Dodoma: Ufunguzi wa Bunge la 12, Ndugai asema Bunge hilo halitakuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani

Dodoma: Ufunguzi wa Bunge la 12, Ndugai asema Bunge hilo halitakuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani

Mkutano wa kwanza wa Bunge la 12 umeanza rasmi leo Novemba 10, 2020, jijini Dodoma, ambapo moja ya shughuli zinazofanyika kwa sasa ni zoezi la kumchagua Spika wa Bunge.

Moja ya kazi za kwanza za vikao vya mwanzo vya mkutano huu itakuwa ni kumchagua Spika wa Bunge, Naibu wake pamoja na kuthibitisha jina la Waziri Mkuu litakalowasilishwa mbele yao na Rais Magufuli, kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoelekeza.

Pia baada ya kuchaguliwa Spika anatarajiwa kufanya kazi ya kuwaapisha wabunge, na inatarajiwa pia wiki hii Rais Magufuli atalizindua Bunge hili la 12, kabla halijaanza rasmi majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.

================

Wakati vikao vya Bunge la 12 la Tanzania vikianza leo jijini Dodoma, bunge hilo litakuwa na muundo tofauti kidogo na Bunge la 11, ambapo katika bunge la sasa hakutakuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani.

Hayo yamesema na mgombea wa nafasi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai wakati akinadi sera zake mbele ya wabunge na kuwaomba kumchagua ashike nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.

“… hatutakuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani kwa kuwa hawataweza kutimiza asilimia 12.5 ambayo ipo katika kanuni yetu,” amesema Ndugai.

Akijibu swali la Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Aida Khenani (CHADEMA), Ndugai amesema licha ya kambi hiyo kutokuwepo, wabunge wa CCM ambao wengi ni vijana kwa kushirikiana na ofisi ya spika, watawatendea haki wabunge wa upinzani.

Vyama vya upinzani vilipata jumla ya wabunge nane (CHADEMA 1, ACT Wazalendo 4 na CUF 3) katika uchaguzi mkuu uliofanyoka Oktoba 28 mwaka huu. Pia, kutokana na idadi kubwa ya kura za wabunge, CHADEMA imepata nafasi ya kuteua wabunge 19 wa viti maalum, hata hivyo chama hicho hakijafanya uteuzi huo.

Endapo CHADEMA itateua wabunge hao, jumla ya wabunge wa upinzani bungeni watakuwa 27, lakini sisipowateua, wabunge wa upinzani watakuwa nane, idadi ambayo ni ndogo sana ikilinganishwa na bunge lililopita.

Katika mkutano wa kwanza wa bunge uliaoanza leo mambo kadhaa yanatarajiwa kufanyika ikiwa ni pamoja na kuthibitisha uteuzi wa waziri mkuu, kuchagua spika na naibu spika, kiapo cha uaminifu kwa wabunge na kusomwa kwa tangazo la Rais la kufungua bunge.



Bunge la Wabunge wenye connection. Sasa tukae mkao wa kuletewa maendeleo.
 
Kinachosikitisha ni watanzania kufanywa wajinga na wao kukubali mara zote!Kweli nchi hii zinaongozwa maiti!

Wakiweka bunge live inapaswa wananchi waihoji serikali,sababu zilizotolewa bunge kuzimwa zilikuwa halali au ulaghai?

Tuliambiwa mambo mawili:
1.Gharama
2.Muda wa kazi na watu wanapaswa kufanya kazi badala ya kuangalia bunge!
Hiyo sababu ya pili waliyoitoa kipindi kile ilikuwa ya kipumbavu sana.
 
Kinachosikitisha ni watanzania kufanywa wajinga na wao kukubali mara zote!Kweli nchi hii zinaongozwa maiti!

Wakiweka bunge live inapaswa wananchi waihoji serikali,sababu zilizotolewa bunge kuzimwa zilikuwa halali au ulaghai?

Tuliambiwa mambo mawili:
1.Gharama
2.Muda wa kazi na watu wanapaswa kufanya kazi badala ya kuangalia bunge!
Mm ndio siendag kupiga kura
 
Nyie mtakavyolifanya na fanyeni sisi hatuna munkari nalo..maana humo ndani kumejaa dhurma; Mauti, mateso!!
 
Bunge la enzi za Nyerere. Tuliokuwa hatupo duniani kipindi cha Nyerere ndo wakati wetu kujua bunge la fikra za mwenyekiti wa chama kudumu,likikuwaje.
 
Naam, kumekucha!

Spika kabla ya kuapisha wabunge awasisitiza kuwa wabunge wasiwe kimya waseme ili wasikike na vyombo vya habari waripoti na Bunge lionekane.

La kujiuliza, kwanini bunge lilopita walikataza na kuzuia lisiwe live?

Je, ile dhana ya kuwa kuonesha Bunge kutawafanya wananchi wasifanye kazi imeisha?
Hata siku wakifuta vyama vya mageuzi wataruhusu kukaa ndani ya mita 100 za vituo vya kupigia kura wataruhusu ndani ya kituo kuingia na camera na simu na matokeo yote kujumlishiwa vituoni
 
Ilikuwa vizuri kama vikao hivi vingekuwa vinafanyika ukumbi wa chama.

Jengo la Bunge litumike kama kumbi za kukodisha kwa wanaohitaji kama vile mikutano mikubwa na sherehe za arusi. Hiyo ingetupunguzia gharama, na kupatikana kipato cha kulipia utilities na watunzaji wa jengo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natamani watunge na sheria ya kumlazimisha kila mtu kutazama Bunge likiwa live. Asiyetazama achapwe viboko na faini juu,
Kwa nch a
Kama huendagi kupiga kura wewe ni dhaifu wa fikra na mawozo yako ni negative
Ni bora kuonekana dhaifu kuliko kuonekana hujielew unapiga kura mgombea anakwambia hata ukipiga kura huko mm ndio ntatengeneza serikal afu ukichek katiba mkurugenz NEC anamteua yy.

Eti mpaka apo hajaelewa nyiny ndio mnasababisha waafrika tutukanwe
 
Bunge lilikuwepo kuanzia miaka ya 2000 +,hadi 2020,hili la sasa sio bunge bali ni kikao cha Chama tawala .
 
Bunge kipindi wakati wa Mwalimu Nyerere licha kwamba lilikuwa la chama kimoja lakini lilikuwa zuri kutokana na wabunge waliokuwemo na mijadala yake ilikuwa mikali.

Sasa wengi waliopo huko ni taka taka, wahuni na wasaka pesa ya kujikimu maisha yao! Wasomi uchwara na wagonga meza tu kichwani hakuna kitu! Hadhi ya Bunge imeteremka mpaka kiwango cha chini kabisa likiongozwa na huyo mgogo! Aibu sana
Bunge la enzi za Nyerere. Tuliokuwa hatupo duniani kipindi cha Nyerere ndo wakati wetu kujua bunge la fikra za mwenyekiti wa chama kudumu,likikuwaje.
 
Back
Top Bottom