kisheria wa kuripoti tukio la kihalifu dhidi yangu?
Mara simu kutoka mamlaka za juu inaita, Afande anaenda kuisikiiza, kisha anarudi
Afande : Mheshimiwa haya mambo unayoyauliza kwa kweli yako nje ya uwezo wangu
Lissu : Gari naweza kulichukua lini?
Afande : Muda wowote tutakuandalia utaratibu
Lissu : Hata kama uchunguzi haujakamilia naweza kulichukua?
Afande : Kimya
Lissu anamwambia Salum Mwalimu : Makamu wa rais turudi kwenye ofisi za chama chetu tukajiandae na kampeni, Safari hii CCM wamekwisha, tukajadili namna ya kuboresha maslahi ya watumishi wa umma, ajira kwa vijana wetu, kueta katiba mpya na bora, kupambana na ufisadi kwa dhati, Maslahi ya mkulima, utawala bora, kuondoa tatizo la TRA kubambikizia wafanyabiashara kodi, kurejesha na kupanua demokrasia, kuwalipa kifuta machozi waliobomolewa nyumba kikatili, kuheshimu na kuwezesha wanawake, kuboresha mpango wa gesi, kusaidia wavuvi, kupunguza rate ya marejesho bodi ya mikopo, kuboresha diplomasia yetu, kuondoa tatizo la lishe duni kwa watoto wetu.
Salum Mwalimu : Nimekuelewa mheshimiwa rais, twende tukapange mipango ya kuomba ridhaa kwa wananchi, Tafadhali usisahau Zanzibar yenye mamlaka kamili
Lissu na Mwalimu wanatokomea zao