DOKEZO Dola zimeadimika, bei ya black market ni Tzs 3000-3200 kwa noti za $.50 & 100

DOKEZO Dola zimeadimika, bei ya black market ni Tzs 3000-3200 kwa noti za $.50 & 100

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwa zaidi ya siku 10 nimekuwa nikitafuta dola 12,000 kwa ajili ya kuweza kuagiza vitu fulani China.

Nimezunguka kwenye mabenki yote makubwa, jibu lao hatuna USD. Nimeenda bureau de change, nako nimezunguka sana.

Jana jioni nikafika kwenye duka moja la kubadilishia fedha, nilipoingia ndani wakaniambia hawana dola, nikatoka nje. Mlinzi akaniita, akasema dola ni Tzs 3,200/ nikasema that's too much, wakanishusha hadi 3,000/-

Mama yangu Samia Suluhu Hassan, hii hali ni mbaya, huko tunakoelekea nchi itaweza kuingia kwenye mfumuko mkubwa sana wa bei, hyper inflation, maana dola ni adimu, inapatikana kwa gharama kubwa. Hii itapelekea kupanda sana kwa bei ya bidhaa hasa ukizingatia zaidi ya 95% ya bidhaa tunazozitumia tunaagiza kutoka nje ambako tunanunua kwa pesa za kigeni.
we kapuku huna lolote unaleta uzushi wa kipuuzi tu ujaribu kuichafua serikali yetu. dola 12,000 hauko serious!
 
Kuna wakati kiongozi mmoja ali-comment kuhusu hali mbaya ya Dola Kenya, na akasema walikuwa wanakuja kwetu kutafuta Dola.
Sasa kwetu yametukumba!
Itabidi mchumi first class Dr Mwigulu PhD aketi na Bingwa wa Uchumi Duniani Prof Lipumba waweze kutufanyia Wepesi!
 
Hahahaaahaaaa aisee pole Sana hakika wewe ni mshamba Sana na hujiekewi!! Ndio nyie mliamini Magufuli alikuwa Mungu!! Kwa taarifa Yako hili ni tatizo la Dunia nzima hata angekuwepo huyo Mungu wako lingetokea tuu!!?
NB : Mama kapandisha mishahara,madaraja,pia ameajiri wakati Mungu wako walishindwa!!!
Suk gang ziiiiiiiiiiii
Nina hakika kama hili lingetokea akiwapo hali ingekuwa mbaya zaidi!
 
we kapuku huna lolote unaleta uzushi wa kipuuzi tu ujaribu kuichafua serikali yetu. dola 12,000 hauko serious!
Yupo sawa, kuna upungufu wa dola. Wengi wanasuffer kwa sasa. Kama upo iselamagazi hili suala halikuhusu
 
Itakua cute wife na mzungu wake wameficha dola nyingi sana. Vyombo vya dola fanyieni kazi hili
 
Sio Kenya tuu Hadi Uturuki..

Ni hivi mfumuko wa bei ya vitu Duniani ulioanzia kwenye Uviko na Sasa vita za Ukraine umesababisha shida hiyo kwenye Nchi nyingi za Dunia.

Kuanzia Ghana Hadi Egypt huko wanaomba mikopo imf Ili kukojoa uchumi zao..
Tanzania tuna nafuu sana na kinachotuokoa ni kwamba vyakula vingi hatuagizi Nje,sie vitu vya viwandani ndio tunaagiza so Serikali inaweka kufanya rationing na maisha yakaenda vizuri.

Bashe anajua kama mavuno yalikua kidogo hivo wakenya waliojazana mashambani kusomba mpunga anazidi kuwachekea au kajifunza somo la usalama wa chakula?
 
Tatizo nchi sasa iko mikononi mwa mafisadi papa, eti Mwigulu awe waziri wa fedha nchi ibaki salama? Samia anayajua hayo na ana sababu zake za kuyafumbia macho
Mkuu hapo naona wanaachiana ulaji
Wee kula huku ila na mimi niachie huku
Huoni Mwinyi kaenda kumuwakilisha Qatar na ameomba waje kuwekeza ZNZ?

Acha nihamie znz tu sasa
 
Katika mambo nimejifunza kipindi hiki ni haya mawili.

La kwanza ni usijidanganye mwanamke anajeuri au uwezo wa kuongoza jamii yeye kama yeye mwisho wa siku ni hasara na fedheha kama tunayopitia. Ni sawa na kumpa kondoo aongoze kundi la mbwa mwitu kama kiongozi wao hiyo ni ndoto, kondoo hajui njia za mbwa mwitu.

La pili, tujitahidi sana viongozi wa ngazi ya majimbo na taifa yaani kuanzia wabunge, mawaziri kwenda juu hadi raisi wawe ni watu wenye exposure ya maisha na tutazame sana makuzi yao waliyopitia utotoni.

Tuepuke watu waliopitia hali ngumu sana ya maisha wakatoboa kwa shida, tuepuke watu waliolelewa na mzazi m'moja yaani mama, tuepuke viongozi ambao hawapo ndani ya familia ya Baba,mama,watoto na wanaupendo na familia na wake zao, tuepuke watu ambao walithubutu hata kupanda stejini enzi za ujana wao kukata mauno ati kwaajiri ya kujifurahisha, tuepuke watumia kilevi waliokubuhu na watu wanaopenda ngono.

Kwa kifupi tuwe na screening kali sana na tuondoe huu mfumo wa chama cha kisiasa kutuamulia nani na nani awe raisi wa taifa.

Halafu na huu muungano utazamwe upya kwamba nani analeta shida na maslahi yake yajulikane wazi wazi yasiwe ya kificho usiwe muungano wa mashaka bali uwe muungano wa uwazi na wa kueleweka.

Inaisikitisha sana, uchumi wa taifa unaelekea shimoni kosa ni Mchunga mbuzi kupewa ofisi ya wizara ya fedha anapigwa matobo hadi basi.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Hii sio ishu ya Samia ni dunia nzima dola imekuwa adimu, nenda hapo Kenya hali ni mbaya zaidi.
Acha kutetea. Baba yako anampiga mama yako watu wanahoji kwann huyu mzee anampiga huyu mama wewe mtoto wake unasema sio mama yangu tu wamama wengi wanapigwa na wanaume zao, hivi unakuwa na akili timamu kusema hivyo?!

Hapa tunazungumzia crisis ya dollar katika uchumi wa Tanzania, wewe unakuja kufanya comparison as if tunashindanisha mataifa hapa. So kama Kenya wana the same issue ndio turelax na tusiiwajibishe serikali katika kutafuta mbinu ya haraka kutatua tatizo?!

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom