DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Tarehe kama hii miaka 3 iliyopita,Tundu Antipas Lissu,wakati huo akiwa mnadhimu wa kambi ya upinzani na mbunge wa Singida Mashariki alipigwa risasi kwenye makazi yake Dodoma.Baada ya kupigwa risasi habari zilisambaa kwa haraka nchi nzima.

Suala la kwanza lilioafikiwa na Bunge kwa maana ya ofisi ya Spika na CHADEMA ilikuwa ni kumleta Tundu Lissu Dsm-Muhimbili,ndege iliyokodiwa ilikuwa ni ya kampuni ya Safari Air Link kwa kutumia bima ya kibunge ya NHIF ambayo ni MEDEVAC,ilikuwa ni Caravan usajili wa 5H-EWA,mali ya Peter Fox(mmiliki wa kampuni ya Safari Air Link).

Bahati mbaya au nzuri,CHADEMA wakapata habari za usalama mdogo wa Lissu kuja kutibiwa Muhimbili,sababu waliokosa kumuuwa kwa risasi,walikusudia njia nyingine,ikatokea mabadiliko ya kwenda Nairobi,na ile ndege ikawa na rubani mmoja na haiwezi kwenda Nairobi usiku ikiwa na rubani mmoja ambaye hakuwa na masaa ya kuruka usiku.

TCAA walikuwa tayari kutoa kibali cha ndege kuruka usiku hata kama ina injini moja kwa sharti la kuwa na marubani wawili,Ukawa ni mtihani mwingine wa kuanza kutafuta ndege nyingine usiku uleule.

Ndege nyingine ya Safari Air Link aina ya Citation(Jet Engines) siku hiyo ilikuwa imeenda Pemba ya Mozambique kama si Zambia,Fox mmiliki wake akawa hana option,sbb pia hiyo ndege isingeweza kubeba abiria wengi ambao CHADEMA walikusudia wasafiri na Lissu.

Ndege kubwa ya kuwatosha mgojwa,daktari pamoja na wasindikizaji akiwemo mkewe, ikawa ni hiyo Citation ya Flight Link,yenye usajili wa 5H-ETG.Ambayo ilipaswa kutoka Dsm kuja Dodoma usiku uleule,ili inyanyuke kwenda Nairobi.

Jambo hili likawezekana,lakini ilipaswa pesa iwe juu ya meza kwa mlipo ya dola,Dodoma hakukuwa na Mbunge wala waziri mwenye dhamana ya dola,Mbunge Turky wa Jimbo la Mpendae akachukua dhamana hiyo ya mali kauli,sababu mmiliki wa kampuni ya Flight-Link(Mhindi) wana ushirika naye kibiashara.Ndege ilinyanyuka Dsm-Dodoma na baadae Nairobi

Siri ya safari ile wakiwa angani,naamini ipo siku Mbowe na Msigwa wataiandikia kitabu(A Day to Remember in a Dark Political Journey),Ilikuwa ni safari ngumu iliyojaa machozi na uchungu mkubwa,walisafiri kwa shida sana,kitanda kilikuwa kinacheza na pia dripu ilibidi Dokta asafiri akiwa ameishika mkononi kaining'iniza juu sababu "height" ya ndege ilikuwa fupi,ilikuwa ni safari ya mateso na experience mbaya sana kwa kina Msigwa na Mbowe pamoja na mke wa Lissu.Mungu aliyemponya Danieli katikati ya Simba wenye njaa,alitenda miujiza.

Huku nyuma waziri wa Afya,akiwa mbele ya waandishi wa habari aliitangazia dunia kuwa serikali ipo tayari kumtibu Lissu popote pale duniani,ikiwa tu familia itapendekeza wapi wanataka ndugu yao akatibiwe,Bunge la Ndugai likatoa taarifa ya kumuhudumia Lissu kama sehemu yake ya "statutory benefits" inavyotaka.

Siku zikaenda,Ummy akajikausha,Ndugai akaikana kauli yake kwa matendo.Akagoma kulipa fedha za matibabu,akamtaja Lissu kama mtoro huku akisema hajui alipo.Mwisho alimfukuza bungeni na kumvua ubunge wake.

