Dodoma: Wanaodaiwa kuwa wapenzi wakutwa wamefariki

Kimsingi....kama huduma za POLISI zingekuwa za faster mwenye nyumba....asingevunja mlango....kazi ingekuwa nyepesi.
 
Mmoja kati yao alifanya tukio maana mwenye nyumba anasema mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani
Wewe kama ni mpelelezi hufai. Mlango kufungwa kwa ndani ndiyo iwe lazima waliopo ndani ndiyo wamefanya? Kama kuna dirisha na muuaji alitumia dirisha kuingia na kutoka je? Kama muuaji alikuwa amejificha darini wakati mwenye nyumba anaingia je? Kama ni mwenye nyumba amewaua halafu akatunga uongo je?
 
Kwa haraka haraka,
kama kisu ni kimoja,
mwanaume kamchinja mwanamke nae kajipiga bisu la tumbo.. alivyoona israel mtoa roho huyu hapa ikabidi aombe msaada.

Kama visu viwili, ina maana wapenzi walishikiana visu.
Na ingekuwa mlango ulikutwa ukiwa wazi ama kufungwa kwa nje basi ningesema hili lilikuwa fumanizi. Ila kwa kuwa mlango ulifungwa kwa ndani basi mwanaume ndiye aliyefunga ili ampe mke kichapo.
 
Wewe kama ni mpelelezi hufai. Mlango kufungwa kwa ndani ndiyo iwe lazima waliopo ndani ndiyo wamefanya? Kama kuna dirisha na muuaji alitumia dirisha kuingia na kutoka je? Kama muuaji alikuwa amejificha darini wakati mwenye nyumba anaingia je? Kama ni mwenye nyumba amewaua halafu akatunga uongo je?
Duh kujua sana nako!
 
Kwanini mshukiwa wakwanza asiwe mwenye nyumba?
Huyu atakuwa saidia polisi. Siyo kila mshukiwa anakuwa mtuhumiwa bali wengine wanakuwa mashahidi na ama kuachiwa huru baada ya upelelezi.

Kuanzisha kesi ya jinai kunahitaji akili na maarifa. Mfano, Kuna baadhi ya watu wakiwa mashahidi wanafit zaidi kuliko kuwa watuhumiwa.

Na Kuna watuhumiwa wanafaa kuwa watuhumiwa wakuu na wengine wanafit kuwa watuhumiwa wasaidizi na wengine waathirika
 
Kama muuwaji karukia dirishani akatoroka nalo linawezekana pia
Nafikiri mpenzi wake ndio kawafumania akawauwa wote wawili na kutoroka

Hii inawezekana pia
Lakini kulingana na maelezo ya mwenye nyumba alipofika jamaa alikuwa anazungumza. Je, hakuweza kuelezea walau kwa kifupi kilichotokea?
 
Mama mzazi wa marehemu Esther, Rachel Izengo amesema jina la mtoto wake ni Esther Ramadhani Isugilo na siyo Samira Mathias ambalo lilizoeleka mtaani.

Esther amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatatu Septemba 18, 2023 kwa madai ya kuchinjwa na mpenzi wake aliyefahamika kwa jina moja la Amos.

Mapema leo asubuhi mmliki wa nyumba aliyokuwa amepanga Esther ambako kulifanyika mauaji hayo, Yohana Nhembelo alisema ndugu wameomba chumba kilichofanyika kisifanyiwe usafi hadi watakapofika na kukiangalia.

Amesema amepata taarifa ya kifo cha mtoto wake kupitia kwa majirani saa 10.00 usiku wa kuamkia leo akiwa mkoani Shinyanga ambako ndiko anakoishi.

Amesema alianza safari muda huo na kufika jijini Dodoma saa 8:00 leo ili kujua sababu ya kifo cha binti yake ambaye ni mtoto wa kwanza kati ya watoto watatu alionao.

“Nimesikitishwa sana na kifo cha mwanangu cha kuchinjwa kwa sababu ni kifungua mimba na sikutarajia kama atakufa kwa kifo kama hiki. Binti yangu alikuwa ni mtu wa watu,”amesema huku akiangua kilio baada ya kushuhudia chumba kichofanyika mauaji hayo.

