Dogo wa kazi kaambiwa aripoti ofisi ya serikali ya mtaa juma tatu asubuhi

Dogo wa kazi kaambiwa aripoti ofisi ya serikali ya mtaa juma tatu asubuhi

Jumamosi ya mwisho wa mwezi ni ya usafi huku adi sa 4 asubui , Leo asubui dogo kafungua goli (salon) sa 3 na nusu , gafla kaja mtendaji kamuuliza jina na kuchukua namba yake ya simu, kisha kamwambia Leo hajafanya usafi aripoti ofisini juma 3.

Dogo kabaki ameshangaa maana hata ofisi ya serikali ya mtaa hajui, anamiez 4 toka aje huku iringa, ndipo kanipigia simu asubui nilikua kazini,

Nimempanga kua aende juma akasema yeye ni mgeni hajui utaratibu huu.

Mimi nilisahau kabisa maana miaka 3 nilikua kijijini na kule hamna huu utaratibu, hata hapa nashangaa Leo ndo wamekuja siku zote anafungua muda ule ule huu mwez wa 4 sasa

Mimi nitakua kazini hiyo juma 3 ningeenda mimi, nasikia jirani yake kamwambia asiemde adi apigiwe simu, ila mi naona bora aende tu akasikie anachoitiwa..

Aliewahi kutana na changamoto hii au mwenyewe uelewa hapa ili nisije pigwa faini. Asanteni
Kutojua sheria haihalalishi kutopewa adhabu. Aitikie wito na kuongea nao.
 
Kwa level ya Halmashauri swala la kutofanya usafi siyo kosa la kubuni ni kosa kweli 😅

Mtendaji ni mwakilishi wa mkurugenzi wa halmashauri kwa level ya kata so ana-wield similar power. Dogo akileta drama anaweza wekwa ndani kwa amri ya mtendaji 😅

Mleta uzi, tafuta namba ya mtendaji muelezee. Omba radhi, msikie atasema nini. Faini ya usafi ni pesa ndogo kwa mtendaji hua wana mirija mingi hao
Asisahau kumpa posho mtendaji👿
 
Umeeleza vyema sana.
 
kaka hao jamaa wakiamulia jambo hawaangalii ugeni,kikubwa akienda ofisini aende na chochote ila awasikilizie kwanza asiingie kichwa kichwa
Changamoto dogo mgeni mgeni afu mwoga mwoga sana nawaza nikimpanga wakimchalenji kidogo tu ataingia kingi
 
dah aisee nipange boss dogo akajieleze vip
Awe msikilizaji sana kuliko kuwa muongeaji ila aongee kama nimuongeaji mzuri..ushauri wangu asitetemeke aeleze anachokijua kwamba alikua hajui na hakubahatika kuona utaratbu huo kwa kipindi alchofika hapo, aombe radhi awaambie yeye ni raia mwema na mtii ndo maana amefika hapo kusikilza aombe asipigwe faini asisitize hilo kama kutakua hakuna wapambe pembeni acheze na mazingira mwisho anyooshe mkono ata kwa kifaru kujilinda kwa siku za mbeleni.
 
mambo ya kifaru sio atahisiwa anatoa Rushwa boss samahan lakini ni maoni tu
 
Changamoto dogo mgeni mgeni afu mwoga mwoga sana nawaza nikimpanga wakimchalenji kidogo tu ataingia kingi
Basi akifika awaombe uongee nao japo ukileta chain nao wataona chakula ipo hapa…ubaya wa hao watu wanaweza kutaka kukuonyesha nguvu yao wakamzuia ata masaa kazaa yaan basi tu…mwambie dogo atoke na chochote kitu alafu wewe ndo utampa maelekezo baada ya kuongea nao kama yeye n muoga muoga. ila atajifunza lini kuongea na binadamu wenzie😂😂
 
nashukuru ngoja tuone mkuu labda atakomaa
 
Faini ya kutofanya usafi ni elf 50 hapo hapo wakikuita ofisini mnaweza kuongea na mkayamaliza.
 
Utaratibu wa usafi wa mwisho wa mwezi upo kwa mujibu wa sheria ndogo za utunzaji mazingira almost halmashauri zote nchini wanacho hicho kitu

Kutokujua sheria sio kinga dhidi ya kosa ulilotenda, hivyo kusema mi mgeni, sijui kusoma, sijaambiwa. Haikusaidii chochote.

Kikubwa aende akasikilize, aongee nao kwa heshima hata akimkuta mtendaji ni bwa mdogo au sista du, heshima kwanza, yanazungumzika.
 
Back
Top Bottom