Dodoma: Wanaodaiwa kuwa wapenzi wakutwa wamefariki

Dodoma: Wanaodaiwa kuwa wapenzi wakutwa wamefariki

Mmoja kati yao alifanya tukio maana mwenye nyumba anasema mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani
Kama muuwaji karukia dirishani akatoroka nalo linawezekana pia
Nafikiri mpenzi wake ndio kawafumania akawauwa wote wawili na kutoroka

Hii inawezekana pia
 
Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni wapenzi wamekutwa wamefariki dunia huku mwanamke akiwa amechinjwa na mmwanaume ambaye hajafahamika jina akiwa na jeraha kubwa tumboni lililosababisha utumbo kutoka nje.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu Septemba 18, 2023 katika Mtaa wa Oysterbay, Kata ya Dodoma Makulu kwenye chumba ambacho mwanamke aliyeuawa Samira Mathias alikuwa amepanga.

Akizungumza na Mwananchi katika eneo la tukio mwenye nyumba hiyo, Donald Nhembelo amesema alisikia kelele za kuomba msaada kutoka kwenye chumba cha mpangaji wake (Samira) saa 7.00 usiku.

Amesema baada ya kufika kwenye chumba hicho alisikia sauti ya mwanaume akiomba msaada ndipo alipouliza Samira yuko wapi na kujibiwa kuwa hawezi kuongea na yeye hawezi kusimama.

“Aliniomba nivunje mlango ili nimsaidie. Nilivunja ubao uliopo juu ya mlango (Venti) na kuingiza mkono kwa ndani na kufungua mlango na nilipowasha taa ndipo nilikuta Samira yuko juu ya kitanda amenyamaza,”amesema.

Amesema damu zilikuwa zimetapakaa kitandani na sakafuni huku mwanaume aliomba msaada ambaye hamfahamu akiwa amelala chini huku utumbo wake ukiwa nje.

Amesema baada ya kuona hali hiyo, aliripoti polisi ambao walifika kwenye eneo hilo ambao baadaye waliondoka na miili ya watu hao.

Balozi wa mtaa wa Oysterbay, Isaya Mabigiri amesema amepata taarifa za uwepo wa tukio kutoka kwa mwenye nyumba hiyo na alipokwenda alikuta miili ya watu.

MWANANCHI
Muke wa mutu sumu
 
Nimeachana na mke wangu wa ndoa miaka kibao bada ya kuniona nimechacha sasa Niko poa na nimeona mwanamke doctor bas anadai taraka na shampa how
Yuko sahihi Na ukitaka uhalali wa hiyo ndoa mpya bora ukubali talaka.La sivyo siku umedanja utashangaa sana(kaburini),maana huyo mke wa pili kisheria hatotambulika na hivyo kukosa hata vile vichache mlivyokusanya pamoja.Sawa ndugu zako waeza kumkingia kifua lakini sio rahisi kihivyo.
Bora muachane vizuri kwa talaka.
Kama kweli unampenda huyu mke mpya,muweke vizuri kisheria.La sivyo unampotezea muda
 
Faza hausi anasema mlango ulikua umefungwa anavunja ubao wa juu ndio akaingia.

Inamaana walimalizana ndani.



Najiuliza maswali yafuatayo

1. huo ubao wa vent wa mlango umekaaje kwa juu aweze kuvunja kisha afungue mlango akiwa nje kwa juu.. unless kama ni ile maana kitasa kinakuwa maeneo ya kifua au tumboni vent ya mlango iko juu je alipenya akashukia ndan kufungua mlango

Kwangu mie kama alivunja juu na kupenya ili afungue mlango maana yake aliweza kuwaona victima bila ya kuhitaji kufungua mlango hali ya waliokuw anayo alipaswa kuita polisi kabla hawajavunja mlango..


Ila kama anasema hakupenya alifungulia mlango kupitia vent nahitaj kujua aina ya hicho kitasa cha huo mlango ambacho mtu anaweza kufungua akovunja vent ya juu

Katika hali ya kawaida huyo mwenyw nyumba anahitaj kuwa ushahd wa kimazingara asiungwe kwenye kesi na hasa watu wamekufa na yeye ndo alikuwa kwenye eneo la
Tukio tena kavunja mlango bora angekuwa katoa taarifa mlango ukavunjwa na poliai au watu wengine wawepo na mwenyekit wa mtaa pia
 
Sasa hapo nani wa kwanza kumua mwenziye

Ova
 
Wauliwe afu mlango ufungwe kwa ndani, hapana mwanaume kahusika.
 
Back
Top Bottom