Dodoma: Ufunguzi wa Bunge la 12, Ndugai asema Bunge hilo halitakuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani

Dodoma: Ufunguzi wa Bunge la 12, Ndugai asema Bunge hilo halitakuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani

Huyu dada wa CHADEMA hajitambui kabisa. Anachotaka ni hela ambayo licha ya kuwa ataipata lakini atakuwa mtumwa mkubwa wa kifikra ndani ya bunge.. Kwa akili yake alifikiri atakuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni. Tormentation inaendelea....
Ndio maana waliamua kumleta kukaa nao kwenye bunge la POMBE. Nadhani angehamia kabisa hata kwenye chama cha POMBE, Ndugai atasimamia.
 
Bunge kipindi wakati wa Mwalimu Nyerere licha kwamba lilikuwa la chama kimoja lakini lilikuwa zuri kutokana na wabunge waliokuwemo na mijadala yake ilikuwa mikali.

Sasa wengi waliopo huko ni taka taka, wahuni na wasaka pesa ya kujikimu maisha yao! Wasomi uchwara na wagonga meza tu kichwani hakuna kitu! Hadhi ya Bunge imeteremka mpaka kiwango cha chini kabisa likiongozwa na huyo mgogo! Aibu sana
Tanzania yazidi kwenda kombo
1605005451660.png
 
Kwanini bunge lisivunjwe kuwe na kikao cha CCM tu Aida kiherehere anaalikwa basi
 
Mkutano wa kwanza wa Bunge la 12 umeanza rasmi leo Novemba 10, 2020, jijini Dodoma, ambapo moja ya shughuli zinazofanyika kwa sasa ni zoezi la kumchagua Spika wa Bunge.

Moja ya kazi za kwanza za vikao vya mwanzo vya mkutano huu itakuwa ni kumchagua Spika wa Bunge, Naibu wake pamoja na kuthibitisha jina la Waziri Mkuu litakalowasilishwa mbele yao na Rais Magufuli, kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoelekeza.

Pia baada ya kuchaguliwa Spika anatarajiwa kufanya kazi ya kuwaapisha wabunge, na inatarajiwa pia wiki hii Rais Magufuli atalizindua Bunge hili la 12, kabla halijaanza rasmi majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.

================

Wakati vikao vya Bunge la 12 la Tanzania vikianza leo jijini Dodoma, bunge hilo litakuwa na muundo tofauti kidogo na Bunge la 11, ambapo katika bunge la sasa hakutakuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani.

Hayo yamesema na mgombea wa nafasi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai wakati akinadi sera zake mbele ya wabunge na kuwaomba kumchagua ashike nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.

“… hatutakuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani kwa kuwa hawataweza kutimiza asilimia 12.5 ambayo ipo katika kanuni yetu,” amesema Ndugai.

Akijibu swali la Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Aida Khenani (CHADEMA), Ndugai amesema licha ya kambi hiyo kutokuwepo, wabunge wa CCM ambao wengi ni vijana kwa kushirikiana na ofisi ya spika, watawatendea haki wabunge wa upinzani.

Vyama vya upinzani vilipata jumla ya wabunge nane (CHADEMA 1, ACT Wazalendo 4 na CUF 3) katika uchaguzi mkuu uliofanyoka Oktoba 28 mwaka huu. Pia, kutokana na idadi kubwa ya kura za wabunge, CHADEMA imepata nafasi ya kuteua wabunge 19 wa viti maalum, hata hivyo chama hicho hakijafanya uteuzi huo.

Endapo CHADEMA itateua wabunge hao, jumla ya wabunge wa upinzani bungeni watakuwa 27, lakini sisipowateua, wabunge wa upinzani watakuwa nane, idadi ambayo ni ndogo sana ikilinganishwa na bunge lililopita.

Katika mkutano wa kwanza wa bunge uliaoanza leo mambo kadhaa yanatarajiwa kufanyika ikiwa ni pamoja na kuthibitisha uteuzi wa waziri mkuu, kuchagua spika na naibu spika, kiapo cha uaminifu kwa wabunge na kusomwa kwa tangazo la Rais la kufungua bunge.


Sawa tumepokea tahalifa, Mambo mengi mda mchache
 
Back
Top Bottom