Haya yote hayakuondoa uhai wa Lissu,sio risasi 16 mwilini,sio kunyimwa matibabu wala kufukuzwa ubunge wake.Vikwazo vyote alipita salama na sasa ni sehemu ya mgombe wa Urais Tanzania,akiwa amehuisha siasa za Tanzania zilizolala kwa miaka mitano.

Amerudi akiwa imara zaidi kuliko mwanzo,jasiri ya tulivyokuwa tukidhani.Mapungufu yake ya kimaumbile kwa maana ya mguu mmoja kuwa mfupi na mkono mmoja kutokunyooka vizuri,hayajaondoa umachachari wa Lissu katika kazi aipendayo,kazi ya siasa na harakati za kukimbizana na watawala.Huu ndio "wito" wa Lissu toka akiwa Iliboru Sekondari mpaka Galanos na chuo Kikuu.

Lissu anaipenda siasa,Lissu anapenda kuwatesa wanasiasa wenzake kwa hoja,anaweza akawa anaona hatashinda kwa mfumo wa siasa za Tanzania,lakini furaha yake ni kuona anazunguka nchi nzima,akiwaamsha wananchi na kuwakosoa watawala,ukosoaji wake unawaamsha watawala,wanatekeleza ahadi na kukumbuka kugawa rasilimali kwa namna inayowanufaisha watu wote katika Taifa,watu wengine hupenda kufanya yale waliyozaliwa kuyafanya,hawazuiliki kwa mtutu wa bunduki wala kwa wosia wa viongozi wa dini.

Lissu aliyeondoka katika machela,kwenye pumzi yenye msaada wa mitungi ya gesi.Lissu aliyekoma kusikia na kuhisi kwa muda wa week mbili na baadae kuwa ICU kwa miezi kadhaa,ndio huyu sasa amefanya siasa za Tanzania katika uchaguzi wa 2020 kuwa hai na za ushindani ambao haukutarajiwa.Miaka mitatu iliyopita,katika tarehe ya leo,tuliamini Lissu atakuwa kamaliza safari yake hapa duniani...

Mara moja Dalali Lama aliwahi kusema,
"Death is a part of all our lives. Whether we like it or not, it is bound to happen. Instead of avoiding thinking about it, it is better to understand its meaning. We all have the same body, the same human flesh, and therefore we will all die. There is a big difference, of course, between natural death and accidental death, but basically death will come sooner or later. If from the beginning your attitude is 'Yes, death is part of our lives,' then it may be easier to face"
Dah!.. Mungu ni mwema wakati wote, hii nchi imepitia mazingira magumu sana ya kisiasa awamu hii.
 
Wakuu,

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ajeruhiwa kwa risasi.

Kwa sasa wapo hospitali ya Mkoa, mjini Dodoma.

Ameshambuliwa kwa risasi wakati akishuka nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma, alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.

Lissu amepigwa risasi 5, miguuni na tumboni.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hali ya Mbunge huyo aliye hospitalini sasa ni mbaya!




56d494001b8e52eca1b71490ff9635e4.jpg


9f94cea0e0708e5fafb57915caf1dd27.jpg

abc21fedd617180297c6247f403b7362.jpg


=======

UPDATES:

=======

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.

Selasini amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na gari tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia. Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari.

"Hao watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia walivyoona kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na kuanza kurusha risasi upande wa Lissu." amesema.

Selasini amesema, “Risasi zilimpata mguuni, mkononi na tumboni lakini daktari anasema anaendelea vizuri."

Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.

Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari huku wengine wakilia.

UPDATE: Ndege imeshawasili Dodoma ili kumchukua Tundu Lissu kumpeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi

Katibu wa Bunge amethibitisha kufika kwa ndege Dodoma kumchukua Tundu Lissu kumpeleka hospitali ya Muhimbili ili kuokoa maisha yake

DODOMA: RPC amesema watu waliomshambulia Tundu Lissu walikuwa wakitumia gari aina ya Nissan la rangi nyeupe

Freeman Mbowe: Ndugu Lissu kwa sasa yuko katika chumba cha upasuaji anajaribu kuokoa maisha yake, nitazungumza baadaye.

