Dodoma: Tundu Lissu afuata gari lake lililoshambuliwa ofisini kwa RPC Muroto. Ashangaa hadi sasa hajahojiwa yeye na Dereva wake

Dodoma: Tundu Lissu afuata gari lake lililoshambuliwa ofisini kwa RPC Muroto. Ashangaa hadi sasa hajahojiwa yeye na Dereva wake

Kudadadeki! Huyu mwamba ni untouchable. Yaani mikwara yote ile ya polisi kutishia kumkamata soon atakaporejea sasa imegeuka barafu.

Anadiriki kutinga hadi kwenye 18 zao na wanaishia kujichekesha tu. Hivi kulikoni jamaa anaogopwa hivi?
 
Hahahah huyu mgonjwa amekuwa kitukp kweli sasa kajipeleka ana shangaa hawajamuhoji wakati hakuwepo na alisha sema kuwa wao ndio walimshambulia sasa sijui anataka wamuhoji nini wakati majibu anayo mkononi hahahaha mgonjwa bwana
SI MLIKUWA MNASEMA ARUDI AHOJIWE? NA MLISEMA AKIKANYAGA TU TANZANIA MNAMKAMATA, SASA KAJILETA MNAKUWA WAPOLE TENA!
 
Kudadadeki! Huyu mwamba ni untouchable. Yaani mikwara yote ile ya polisi kutishia kumkamata soon atakaporejea sasa imegeuka barafu.

Anadiriki kutinga hadi kwenye 18 zao na wanaishia kujichekesha tu. Hivi kulikoni jamaa anaogopwa hivi?
HATA MIMI NASHANGAA. HIVI IGP BADO NI SIRRO YULE ALIYESEMA LISSU AKIKANYAGA TU ARDHI YA TANZANIA ANAMKAMATA
 
Ati anashangaaa!!!.. kibaraka akumbuke ana kesi.. huyu ni hatari sana.. hata mwili wake.. hakukumbuka ya gari.. hadi kamaliza kukamilisha ubaraka wake aliotumwa na mabeberu.. hafai kuwa kiongozi wa nchi hii hata kwa sekunde moja.. tukisema ilikuwa mipango yao wenyewe.. bado munapiga kelele. Ati nini!!!😅😅😅😅😅

Magufuli 2020 💯
Shombo tupu mpaka kwenye tenenge yako....endelea kugeuzwa geuzwa mwili na akili kama gogo
 
Hahahah huyu mgonjwa amekuwa kitukp kweli sasa kajipeleka ana shangaa hawajamuhoji wakati hakuwepo na alisha sema kuwa wao ndio walimshambulia sasa sijui anataka wamuhoji nini wakati majibu anayo mkononi hahahaha mgonjwa bwana
Ruttashobolwa =Rutashobokerwa! Hopeless.
 
Wasiojulikana mpaka wajulikane.
Tayari wanajulikana vizuri na mkuu wa shambulio Daud Bashite hana raha anashinda makanisani mchana na usiku anakesha kwa waganga wa kienyeji kwa mujibu wa Le mutuz
 
Hahahahah [emoji1787][emoji1787][emoji1787] nimecheka kweli

Huwa wanamsimanga akiwa mbali

Ila akiwa karibu wote wanakuwa washikaji
Hawana uhakika October 28 itakuaje maana huenda Lisu akawa mkazi wa Chamwino na mtukufu kurejea chato.
 
Uzuri selikali yangu na ccm sijaona mtu akimshobokea huyo jamaa yenu anaehangaika kama kuku anataka kutaga.
.
Watu wamemuacha ajihangaishe weee, hasira zikiisha atatulia ale ugali vizuri.
Hahitaji kushobokewa tokea lini atake wewe na wasiojulikana mmshobokee? nyinyi ni maadui lazima aendee kupiga kelele mpaka muache ushetani wenu wote
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

Mgombea Urais wa JMT kwa tiketi ya CHADEMA, Mh. Tundu Lissu, leo ametembelea Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuchukua gari lake ambalo limehifadhiwa na Jeshi la Polisi Mkoa huo jaribio la mauaji dhidi ya Mh. Lissu la tarehe 7 September 2017.

Mh. Lissu aliambatana na mgombea mwenza wake Mh. Salum Mwalimu na alipokelewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP Giles Muroto.

Katika mazungumzo yake na SACP Muroto, Mh. Lissu alisema kwamba ameamua kuja yeye mwenyewe baada ya utaratibu wa kulipata hilo kwa njia zingine kushindikana.

Kwa upande wake, SACP Muroto alimweleza Mh. Lissu kwamba Jeshi la Polisi mkoani hapo linahitaji muda zaidi ili kujiandaa kulikabidhi gari hilo kwake.

Aidha, SACP Muroto alimweleza Mh Lissu kwamba Jeshi la Polisi linamhitaji atoe maelezo kwa Jeshi la Polisi kuhusu kushambuliwa kwake September 2017.

Mh. Lissu alijibu kwamba yeye yuko tayari kutoa maelezo polisi kwa tarehe na muda utakaokuwa muafaka kwa pande zote mbili.

Mh. Lissu alisisitiza mshangao wake kwamba hadi sasa, takriban miaka mitatu tangu kushambuliwa kwake, Jeshi la Polisi halijafanya uchunguzi wowote, ikiwemo kumhoji yeye na dereva wake Adam Bakari Mohamed, licha ya kuahidi kwamba lingefanya tangu Mh. Lissu akiwa hospitalini nchini Kenya.

Imetolewa leo Alhamis, Agosti 27, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Analazimisha ahojiwe sasa ili atuhumu kwamba polisi wametumwa na Magufuli kumharibia ratiba zake za kampeni.

Trust me. This guy is an insane.
 
Bora Lissu ameenda polisi, hapo karudisha mpira kwa polisi na atatoa maelezo kwa muda sahihi kwake, polisi wasiendelee kusema Lissu anawakwepa kutoa maelezo, na baada ya hayo maelezo ya Lissu polisi itabidi waueleze umma wa watanzania uchunguzi wa shambulio dhidi ya Lissu umefikia wapi.

Kwa hili, Muroto hakuwa na jibu. Hakujipanga na kuuliza mamlaka ya juu. Amejiumauma tu. HONGERA SANA Mhe LISSU. Unajua cha kufanya, lini, na kwa hoja ipi. Ni wewe 2020. Kwa hili pia umeliacha uchi Jeshi la Polisi.
 
Analazimisha ahojiwe sasa ili atuhumu kwamba polisi wametumwa na Magufuli kumharibia ratiba zake za kampeni.

Trust me. This guy is an insane.
Angekufa mngetaifisha Gari lake? acha visingizio vya kishamba toka kolomije
 
Ni kweli wapo wafia chama au pro jamaa yangu. Lakini unaposoma comments zao, unavunjika moyo.

Ninachokiona kwa team hiyo , ni kuwa hawakuamini kama jamaa angelirudi na kuendelea na maisha kama kawaida . Na pia hawaamini ktk mawazo mbadala au tofauti na mapenzi yao.
CCM hawataki ushindani wa wazi ndiyo maana walipenyeza figisu figisu kila kona kuwahujumu chadema, wanajinadi kununua Ndege kujenga SGR na miradi mingi lakini hawajiamini na bado wapo busy kuwahujumu chadema.
 
Back
Top Bottom