Uchaguzi 2020 Dodoma yazizima kwa Maandalizi ya Lissu kuchukua fomu 8.8.2020

October 2020 uchaguzi lakini mpaka sasa wanyanyembe hamjajipanga kwenye kitengo cha habari?
Mgombea wenu Lissu mpaka sasa hajajua aelekee wapi mpaka afundwe?
Hata ratiba za sikuu hamzijui?
Nyinyi hamna umakinifu hamuwezi kupewa nchi.

Sisi sio chama bali ni washabiki wa Cdm tunaotoa maoni yetu kupitia mitandao ya kijamii. Maoni yetu ni kwa ajili ya kuboresha, iwapo chama kitaona maoni yetu yanafaa watayachukua, na kama tayari wanayo watayaboresha zaidi. Kupewa nchi hatupewi kwa utashi wa ccm, bali kwa maamuzi ya wananchi.
 
Kipindi chake kipi?. Si kashamaliza miaka yake mitano.Vipindi vya uongozi ni miaka mitano mitano ikiisha unaomba tena. sasa wananchi ndo watakao amua urudi ikulu au uwe mstaafu ukachunge ng'ombe kijijini.
Binafsi sioni dhambi vyama vyote kumuunga mkono Magufuli amalize kipindi chake. Otherwise ni kupoteza fedha na rasilimali. Uchaguzi si vita, bali mchezo wa hesabu. Namba zilishagoma kwingine.
 
Chadema mlivyo na fitina mnataka muende kesho siku ya nane nane mkute milango imefungwa mje mseme mmenyimwa fomu.
 
Mkuu umasikini wako haujaletwa na CCM Bali ni uzembe wako wa kufanya kazi,ulitaka ccm ije ikuamshe asubuhi uende shambani
Hausikii wakulima wanavyokamatwa kisa kauza mazao nchi jirani kwa bei nzuri, ukipita vijijini haoni beria za kuzuia mazao, hauoni watu wanakamatwa kisa kakata mti wake alioupanda mwenyewe, wewe uko nchi gani labda!
 
WanaJF

Dodoma Inazizima.Ndivyo tunavyoweza kusema kwa Sasa.

Mapokezi kabambe yanamsubiri mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Antipass Lissu ambaye atachukua rasmi fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kesho siku ya Nane Nane.

Inatarajiwa mgombea huyo kusindikizwa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Dodoma katika kile kinachoonyesha Imani kubwa waliyo nayo kwa kiongozi huyo.

Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Lazaro Nyalandu ametoa wito rasmi kwa wakazi wa jiji la Dodoma na mikoa jirani kumsindikiza mgombea huyo Safari itakayoanzia makao makuu ya Chadema Kanda ya Kati.

Katika mahojiano na wakaazi kadhaa wa jiji Hilo wameonyesha shauku kubwa ya kutaka kumuona Tundu Lissu ikiwa ni miaka mitatu alipoondolewa katika jiji Hilo akiwa nusu mfu baada ya kupigwa risasi kumi na sita na watu wasiojulikana na Sasa anarejea jiji Hilo Hilo akiwa mzima wa afya na akitembea kwa miguu yake miwili huku wabaya wake waliotaka kumuua wakifichama kusikojulikana.

Hapo Jana wanafunzi wa vyuo vikuu vya UDOM, CBE na Mipango walikuwa katika vikao vya namna ya kumsindikiza Lissu ambaye walimwita shujaa wao.

Tundu Lissu amejizolea uungwaji mkono na umaarufu mkubwa kutokana na sera yake ya kuwapa watu Uhuru wa kusema na kutoa maoni yao bila kuingiliwa na vyombo vya Dola endapo atachaguliwa kuwa Rais.Na pia kuruhusu vyama vya siasa. NGO's na vyombo vya Habari kufanya kazi zake kwa Uhuru Kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Chadema leo inatarajiwa kutoa ratiba njia atakazopita mtetezi huyo wa wanyonge na Msemaji wa wasio na sauti ili walau watu kujipanga manjiani kumsalimia na kumsindikiza.
Muwe waangalifu sana Chadema.Kuruhusu umati wa watu wamsindikize Lissu kwenye ofisi za Uchaguzi ni kujitafutia matatizo yasiyo ya lazima.CCM ingeweza kuweka msululu wa watu barabarani wakati mgombea wao anaenda kuchukuwa Fomu lakini hawajafanya hivyo na haikuwa kwa bahati mbaya.MUWE WAANGALIFU.Lissu akachukuwe Fomu na kuongea na wananchi kwa mfumo ule ule aliotumia mgombea mwenzake.Mambo mengine SUBIRINI KAMPENI ZIKIANZA.

Bila shaka mliona jana kulivokuwa na utulivu katika ofisi za Uchaguzi wakati mgombea wa CCM alivyoenda kuchukuwa Fomu yake.Nashauri kesho iwe hivyo hivyo.TAFADHALINI.
 
Yetu macho mlishaambiwa mambo ya kwenda ofisi za NEC na umati campaign bado. Hakuna alietangaza anaenda kuchukua form na akaenda na umati.

