Dokezo la Kisera Kuhusu Changamoto ya Usafiri wa Pantoni Kati ya Magogoni na Kigamboni: Serikali ibinafsishe usafiri wa Pantoni

Dokezo la Kisera Kuhusu Changamoto ya Usafiri wa Pantoni Kati ya Magogoni na Kigamboni: Serikali ibinafsishe usafiri wa Pantoni

Doctor Mama Amon

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
2,089
Reaction score
2,725
1723298817649.png

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa

1. Usuli

“Kama una haraka tangulia lakini ujue nitakukuta feri,” ni msemo uliozoeleka kwa wakazi wa Kigamboni tangu uhuru wa Tanganyika hadi leo. Mtu anasafiri kutoka Kibada hadi Feri kwa dakika 15 lakini anasubiri pantoni kwa dakika 60.

Dokezo hili linajenga hoja kwamba wakati umefika kwa serikali kuruhusu biashara huria katika eneo la Magogoni ili kumaliza kadhia hii, kama ambavyo boda boda, bajaji na daladala zimekuwa jibu la matatizo ya usafiri kutoka Mbezi Luis hadi Katikati ya mji.

Kwa ajili hii, mapendekezo manne yanatolewa ili kuwapa wakazi wa Kigamboni furaha walioyoikosa tangu 1961.

  • Mosi, wasafiri walio tayari kulipia nauli ya TZS 1,000/= hadi 2000/= katika vivuko binafsi kama vile Azam Sea Taxi wapewe uhuru huo kuanzia sasa, kama jawabu la muda mfupi.
  • Pili, serikali kuu inunue Sea-Taxi kama hizo zinazomilikuwa na kampuni Azam, na kuziweka pale Magogoni, ili kutoa uhuru wa wasafir kuchagua aina ya usafiri wanaoutaka na kuuweza (price diversity), huu ukiwa ni mkakati wa muda wa kati.
  • Tatu, wakati huu ambapo kuna kivuko kimoja, na serikali haijanunua sea-taxi zake, Azam waruhusiwe kutoa huduma tangu asubuhi hadi jioni kwa bei ya soko badala ya kubanwa na sharti la TZS 200/= ya sasa.
  • Na nne, katika mkakati wa muda mrefu, serikali ianzishe mkakati wa kuhamisha bandari ya dar es Salaam na kuipeleka kweney ufukwe wa Coco-Beach ili kutoa mwanya wa kujengwa kwa Daraja la kudumu pale Magogoni.
Pantoni1.jpg

2. Utangulizi: Kuna tatizo gani?

Kulingana na Kamanya Chumila Sogoye na wenzake watatu (2024), Tanzania inayo maeneo manne ya maji yanayotumia pantoni. Maeneo hayo ni Bahari ya Hindi, Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, na Ziwa Nyasa. Katika Ziwa Victoria pantone zinaunganisha miji ya Bukoba, Musoma, Mwanza, na Ukerewe, vikiwemo visiwa vidogo vipatavyo 50. Na katika Bahari ya Hindi, pantoni zinaunganisha wilaya za Ilala na Kigamboni, ilala ikiwa ni kitovu cha jiji kibiashara.

Kwa ujumla, Jiji la Dar es Salaam ni kitovu cha shughuli za kila siku zinazofanywa na wakazi wake kutoka kona mbalimbali hadi kwenye kitovu chake kiitwacho Posta Mpya, na kisha kurudi nyumbani kwao jioni.

Nimesafiri kutoka ufukwe wa Magogoni kwenda ufukwe wa Kigamboni na kurudi Magogoni kwa njia ya Pantoni. Pale kuna tatizo kubwa la usafiri. Nimeona Pantoni moja tu ndio linafanyakazi Kigamboni.

Nyingine nimeambiwa zimeharibika na ziko matengenezo huko Kenya. Kashikashi ya kusukumana kuwahi kuingia ni kubwa. Watu wanachelewa kuingia kazini, kufanya kazi zao za uzalishaji, na hata kurudi nyumbani kwa wakati. Uchambuzi ufuatao unalenga kuweka bayana umuhimu na uhara katika kutatua Changamoto ya Usafiri wa Magogoni-Kigamboni.

