Dodoma: Tundu Lissu afuata gari lake lililoshambuliwa ofisini kwa RPC Muroto. Ashangaa hadi sasa hajahojiwa yeye na Dereva wake

Kinachofuata atajipiga kisu huyu ili kuamsha hisia tu,maana kila anapogusa watu wamemchunia
😂😂😂na akisema ajidhuru au kujiteka tuu atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria
 
Anachotafuta kwa sasa Ni sympathy,ananjijua hana uwezo wa kawaida wa kumshinda Magufuli,Leo kajipeleka polisi,kesho atavamia bunge kufuata documents zake ili mradi tu apate KUKAMATWA!
 
Duh!! Lissu is quite a Dude aisee!
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

Mgombea Urais wa JMT kwa tiketi ya CHADEMA, Mh. Tundu Lissu, leo ametembelea Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuchukua gari lake ambalo limehifadhiwa na Jeshi la Polisi Mkoa huo jaribio la mauaji dhidi ya Mh. Lissu la tarehe 7 September 2017.

Mh. Lissu aliambatana na mgombea mwenza wake Mh. Salum Mwalimu na alipokelewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP Giles Muroto.

Katika mazungumzo yake na SACP Muroto, Mh. Lissu alisema kwamba ameamua kuja yeye mwenyewe baada ya utaratibu wa kulipata hilo kwa njia zingine kushindikana.

Kwa upande wake, SACP Muroto alimweleza Mh. Lissu kwamba Jeshi la Polisi mkoani hapo linahitaji muda zaidi ili kujiandaa kulikabidhi gari hilo kwake.

Aidha, SACP Muroto alimweleza Mh Lissu kwamba Jeshi la Polisi linamhitaji atoe maelezo kwa Jeshi la Polisi kuhusu kushambuliwa kwake September 2017.

Mh. Lissu alijibu kwamba yeye yuko tayari kutoa maelezo polisi kwa tarehe na muda utakaokuwa muafaka kwa pande zote mbili.

Mh. Lissu alisisitiza mshangao wake kwamba hadi sasa, takriban miaka mitatu tangu kushambuliwa kwake, Jeshi la Polisi halijafanya uchunguzi wowote, ikiwemo kumhoji yeye na dereva wake Adam Bakari Mohamed, licha ya kuahidi kwamba lingefanya tangu Mh. Lissu akiwa hospitalini nchini Kenya.

Imetolewa leo Alhamis, Agosti 27, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
 
Anachotafuta kwa sasa Ni sympathy,ananjijua hana uwezo wa kawaida wa kumshinda Magufuli,Leo kajipeleka polisi,kesho atavamia bunge kufuata documents zake ili mradi tu apate KUKAMATWA!
Kuna mtu amekuomba usympasize nae!?
 
Anachotafuta kwa sasa Ni sympathy,ananjijua hana uwezo wa kawaida wa kumshinda Magufuli,Leo kajipeleka polisi,kesho atavamia bunge kufuata documents zake ili mradi tu apate KUKAMATWA!
Atajichosha sana🤣🤣🤣
 
Hahahah huyu mgonjwa amekuwa kitukp kweli sasa kajipeleka ana shangaa hawajamuhoji wakati hakuwepo na alisha sema kuwa wao ndio walimshambulia sasa sijui anataka wamuhoji nini wakati majibu anayo mkononi hahahaha mgonjwa bwana
unakosa hoja hadi unajichekeshachekesha hovyo.
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

Mgombea Urais wa JMT kwa tiketi ya CHADEMA, Mh. Tundu Lissu, leo ametembelea Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuchukua gari lake ambalo limehifadhiwa na Jeshi la Polisi Mkoa huo jaribio la mauaji dhidi ya Mh. Lissu la tarehe 7 September 2017.

Mh. Lissu aliambatana na mgombea mwenza wake Mh. Salum Mwalimu na alipokelewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP Giles Muroto.

Katika mazungumzo yake na SACP Muroto, Mh. Lissu alisema kwamba ameamua kuja yeye mwenyewe baada ya utaratibu wa kulipata hilo kwa njia zingine kushindikana.

