Tarehe kama hii miaka 3 iliyopita,Tundu Antipas Lissu,wakati huo akiwa mnadhimu wa kambi ya upinzani na mbunge wa Singida Mashariki alipigwa risasi kwenye makazi yake Dodoma.Baada ya kupigwa risasi habari zilisambaa kwa haraka nchi nzima.
Suala la kwanza lilioafikiwa na Bunge kwa maana ya ofisi ya Spika na CHADEMA ilikuwa ni kumleta Tundu Lissu Dsm-Muhimbili,ndege iliyokodiwa ilikuwa ni ya kampuni ya Safari Air Link kwa kutumia bima ya kibunge ya NHIF ambayo ni MEDEVAC,ilikuwa ni Caravan usajili wa 5H-EWA,mali ya Peter Fox(mmiliki wa kampuni ya Safari Air Link).
Bahati mbaya au nzuri,CHADEMA wakapata habari za usalama mdogo wa Lissu kuja kutibiwa Muhimbili,sababu waliokosa kumuuwa kwa risasi,walikusudia njia nyingine,ikatokea mabadiliko ya kwenda Nairobi,na ile ndege ikawa na rubani mmoja na haiwezi kwenda Nairobi usiku ikiwa na rubani mmoja ambaye hakuwa na masaa ya kuruka usiku.
TCAA walikuwa tayari kutoa kibali cha ndege kuruka usiku hata kama ina injini moja kwa sharti la kuwa na marubani wawili,Ukawa ni mtihani mwingine wa kuanza kutafuta ndege nyingine usiku uleule.
Ndege nyingine ya Safari Air Link aina ya Citation(Jet Engines) siku hiyo ilikuwa imeenda Pemba ya Mozambique kama si Zambia,Fox mmiliki wake akawa hana option,sbb pia hiyo ndege isingeweza kubeba abiria wengi ambao CHADEMA walikusudia wasafiri na Lissu.
Ndege kubwa ya kuwatosha mgojwa,daktari pamoja na wasindikizaji akiwemo mkewe, ikawa ni hiyo Citation ya Flight Link,yenye usajili wa 5H-ETG.Ambayo ilipaswa kutoka Dsm kuja Dodoma usiku uleule,ili inyanyuke kwenda Nairobi.
Jambo hili likawezekana,lakini ilipaswa pesa iwe juu ya meza kwa mlipo ya dola,Dodoma hakukuwa na Mbunge wala waziri mwenye dhamana ya dola,Mbunge Turky wa Jimbo la Mpendae akachukua dhamana hiyo ya mali kauli,sababu mmiliki wa kampuni ya Flight-Link(Mhindi) wana ushirika naye kibiashara.Ndege ilinyanyuka Dsm-Dodoma na baadae Nairobi
Siri ya safari ile wakiwa angani,naamini ipo siku Mbowe na Msigwa wataiandikia kitabu(A Day to Remember in a Dark Political Journey),Ilikuwa ni safari ngumu iliyojaa machozi na uchungu mkubwa,walisafiri kwa shida sana,kitanda kilikuwa kinacheza na pia dripu ilibidi Dokta asafiri akiwa ameishika mkononi kaining'iniza juu sababu "height" ya ndege ilikuwa fupi,ilikuwa ni safari ya mateso na experience mbaya sana kwa kina Msigwa na Mbowe pamoja na mke wa Lissu.Mungu aliyemponya Danieli katikati ya Simba wenye njaa,alitenda miujiza.
Huku nyuma waziri wa Afya,akiwa mbele ya waandishi wa habari aliitangazia dunia kuwa serikali ipo tayari kumtibu Lissu popote pale duniani,ikiwa tu familia itapendekeza wapi wanataka ndugu yao akatibiwe,Bunge la Ndugai likatoa taarifa ya kumuhudumia Lissu kama sehemu yake ya "statutory benefits" inavyotaka.
Siku zikaenda,Ummy akajikausha,Ndugai akaikana kauli yake kwa matendo.Akagoma kulipa fedha za matibabu,akamtaja Lissu kama mtoro huku akisema hajui alipo.Mwisho alimfukuza bungeni na kumvua ubunge wake.
Haya yote hayakuondoa uhai wa Lissu,sio risasi 16 mwilini,sio kunyimwa matibabu wala kufukuzwa ubunge wake.Vikwazo vyote alipita salama na sasa ni sehemu ya mgombe wa Urais Tanzania,akiwa amehuisha siasa za Tanzania zilizolala kwa miaka mitano.
Amerudi akiwa imara zaidi kuliko mwanzo,jasiri ya tulivyokuwa tukidhani.Mapungufu yake ya kimaumbile kwa maana ya mguu mmoja kuwa mfupi na mkono mmoja kutokunyooka vizuri,hayajaondoa umachachari wa Lissu katika kazi aipendayo,kazi ya siasa na harakati za kukimbizana na watawala.Huu ndio "wito" wa Lissu toka akiwa Iliboru Sekondari mpaka Galanos na chuo Kikuu.
Lissu anaipenda siasa,Lissu anapenda kuwatesa wanasiasa wenzake kwa hoja,anaweza akawa anaona hatashinda kwa mfumo wa siasa za Tanzania,lakini furaha yake ni kuona anazunguka nchi nzima,akiwaamsha wananchi na kuwakosoa watawala,ukosoaji wake unawaamsha watawala,wanatekeleza ahadi na kukumbuka kugawa rasilimali kwa namna inayowanufaisha watu wote katika Taifa,watu wengine hupenda kufanya yale waliyozaliwa kuyafanya,hawazuiliki kwa mtutu wa bunduki wala kwa wosia wa viongozi wa dini.
Lissu aliyeondoka katika machela,kwenye pumzi yenye msaada wa mitungi ya gesi.Lissu aliyekoma kusikia na kuhisi kwa muda wa week mbili na baadae kuwa ICU kwa miezi kadhaa,ndio huyu sasa amefanya siasa za Tanzania katika uchaguzi wa 2020 kuwa hai na za ushindani ambao haukutarajiwa.Miaka mitatu iliyopita,katika tarehe ya leo,tuliamini Lissu atakuwa kamaliza safari yake hapa duniani...
Mara moja Dalali Lama aliwahi kusema,
"Death is a part of all our lives. Whether we like it or not, it is bound to happen. Instead of avoiding thinking about it, it is better to understand its meaning. We all have the same body, the same human flesh, and therefore we will all die. There is a big difference, of course, between natural death and accidental death, but basically death will come sooner or later. If from the beginning your attitude is 'Yes, death is part of our lives,' then it may be easier to face"