Kuna msemo unaosema ".....kuna mstari mwembaba sana (finest line) unaotenganisha kifo na uzima ...... kushindwa na kushinda....giza na mwanga...."
Nchi yetu kwa sasa iko katika kipindi kigumu na cha hatari sana. Kama tusipokuwa makini na wenye hekima basi punde giza na hatari vitatuvaa na tusijue tumefikwaje na hayo. Siasa ni sehemu ndogo ya maisha, kwa hiyo haipaswi kuwa kipimo cha kila kitu kinachofanyika katika jamii au nchi yetu. Siasa ni sehemu tu na sio kitu kizima cha kinachoitwa jamii au nchi. Siasa ni kitu kinachoweza kuleta mabaya au mema kwa jamii au nchi yoyote ile. Hivyo tusitazame na kupima mambo yote kwa mizani au miwani ya siasa.
Napenda kuweka kwenye kumbukumbu sawa; kwa viongozi wakuu wa nchi yetu, serikali, vyama na taasisi zote.
"Kwani atafaidiwa nini MTU akiupata Ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au MTU atatoa nini badala ya nafsi yake?"Mathayo 16:26
Kwamba, kwa Mwenyezi Mungu nafsi ya mwanadamu mmoja ina thamani kuliko ulimwengu wote.
Ulimwengu wote = madini yote ya thahabu, almasi, tanzanite, shaba, gesi, uranium, vito vyote vya thamani nk nk.
Ulimwengu wote = samaki wote wa aina zote, tembo wote, faru wote, simba wote, ndege wote, wanyama wote nk.
Ulimwengu wote = milima yote, mabonde yote, mito, maziwa, bahari, mashamba, misitu, mbuga, migodi nk nk nk
Ulimwengu wote = viwanda, mabenki, fedha zote, vyuo, majumba, reli, barabara, bandari, magari, meli, ndege nk nk
Ulimwengu wote = ni vitu vyote vilivyo juu ya uso wa nchi na chini ya uso wa nchi (mfano mafuta nk nk)
Sasa Watanzania kwa nini tunautukuza uovu? Kwa nini tunatukuza ujinga na upumbavu? Kwa nini tunatoa nafasi ya kupoteza amani yetu, utaifa wetu, umoja wetu, mustakabali wetu kwa vigezo tata na dhaifu viitwavyo "uzalendo" na kingine "rasilimali za nchi" na kingine "mamlaka" viwe sababu ya watu kuteswa na wengine kuuawa????? Kwa sehemu pamoja na madhaifu mengi ya Katiba yetu ya 1977, lakini uhai na haki za raia (wanadamu) zinaelezwa na kulindwa kwa nguvu humo. Ibara za
Damu ya mwanadamu yeyote ikimwagika (isivyo haki) huacha laana na madhara makubwa kwa wanaoishi juu ya uso wa nchi.
Nimalizie na historia ya mwanzo kabisa ya mwanadamu.
1) Mwanzo 4:
Wengi tunakubali kuwa Adam na Hawa (Adam and Eve) ndio binadamu wa mwanzo kuumbwa, na sisi ni watoto wao. Lakini watoto wao wa kwanza kabisa yaani ni Kaini na Habili (Cain and Abel), mmoja alimwua mwingine. Kaini alimwua Habili.
4:11 "Basi umelaaniwa wewe (Kaini) katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako (Habili) kwa mkono wako"
2) Mwanzo 9:5-6
"Hakika damu yenu (wanadamu) ya uhai wenu nitaitaka, na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka, na kwa mkono wa kila mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu"
"Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na wanadamu, maana kwa mfano wake MUNGU alimfanya mwanadamu"
Kwa hiyo ndugu zangu, nawasihi sana tusicheze na maisha na uhai wa wanadamu wenzetu kwa kigezo chochote kile. Ni mtego rahisi wa Adui tu. Tuukatae, tuupinge nasi tutaushinda uovu.
Huyu ndiye aliyeomba ruhusa kumuua Tundu Lissu