View attachment 583459
UPDATES: Miongoni mwa waliofika hospitali kumuona Lissu ni Spika Job Ndugai, Waziri Ummy Mwalimu na katibu mkuu wa bunge, Dkt. Thomas Kashilila

Rais Magufuli ametoa pole na kutaka Vyombo vya Dola kuchukua hatua:

CCM imetoa pole

Waziri wa zamani, Mark Mwandosya naye ametoa pole
View attachment 583477

UPDATES: 2235HRS
Ndege iliyokuja kumchukua Tundu Lissu ndo inatua Uwanja wa Dodoma. Ni ndege binafsi, imetoka Dar Es Salaam na itampeleka Mh. Lissu Nairobi Kenya kwa matibabu zaidi.
6a0df0d4014896f500bc344cb3ddcb26.jpg

TunduLissu akipakiwa kwenye ndege usiku huu tayari kwa safari ya Nairobi kwa matibabu zaidi
3c38765220348b8a8712fc343f512797.jpg


*Rais wa Chama cha Mawakili Kenya(LSK), Isaac Okero amesema Lissu amelazwa Hospitali ya Aga Khan, Nairobi.

Lissu awasili Nairobi salama lakini Ubalozi wa Tanzania haujatoa ushirikiano

Mbowe: Hali ya Lissu ni mbaya na yupo kwenye chumba cha upasuaji

TAARIFA YA AWALI KUHUSU SHAMBULIO LA KUPIGWA RISASI MHE. TUNDU LISSU

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kupigwa risasi Mwanasheria Mkuu wa Chama ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Antipus Lissu baada ya kikao cha Bunge mchana wa leo.

Shambulio hilo limetokea majira ya mchana nyumbani kwake Area D Dodoma na kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hosiptali ya Mkoa wa Dodoma.

CHADEMA tunalaani vikali kitendo hicho, na tunafuatilia kwa karibu hali yake.

Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Imetolewa na Kurugenzi ya Uenezi, Mawasiliano na Mahusiano ya Nje.

CHADEMA MAKAO MAKUU

DAR ES SALAAM.

=====

Preliminary Press Statement on the incidence of Hon. Tundu Lissu being shot

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) has received with great shock the report on the shooting of the Attorney General of the Party who is also the Chief Whip of the Official Opposition in Parliament and MP of Singida East, Hon. Tundu Antipus Lissu just after a Parliamentary session today.

The attack took place at his Dodoma residence at midday and was seriously wounded and had been rushed to the Dodoma Regional Hospital.

CHADEMA strongly condemns this act, and we are following up closely on his condition.

We will continue to update as we get more information.

Issued by the Directorate of Ideology, Publicity, Communications and Foreign Relations.

=====

Dar es Salaam. Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi kati ya 28 hadi 32, huku tano zikimpata mwilini.

Lissu alishambuliwa jana Alhamisi kabla hajashuka kwenye gari baada ya kumaliza kikao cha Bunge na alipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kabla ya kusafirishwa saa sita usiku, kuelekea Hospitali ya Aga Khan ya Nairobi, Kenya.

Akitoa taarifa ya tukio hilo kwenye kikao cha Bunge leo Ijumaa, Ndugai amesema risasi mbili zilimpata Lissu kwenye miguu, mbili tumboni na moja kwenye mkono.

Amesema watu wasiofahamika wakiwa kwenye gari aina ya Nissan ambalo halijajulikana walimpiga risasi kisha kutoweka.

“Baada ya tukio hilo watu hao walikimbia,” amesema Ndugai. Alisema Lissu alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa kutumia gari la familia ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kwa kuwa wanaishi jirani.

“Alipofika hospitali aliingizwa kwenye chumba cha upasuaji na kufanyiwa upasuaji ili kuzuia damu kuendelea kutoka katika majeraha aliyokuwa ameyapata,” amesema Ndugai.

Amesema upasuaji huo uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya akishirikiana na madaktari wengine.

“Baada ya upasuaji tulielezwa kuwa hali yake iliendelea kutengemaa na anaweza kusafirishwa kwa matibabu zaidi,” amesema.

Ndugai amesema ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ilishaandaa ndege saa 10:30 jioni kwa ajili ya kumchukua mgonjwa na kumpeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

Hata hivyo, amesema baada ya kushauriana na familia na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe waliona ni vyema mgonjwa huo apelekwe katika Hospitali ya Aga Khan, Nairobi.

“Hivyo kwa kushirikiana na ofisi ya Bunge ilipatikana ndege nyingine ya Flying Doctors na kuondoka na mgonjwa saa sita usiku, kuelekea Nairobi,” amesema.