TBC wameliongelea sana jana anaetakiwa kwenda ofisi za NEC ni mgombea, mgombea mwenza na katibu mkuu wa chama. Ndio maana CCM wakaenda kukutana na wapambe wao huko kwenye ofisi zao baada ya kuchukua form tena wakajifanya hata hiyo ni surprise.
 
Muwe waangalifu sana Chadema.Kuruhusu umati wa watu wamsindikize Lissu kwenye ofisi za Uchaguzi ni kujitafutia matatizo yasiyo ya lazima.CCM ingeweza kuweka msululu wa watu barabarani wakati mgombea wao anaenda kuchukuwa Fomu lakini hawajafanya hivyo na haikuwa kwa bahati mbaya.MUWE WAANGALIFU.Lissu akachukuwe Fomu na kuongea na wananchi kwa mfumo ule ule aliotumia mgombea wa mwenzake.Mambo mengine SUBIRINI KAMPENI ZIANZA.
Jamaa wana matatizo makubwa halafu watakuja kupiga kelele hapa; yaani wanatafuta kila sababu ya kuchokozana na NEC au polisi.
 
WanaJF

Dodoma Inazizima.Ndivyo tunavyoweza kusema kwa Sasa.

Mapokezi kabambe yanamsubiri mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Antipass Lissu ambaye atachukua rasmi fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kesho siku ya Nane Nane.

Inatarajiwa mgombea huyo kusindikizwa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Dodoma katika kile kinachoonyesha Imani kubwa waliyo nayo kwa kiongozi huyo.

Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Lazaro Nyalandu ametoa wito rasmi kwa wakazi wa jiji la Dodoma na mikoa jirani kumsindikiza mgombea huyo Safari itakayoanzia makao makuu ya Chadema Kanda ya Kati.

Katika mahojiano na wakaazi kadhaa wa jiji Hilo wameonyesha shauku kubwa ya kutaka kumuona Tundu Lissu ikiwa ni miaka mitatu alipoondolewa katika jiji Hilo akiwa nusu mfu baada ya kupigwa risasi kumi na sita na watu wasiojulikana na Sasa anarejea jiji Hilo Hilo akiwa mzima wa afya na akitembea kwa miguu yake miwili huku wabaya wake waliotaka kumuua wakifichama kusikojulikana.

Hapo Jana wanafunzi wa vyuo vikuu vya UDOM, CBE na Mipango walikuwa katika vikao vya namna ya kumsindikiza Lissu ambaye walimwita shujaa wao.

Tundu Lissu amejizolea uungwaji mkono na umaarufu mkubwa kutokana na sera yake ya kuwapa watu Uhuru wa kusema na kutoa maoni yao bila kuingiliwa na vyombo vya Dola endapo atachaguliwa kuwa Rais.Na pia kuruhusu vyama vya siasa. NGO's na vyombo vya Habari kufanya kazi zake kwa Uhuru Kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Chadema leo inatarajiwa kutoa ratiba njia atakazopita mtetezi huyo wa wanyonge na Msemaji wa wasio na sauti ili walau watu kujipanga manjiani kumsalimia na kumsindikiza.
Hahahahahahhahahahihihihihiihihihhhohohohohoohohohuhuhuhuhuuhuh
 
Jamaa wana matatizo makubwa halafu watakuja kupiga kelele hapa; yaani wanatafuta kila sababu ya kuchokozana na NEC au polisi.
Kuna mahali popote Chadema imesema inachokoza mtu?
 
Wewe hujui unachoandika humu.
Binafsi sioni dhambi vyama vyote kumuunga mkono Magufuli amalize kipindi chake. Otherwise ni kupoteza fedha na rasilimali. Uchaguzi si vita, bali mchezo wa hesabu. Namba zilishagoma kwingine.
 
Mzee wenu Jiwe anavyocharuka Ziarani ninyi mnamuona Lissu tu .Na apunguze maneno
Usilinganishe raisi wa nchi na raia wa kawaida. Raisi atazunguka popote kutimiza majukumu yake. Hatuna maraisi wawili nchi hii. Hiyo ndiyo incumbency advantage.
 
Yetu macho mlishaambiwa mambo ya kwenda ofisi za NEC na umati campaign bado. Hakuna alietangaza anaenda kuchukua form na akaenda na umati.

TBC wameliongelea sana jana anaetakiwa kwenda ofisi za NEC ni mgombea, mgombea mwenza na katibu mkuu wa chama. Ndio maana CCM wakaenda kukutana na wapambe wao huko kwenye ofisi zao baada ya kuchukua form.
Wewe Jana uliona CCM walienda watu watatu tu? Fear of Unknown
 
Hausikii wakulima wanavyokamatwa kisa kauza mazao nchi jirani kwa bei nzuri, ukipita vijijini haoni beria za kuzuia mazao, hauoni watu wanakamatwa kisa kakata mti wake alioupanda mwenyewe, wewe uko nchi gani labda!
Amejifunika shuka hataki kutizama
 
Back
Top Bottom