Pantoni2.jpg


3. Utaratibu wa utafiti

Utafiti huu umefanyika kwa kushiriki usafiri wa Pantoni ya Kigamboni-Magogoni, kuhoji wasafiri wenzangu, na kupitia kumbukumbu za kimaandishi. Kwa ajili ya utafiti huu, maswali yafuatayo yalipaswa kujibiwa:

  • Watu wangapi wanasafiri kutoka Kigamboni hadio Posta Mpya na kududi Kigamboni kila siku?
  • Wasafiri hawa wanatumia usafiri gani?
  • Wanayo maoni gani kuhusu kiwango cha ubora wa huduma wanazozipata? Kwa nini kuna msongamano mkubwa pale Magogoni?
  • Kwa nini pantoni inachelewa kuvusha abiria? Kwa nini pantoni ndogo zinaanza saa 12 na kusitisha huduma saa 3 asubuhi, na tena kuanza saa 10 mchana na kusitisha saa 12 jioni?
  • Ni sababu gani zinaathiri ubora wa huduma za pantone katika feri ya Kigamboni?
  • Hatua gani zichukuliwe ili kuwa furaha wakazi wa Kigamboni wanaokuja Posta Mpya kila siku?
Ferry--MV Kazi.PNG

4. Matokeo ya utafiti

Utafiti huu umeonyesha kwamba, kwa mujibu wa sensa ya mwala 2022, Halmashauri ya Kigamboni inao wakazi 317,902 wanaume wakiwa 156,400 na wanawake 81,733, wakiwa wanaishi katika kaya 43,166 zenye watu 5 kila moja. Watu wapatao 150,000 husafiri kila siku kutoka Kigamboni Kwenda wilaya ya Ilala kwa kutumia pantone za Magogoni.

Aidha, imebainika kwamba, Pantoni zilizo katika Feri ya Magogoni zinaendeshwa na Tanzania Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (Tanzania Electrical, Mechanical and Electronics Services Agency -TEMESA).

Kuna umbali wa meta 300 kutoka ufukwe wa Magogoni hadi ufukwe wa Kigamboni. Pantoni kubwa huweza kubeba watu 100-500 kwa raundi moja, bila magari. Hadi 2017 kulikuwa na pantone tatu.

Kwa sasa kuna pantone moja pekee. Zamani, wakati wa mchana, pantoni ilikuwa inaondoka upande mmoja Kwenda upande wa pili kila baada ya dakika tano, kwa wastani. Kwa sasa, wakati wa mchana, pantoni inaondoka upande mmoja Kwenda upande wa pili kila baada ya dakika 45, kwa wastani.

Utafiti huu umeonyesha kwamba, kuna watu wanatoka Kibada na fukika feri kwa robo saa. Lakini, wanalazimika kusubiri pantoni iliyo upande wa pili kwa saa moja, msafiri mmoja alisema.

Kama kuna meli inapita, wanasubiri kwa saa moja na nusu, maana meli lazima zikatize kwanza kabla ya pantoni kuanza safari.

Kigamboni kuna wakazi wanafanya kazi upande wa pili wa Magogoni, kama vile Posta Mpya. Wanachelewa sana ofisini. Kuna pantoni ndogo za Azam zinaitwa Sea Taxi.

Lakini zinafanya kazi kuanzia saa 12.00 asubuhi hadi saa 3.00 asubuhi. Kisha zinarudi jioni kuanzia saa 10.000 mchana hadi saa 12.00 jioni.

Kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi mchana, safari za Kigamboni kwenda Magogono na kurudi ni kero kubwa.

Utafiti umebainisha kuwa, sababu zinaathiri ubora wa huduma za pantone za Magogoni ni Pamoja na haya:

  • Pantoni za tekinolojia duni, kwa maana ya injini dhaifu;
  • Serikali kuwa na tabia ya kununua pantoni mitumba;
  • Serikali kukosa ubunifu wa kununua pantone ndogo zenye kazi kama zile sea-taxi za Azam;
  • Kigugumizi cha serikali kubinafsisha usafiri wa magogoni ili bei ya soko ianze kufanya kazi; na
  • Uwepo wa bandari ya Dar es Salaam inayokwaza kasi za pantone kila mara meli kubwa zinapikuwa zinapita.
Msafiri mmoja alitoa mfano wa usafiri wa Mbezi Luis Kwenda Posta unaotumia mabasi ya BRT, daladala, bajaji, na bodaboda, ambapo kila abiria anakuwa na uhuru wa kuchagua kulingana na mfuko wake Pamoja na uharaka wake.

“Ubunifu wa aina hii haupo pale feri ya Magogoni,” anasema msafiri huyo aliyejitambulisha kama mkazi wa KIbada.

Kwa ufupi, ni wazi kwamba, kuna tatizo la usafiri wa umma hapa. tatizo hili linachangiwa na taratibu za usafiri wa meli zinazotia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam.


1723299048867.png

5. Mapendekezo ya kisera

Hivyo, kutokana na matokeo ya utafiti yaliyobainishwa hapo juu, ni wazi kuwa hatua za kisera zinahitajika kutokana na ushirikiano wa Wizara zaidi ya moja. Hivyo, Waziri Mkuu anayo nafasi kubwa katika kukabiliana na changamoto hii. Mapenekezo yafuatayo yanahusika:

  • Mosi, wasafiri walio tayari kulipia nauli ya TZS 1,000/= hadi 2000/= katika vivuko binafsi kama vile Azam Sea Taxi wapewe uhuru huo kuanzia sasa, kama jawabu la muda mfupi.
  • Pili, serikali kuu inunue Sea-Taxi kama hizo zinazomilikuwa na kampuni Azam, na kuziweka pale Magogoni, ili kutoa uhuru wa wasafir kuchagua aina ya usafiri wanaoutaka na kuuweza (price diversity), huu ukiwa ni mkakati wa muda wa kati.
  • Tatu, wakati huu ambapo kuna kivuko kimoja, na serikali haijanunua sea-taxi zake, Azam waruhusiwe kutoa huduma tangu asubuhi hadi jioni kwa bei ya soko badala ya kubanwa na sharti la TZS 200/= ya sasa.
  • Na nne, katika mkakati wa muda mrefu, serikali ianzishe mkakati wa kuhamisha bandari ya dar es Salaam na kuipeleka kweney ufukwe wa Coco-Beach ili kutoa mwanya wa kujengwa kwa Daraja la kudumu pale Magogoni.
Kwa kuwa mapendekezo haya yanagusa Wizara zaidi ya moja, ni wakati mwafaka sasa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuchukua hatua.
1723299199124.png


6. Marejeo

  • Kamanya Chumila Sogoye and three others (2024), “Factors Affecting Service Quality at Kigamboni Ferry Terminal A Case Study of Dares Salaam Region,” International Journal of Economics and Financial Management (IJEFM), Vol 9.3: 80-92.
  • Kigamboni Municipal Council: Second Strategic Plan 2021/22 - 2025/26, dated September 2022.
  • URT(2008), Dar es Salaam Transport Policy and System Development Master Plan: Final Report (JICA)
 
nimesoma na kumaliza yote.
nasemaje si kwa serikali ya sisiemu.
suala la Kigamboni itoshe kusema serikali haina hata huo mpango wa kuitatua.
 
Mi nadhani hawashindwi kuweka vivuko vya kuaminika. Hapa nanusa mipango ya makusudi ya kulazimisha magari yapite darajani na kuongeza Hela kwenye fuko la NSSF ambalo hatujui linajaa lini ili watu wapite bure.
 
Tangu lini serikali hii ya ccm ikaweza kuendesha mradi
Pantoni tu hapo wana mbwelambwela
Mwendokasi hoiiiii
Hii SGR wameanza kwa mbwembwe mapichapicha maselfie ila huko mbeleni tunajuwa nini kitatokea

Ova
 
Hatimae yametimia.
Mama anaupiga mwingi sana
 
Back
Top Bottom