Does Africa have its own (unique) definition of democracy?

Does Africa have its own (unique) definition of democracy?

Kwa uelewa wangu mdogo kuna mambo mawili
1.Kwa asili ya Africa hatuwezi kuwa na mfumo wa demokrasia kwa vitendo kwa jinsi tulivyo tangu kuumbwa(ndo maana nchi duniani hata waliona bora wajitafutie mfumo wao tuu utakaoendana nao
2.Au bado hatujafikia kiwango cha kuwa na mfumo wa demokrasia kwa sababu mbalimbali
Definition itabaki kuwa vilevile ila kimatendo haitafanya kazi ila tutabakai na vitabu vya wasomi na kujaza maktaba
 
Afrika tunao wasomi ila wenye akili wachache mno tuliobaki nikiwemo MIMI huwezi kuleta mfumo wa utawala wenye mazingira tofauti, tamaduni tofauti mtindo wa Maisha tofauti , halafu eti uwe global ni Upuuzi.

Mashirika ya kijasusi ya magharib kama NED(National Empowerement for Democracy), USAID, na mengine wale kazi yao ni kutengeneza chaois, vurugu, uhasama miongoni mwetu, hata tunatwangana risasi, tunashadadia wahuni na mikataba yao.

Bora hata huyu alichosema
 
Kuna mtu alisema “Africa is no place for Democracy” mwingine akasema “we can apply it (democracy) but not down to the latter “
wote hao walikuwa marais
 
Democracy ni Democracy mkuu...ina ingredients zake ili iwe Democry na hii ni kwa ulimwengu mzima...kama kuna vitu essential havipo hiyo haiwezi kuwa Democracy hata kama iwe ni America.

Mfano huwezi sema Tanzania kuna Democracy kwa sababu tu kila baada ya miaka kumi Rais mmoja humpisha mwingine kupitia uchaguzi mkuu wa vyama vingi...ikiwa nguvu ya mwananchi inabanwa au kuminywa vilivyo na tabaka tawala likitumia vyombo vya ulinzi na usalama Viki act kwa maslahi yao...maandamano ya Amani yanayoruhusiwa ni Yale tu ya wakatoliki ya Siku ya Mitende...kinyume na hapo utaambiwa utaatarisha usalama wa nchi...wakati ni haki ya kikataba na katiba ndiyo agano kuu la wananchi kwa ujumla na utawala kuikiuka ni kukiuka makubaliano ya wananchi juu ya utawala uweje...ni kukiuka haki zao za msingi...so huwezi kuchukua kigezo cha uchaguzi tu na Kusema Tanzania kuna Democracy... Inabidi utafute jina la kutumia hapo siyo Democracy.
 
Back
Top Bottom