Amesema tukio hilo liliripotiwa polisi ambako waliahidi kufanya msako kuwatafuta wahalifu hao na Serikali itatoa taarifa kamili kwa kuzingatia utaratibu wa kibunge.

Spika Ndugai amesema tukio hilo ni la kwanza la aina yake tangu Bunge lilipohamia Dodoma na kwamba, haijawahi kutokea mbunge akashambuliwa kwa risasi.

Amesema pia haijawahi kutokea tukio la aina hiyo wakati Bunge likiendelea na vikao, hivyo amewaomba Watanzania kuwa na subira wakati vyombo vya dola vikiendelea na kazi.

“Utaratibu wetu wa kibunge wa matibabu ambao ndiyo utaratibu wa Watanzania wote, baada ya mwenzetu kupata tatizo hili tulikuwa tumeshaagiza ndege kumpeleka Muhimbili,” amesema.

Amesema ingekuwa anatakiwa kusafirishwa nje, Serikali ina mkataba na Hospitali ya Apollo ya India na kwamba, Lissu amepelekwa Nairobi kwa sababu familia imeomba.

“Lakini kwa nini mwenzetu alipelekwa Nairobi, ni kwa sababu familia iliomba. Nimnukuu Mheshimiwa Mbowe kwa niaba yake si kwamba wana shaka na umahiri na uwezo wa madaktari wetu,” amesema.

Amewataka Watanzania kuendelea kumuombea kiongozi huyo katika kipindi hiki kigumu.

Amewashauri wabunge walioanza kutuma ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kutumia maneno ya hekima badala ya kuendelea kuchonganisha pande mbili.

Habari zaidi, soma=>Ubelgiji: Tundu Lissu aruhusiwa kutoka Hospitalini

Ilikua siku ngumu hii,Ashukuriwe Mungu mkuu alietengua mipango ya waovu, spirituality
 
Mkuu asante,
Baada ya kusoma hiki ulichoandika hapa,nimeona jinsi taabu na mateso aliyopitia Lissu tangu yupo safarini kwenda kwenye matibabu Nairobi

Pili nimeona Ukuu wa Mungu alivyoweza kuushikilia uhai wa Lissu akiwa katika mapambano ya Uhai wake

Mwisho nimepata tumaini kwakua amerudi akiwa na Afya ya mwili na akili na yupo tayari kuendelea kuwatetea watanzania,

Hakika Mungu ni Mwema,Watesi wake wameshindwa na sasa Mungu atawataabisha,na kuwafedhehesha

Amen

..nilisikiliza interview ya mke wa TL ilinisikitisha sana.

..mama yule alielezea safari yake ya kutoka Dsm kumfuata mume wake aliyekuwa ameshambuliwa Dodoma.

..pia Mh.Mbowe aliwahi kufika Singida na kuelezea jinsi walivyomtoa TL Dodoma mpaka kutua Nairobi na kumfikisha mgonjwa hospitali.

..lakini wako mashujaa watatu wa tukio hili. Na ni wasaidizi wa TL ambao walimchukua toka area D na kumkimbiza Dodoma Hospital.

..Nawazungumzia Khadija Akukweti aliyetoa msaada wa gari; Amina Abrahman Kanyama aliyetafuta msaada kwa Khadija; na Adam Mohamed Bakari dereva wa TL.

Mh.Mbowe:

 
Leo hii ikiwa ni tarehere 07/09/2020,ni miaka mitatu kamili tangu Tundu Lissu ashambuliwe mkoani Dodoma huku waliohusika na unyama huu wakiendelea kuitwa wasiojulikana.

Kibaya zaidi, watu fulani, hasa wa upande fulani, wanaonekana kuendelea kutoa kauli za kejeli juu ya tukio hili lengo likionekana kuwa ni kumfurahisha Bwana Yule anaedhaniwa kuwa yuko nyuma ya tukio hili.

Binafsi nasema,kwakuwa wameshindwa kuwa waungwana walau hata kwa kuacha kujeli,basi mwenyezi Mungu awashushie pigo takatifu wao na huyo wanamnyenyekea ambae dalli zinaonyesha alitoa baraka zake katika kutekeleza huu unyama.

Tuitumie siku ya leo kuwalaani hawa watu hasa wale wanaojitoa akili kisa kumfurahisha boss wao.

1599509389270.png
 
Back
Top Bottom