Dola zimeadimika kwasababu wageni wanavuna fedha za miradi kuliko wazawa

Inategemea na time frame, not miradi yote tunaweza fanya kwa style hiyo.
Although ninwazo zuri
Ni lazima yote kufanya hivyo.Kama tumepiga marufuku kuchimba Madini mkakati bila kufanya value addition ndani ya Nchi hilo la wakandarasi ni very minor ,na miradi ya hivyo ratio iwe 60% vs 40% au hata 50% vs 50% kabisa
 
kama ulikua hujui nikwambie tu kuwa hao wakandarasi wa bongo ni tia maji sana, wengi wao ni wezi na hawako punctual kwenye kazi zao, uvivu [kazi ya mwezi itakamilika ndani ya mwaka kwa visingizio vingi sana] - talking from experience.
Shida kubwa kwa wakandarasi wazalendo ni kucheleweshewa malipo. Ukishapewa malipo ya mwanzo hayo madai mengine haulipwi kwa muda wa siku 28 kadri ya mikataba baada ya tathmini ya kazi iliyokwishakamilika. Wanasingizia pesa haijatoka wizarani. Pia wizarani wanatoa kipaumbele kwa wa nje maana watashtaki ila wa hapa ukishtaki mwisho wa kupewa tenda. Hivyo ulipaji ndio unaochelewesha kazi kwa wakandarasi wazalendo. Kama ni uongo kila mwaka bajeti wanasema kuna madai ya wakandarasi. INAKUWAJE PAWE NA MADAI AMBAYO NI KAZI ZILIZOPIMWA NA KUHITAJIKA KULIPWA KWA MUDA WA MKATABA MPAKA MADAI HAYO YAWEKWE KWENYE BAJETI WAKATI TAYARI PESA ILIKUWEPO KATIKA MWAKA UNAOISHA KABLA YA BAJETI? HIVYO TUNAJIFICHA KWA WAKANDARASI WAZALENDO JUU YA UKOSEFU WA PESA. MASIKINI MPAKA WENGINE WANABANWA NA MABENKI WALIYOKOPA. WAKANDARASI NA WALIPAJI WANALIELEWA HILI.
 
Wizara zimekaliwa na watu wenye uwezo duni na vibaka!
 
Hapo Sumbawanga ujenzi wa Mradi wa Tactic km 12 kapewa Mchina wakati Sumry anaweza.

Mbeya Jiji km 15 kapewa Mchina wakati Wazawa wapo .

Huu upumbavu ukome mara Moja.
Wakandarasi wa ndani wenyewe wakipewa kazi mnawapiga hamwalipi kwa wakati huo uwezo wa kimitaji na mitambo anaupata vipi.

Mkandarasi anapewa kazi anafanya kwa tabu sana halafu analipwa baada ya miaka 10 toka akamilishe mradi na hela yenyewe anaipata kwa kugawana na wahuni walioko kwenye mfumo.
 
Kwa sababu sera haikuwa inawapa kipaombele ila Kwa Sasa yote hayo yatakuwa addressed.

Najua hujui kwamba Kuna Samia Infrastructure bond imeanzishwa Kwa Ajili ya wakandarasi kupata pesa na dhamana za kazi.
 
uchumi wa maframe

nchi ya kichuuzi

unatategemea kupata dola kweli

nyie wazawa biashara zenu mabar,na usanii kukata mauno

ova
 
Tunamtakia tuwajengee uwezo wa ndani kwanza baadae wamikua wataenda Nje.
Nje wana viwango vya juu sana? So swali langu bado hata wakienda nje je watatekeleza kwa viwango vya kwao?

Nafikiri ni vema wakawa attached kwenyenmakampuni ya nje, wapate uzoefu kwanza kabla ya kurudi nyumbani
 
Tukikwambia ccm ni laana ya hili taifa ndo uwe unatuelewa
 
Nje wana viwango vya juu sana? So swali langu bado hata wakienda nje je watatekeleza kwa viwango vya kwao?

Nafikiri ni vema wakawa attached kwenyenmakampuni ya nje, wapate uzoefu kwanza kabla ya kurudi nyumbani
Lazima wapate uzoefu kutoka hapa ndio wataenda Nje.Wachina waliopata uzoefu kwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…