Ndugu wa marehemu wamesema baada ya kuangalia hali ya mwili wa mtoto wao ndipo watafanya uamuzi wazike wapi.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Martin Otieno amesema kuwa chanzo cha mauaji ya wapenzi hao waliokutwa wamefariki dunia usiku wa kuamkia ni wivu wa mapenzi.

Kamanda huyo amesema mwanaume aliyejulikana kwa jina moja la Amos alimchoma kisu maeneo ya shingoni Esther maeneo ya shingoni kama mara tatu na kupelekea koromeo kutoka nje na akawa amemchoma kwenye mkono begani kisha yeye kujichoma kisu kwenye kitovu na kupelekea utumbo wote kutoka nje.

(Imeandikwa na Sharon Sauwa)

#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa
 
Watalaam wa criminology na forensic science wanasema upelelezi wa hizi case za homicides zinaanzia ndani then zinaenda nje. Kwa maana ya hao majirani plus faza house lazima wapelelezwe deeply halafu ndio upelelezi u extend hadi nje .Mfn mawasiliano ya victims wamefanya na nani and so on.
 
Mama mzazi wa marehemu Esther, Rachel Izengo amesema jina la mtoto wake ni Esther Ramadhani Isugilo na siyo Samira Mathias ambalo lilizoeleka mtaani.

Esther amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatatu Septemba 18, 2023 kwa madai ya kuchinjwa na mpenzi wake aliyefahamika kwa jina moja la Amos.

Mapema leo asubuhi mmliki wa nyumba aliyokuwa amepanga Esther ambako kulifanyika mauaji hayo, Yohana Nhembelo alisema ndugu wameomba chumba kilichofanyika kisifanyiwe usafi hadi watakapofika na kukiangalia.

Amesema amepata taarifa ya kifo cha mtoto wake kupitia kwa majirani saa 10.00 usiku wa kuamkia leo akiwa mkoani Shinyanga ambako ndiko anakoishi.

Amesema alianza safari muda huo na kufika jijini Dodoma saa 8:00 leo ili kujua sababu ya kifo cha binti yake ambaye ni mtoto wa kwanza kati ya watoto watatu alionao.

“Nimesikitishwa sana na kifo cha mwanangu cha kuchinjwa kwa sababu ni kifungua mimba na sikutarajia kama atakufa kwa kifo kama hiki. Binti yangu alikuwa ni mtu wa watu,”amesema huku akiangua kilio baada ya kushuhudia chumba kichofanyika mauaji hayo.

Ndugu wa marehemu wamesema baada ya kuangalia hali ya mwili wa mtoto wao ndipo watafanya uamuzi wazike wapi.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Martin Otieno amesema kuwa chanzo cha mauaji ya wapenzi hao waliokutwa wamefariki dunia usiku wa kuamkia ni wivu wa mapenzi.

Kamanda huyo amesema mwanaume aliyejulikana kwa jina moja la Amos alimchoma kisu maeneo ya shingoni Esther maeneo ya shingoni kama mara tatu na kupelekea koromeo kutoka nje na akawa amemchoma kwenye mkono begani kisha yeye kujichoma kisu kwenye kitovu na kupelekea utumbo wote kutoka nje.

(Imeandikwa na Sharon Sauwa)

#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa
dada kama anatumia majina bandia mbona kama kuna jambo hapa
 
Intelegensi nyepesi inaonyesha ya kuwa mwanaume huyo kwa wivu wake alimchinja dada huyo na yeye kujidhuru tumboni, Case closed!
 
SAFI SANA HAPO HAKUNA KESI,
KUNA UWEZEKANO UAMINIFU ZIRO NDIO CHANZO
 
Wewe kama ni mpelelezi hufai. Mlango kufungwa kwa ndani ndiyo iwe lazima waliopo ndani ndiyo wamefanya? Kama kuna dirisha na muuaji alitumia dirisha kuingia na kutoka je? Kama muuaji alikuwa amejificha darini wakati mwenye nyumba anaingia je? Kama ni mwenye nyumba amewaua halafu akatunga uongo je?
Je kama dirisha lina gril mtu anapitaje? Kama nyumba haina dari alijifichaje? Ok kama kulikuwa na huyo third person aliwezaje kutekeleza hayo pasipo kushtukiwa na majirani na hizo rapsha ?
 
Back
Top Bottom