Bwana
Infantry Soldier,
Demokrasia kama nadharia na kanuni ya kiutawala husisitiza kwamba uhalali wa utawala wowote ule duniani ni lazima utoke kwa wananchi na siyo vinginevyo, pia uhalali wa utawala ni lazima ulenge katika kuwafanya hawa wananchi wapate maendeleo. Hapa unaweza ukawa na mfumo wa aina yoyote ile, aidha Ufalme (A Monarchy), Udini (A Theocracy) au Jamhuri (A Republic) muhimu kabisa ni kwamba lazima nguvu itoke kwa wananchi na siyo vinginevyo.
Watawala lazima watawale kwa matakwa ya wananchi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa baina ya watawala na watawaliwa. Watawala hawatakiwi kufanya jambo lolote lile ambalo litaathiri mustakabali wa wananchi bila wananchi kuhusishwa. Wakijiamulia tu mambo, tena ambayo yanaumiza watawaliwa basi uhalali wao wa kutawala unapotea.
Wanafalsafa wa kale kama
John Locke,
Thomas Hobbes na
Jean-Jacques Rousseau walizungumzia kitu kiitwacho
The Social Contract ambapo walisema mataifa hutengenezwa kwa makubaliano baina ya watawala na watawaliwa. Pindi watawala wanavunja hayo makubaliano na kujiamulia kufanya jambo ambalo litawadhuru wananchi wao basi wanapoteza uhalali.
Nakubaliana na
Mzee Nyerere kwamba kila sehemu ina Demokrasia yake, japo lazima tukubali kwamba tunaweza kutoa tafsiri mbalimbali za demokrasia na tusiwe na tafsiri moja kuhusu demokrasia. Lakini nachelea kusema kwamba lengo la demokrasia ni moja tu duniani kote, kwenye mifumo yote ya utawala nalo ni "KUHAKIKISHA NCHI INAWALIWA KWA KUFUATA MATAKWA YA WATAWALIWA"
Hivyo basi naweza kumaliza kwa lugha ya kiingereza kwa kusema haya yafuatayo "Democracy as a value does not have a single accepted Universal definition. We can only define Democracy well through a Purposive Approach of what democracy aims to achieve within a particular society. And that is Ensuring the power to rule is derived from the people for their benefit: Suffice to say it, such benefit should always be just, moral and equitable"
NB: Tusijitie moyo, katika hili wenzetu wazungu pamoja na Ubepari wao wametushinda mbali sana. Kitendo cha kutawala kwa kufuata miiko ya kisheria kwa manufaa ya wananchi ndicho kimewafanya wafike hapa walipo leo: Sisi Afrika hata Katiba kuheshimu ni shida, utasemaje kwamba tuna demokrasia yetu ???