Kwa habari ambayo siyo nzuri maskioni kwa mtanzania ni MH. TUNDU LISSU, Mbunge wa Singida mashariki na rais wa chama cha wanasheria nchini TLS, amepigwa risasi na watu wasio julikana.
Sina maneno menhi ila tunapaswa kujua kws trend ya matukio ya Tundu Lissu na kuikosoa serikali hili ni tukio ambalo linaweza kutuacha na maswali mengi ambayo kwa kila atakaye yatafakari anaweza kuamua au kupata majibu ya chuki za kusiasa.
Serikali inayodhamana ya kutoa ulinzi kwa kila raia wa nchi hii na zaidi kutoa ulinzi kwa viongozi wa nchi wakiwemo wabunge wa bunge la jamhuri ya Muungano.
Kushambuliwa kwa Tindu Lissu kunaweza ibua chuki za kisiasa kali miongoni mwa raia na viongozi kwa ujumla, siwezi kusema serikali inahusika moja kwa moja maana nitaombwa kuthibitisha ila narudia kusema serikali km chombo chenye dhamana ya kilinda haki, usalama wa raia wake na mali zao, ilikuwa dhahiri watoe ulinzi kwa mh. Tundu Lissu sababu kuu ni mbili moja kwa watu wa kariba ya Lissu watu wasio tutakia mema ni rahisi kuwatumia kwa namna yeyote kuwachonganisha wananchi na serikali, kwa taaluma ndogo ya kijitafutia kuhusu mambo ya usalama ni rahisi adui kujipenyeza na kuandaa uharifu wa namna hii ambao unaweza kuwaacha midomo wazi wananchi na serikali.
Kwa dhamana aliyonayo serikali kwa kila raia tukisema serikali inahusika wenda wakashindwa kujibu kwanza mh.,Lissu amekuwa mkosoaji mkuu wa serikali ya mh. Rais JPM kesi lundo zinamkabili Mh. Lissu ni ushahidi tosha kuwa serikali ilitakiwa kumpa ulinzi kuzuia hisia hasi juu ya tukio km hili kusema kweli.
Binafsi nichukue nafsi hii kulaani na kuhisihi serikali iwe imehusika au hauijahusika watambue AMANI ya nchi hii iko mikononi mwa raia(watanzania) wenyewe wala siyo vifaru, majeshi, polisi , au matumizi ya sheria kali na kandamizi ambazo mara nyingi huwa zinaleta utengano badala ya utangamano.
Mwisho mh. Rais kwa mamlaka uliyonayo please nikuombe yatumie kuagiza vyombo vya dola kusaka hawa waarifu wa tukio hili, km kweli serikali hausiki maana hili tukio baya kabisa katika historia ya nchi yetu. Ukisikia RWANDA,KONGO, BURUNDI, SOUTH SUDANI, SOMALIA NA NCHI NYINGI ZA AFRICA chanzo ni utawala usiofuata demokrasia na ukandamizwaji wa uhuru wa maoni ya watu, hii hutoa mwanya kwa wazungu kujipenyeza na kupandikiza chuki za kijinga na badae kusuport vikundi vya waasi.
Chondechonde watanzania haya matukio ya kushambuliana viongozi wa kisiasa ni kati ya matukio maovu kabisa.