Kwa upande wake, SACP Muroto alimweleza Mh. Lissu kwamba Jeshi la Polisi mkoani hapo linahitaji muda zaidi ili kujiandaa kulikabidhi gari hilo kwake.

Aidha, SACP Muroto alimweleza Mh Lissu kwamba Jeshi la Polisi linamhitaji atoe maelezo kwa Jeshi la Polisi kuhusu kushambuliwa kwake September 2017.

Mh. Lissu alijibu kwamba yeye yuko tayari kutoa maelezo polisi kwa tarehe na muda utakaokuwa muafaka kwa pande zote mbili.

Mh. Lissu alisisitiza mshangao wake kwamba hadi sasa, takriban miaka mitatu tangu kushambuliwa kwake, Jeshi la Polisi halijafanya uchunguzi wowote, ikiwemo kumhoji yeye na dereva wake Adam Bakari Mohamed, licha ya kuahidi kwamba lingefanya tangu Mh. Lissu akiwa hospitalini nchini Kenya.

Imetolewa leo Alhamis, Agosti 27, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Lisu huu ujasiri wa kum face kiongozi yoyote wa serikali anautoa wapi ?

I wish watanzania wote tungekuwa tunajitambua na majasiri kama Tundu Anthipas Lissu, msomi mbobezi wa sheria na haki za watu.

Leo tusingekuwa tunashangilia ujinga ujinga pale serikali inapotekeleza wajibu kama kuimarisha miundombinu.
 
thetallest, Sasa hapo kuna kiki gan mkuu? Yeye kaenda polisi ili wamuhoji ambapo polisi walisema hatoi ushirikiano yeye kaleta ushirikiano wewe unasema anataka kiki

Ulipaswa kumpongeza mkuu kwa ushirikiano wake wa polisi maana wale polisi iliyowaita wasiojulikana sasa inabidi wajulikane maana ushirikiano kwa pande zote mbili sasa unapatikana
Bladha naona jamaa imembidi ahisi kajinyea mpaka kuifuta comment😂😂
 
  • Thanks
Reactions: jme
Ati anashangaaa!!!.. kibaraka akumbuke ana kesi.. huyu ni hatari sana.. hata mwili wake.. hakukumbuka ya gari.. hadi kamaliza kukamilisha ubaraka wake aliotumwa na mabeberu.. hafai kuwa kiongozi wa nchi hii hata kwa sekunde moja.. tukisema ilikuwa mipango yao wenyewe.. bado munapiga kelele. Ati nini!!![emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Magufuli 2020 [emoji817]
Kweli aise, cheki walivyo waondoa walinzi siku ile na baadaye kung'oa cctv camera [emoji23][emoji23]
 
Kila kitengo hujiendesha Kwa kanuni na taratibu zake, haiwezekani mtu kutoka anakokujua Yeye atake matakwa yake Yeye yafuatwe!! Utakuwa upumbavu
Hapo Lisu anatega mtego serikali ikitegeka itanasa kweli kweli na kumfukia John mazima. Siwaambii mtego gani umetegwa. Lumumba mtajibeba mwaka huu.
 
Lissu ni mjinga bahati mbaya kawaambukiza ujinga na watu wanaomwabudu anachofanya ni kutaka attention huyo dereva wake anaomzungumzia yuko wapi , pamoja na kuichukia ccm lakini siwezi kumpa Lissu kura yangu
 
Hahahah huyu mgonjwa amekuwa kitukp kweli sasa kajipeleka ana shangaa hawajamuhoji wakati hakuwepo na alisha sema kuwa wao ndio walimshambulia sasa sijui anataka wamuhoji nini wakati majibu anayo mkononi hahahaha mgonjwa bwana
kweli ukiwa ccm unakuwa Lofa hivi hujui kuna technolojia ya kuhojiana hata mtu akiwa mbali na wewe inaitwa kwa njia ya simu??? au telecomferencing!? wangeweza kumuhoji hata kama alikuwa nje ya nchi we zoba
 
Back
Top Bottom