Dola zimeadimika kwasababu wageni wanavuna fedha za miradi kuliko wazawa

Dola zimeadimika kwasababu wageni wanavuna fedha za miradi kuliko wazawa

Tukitaka wazawa wapewe kazi, waaminiwe na mabenki ya ndani ili wakopesheke. Short of that ni ngumu sana, mtu akikufadhili atakupa masharti yake na lazima uyatimize. Ila ukiwa unafinance miradi kwa fedha zako(kupitia mabenki yako) mtu hawezi kukupa masharti ya wapi uchukue materials, labour force(skilled/unskilled) na mwishowe hutawalipa kwa fedha za kigeni.
 
Hivi Fedha zinazokopwa kwa ajili ya hii miradi ya maendeleo si inakuwa kwa USD?
 
Kila siku tunalia kuhusu kuadikika Kwa Dola licha ya juhudi za kukuza Uchumi lakini hakuna ambae anajadili jambo Hilo Kwa kuangalia sababu za msingi.

Mojawapo ya vitu vinavyosababisha kuadikika Kwa Dola Nchini no hizo hapa 👇

1. Kuwapa kazi za Ujenzi wakandarasi wa kigeni badala ya wazawa Kwa visingizio vya hawana uwezo na uzoefu(wageni hulipwa Kwa Dola)

2. Kuagiza bidhaa nyingi ambazo tunaweza Kuzalisha wenyewe ndani ya mwaka eg maziwa,ngano,Mafuta ya kula, sabuni, vyakula vya mifugo, mbegu nk

3. Kukwamisha uwekezaji kutoka Nje kutokana na mitizamo ya siasa za ujamaa(kusema Nchi imeuzwa Kwa Waarabu,kuwa na sera ambazo hazitabiriki,Urasimu wa Kiserikali na Rushwa) eg miradi ya Lindi LNG na Liganga imekwama kutokana na siasa uchwara.

---
WAGENI WAVUNA FEDHA ZA MIRADI KULIKO WAZAWA

SERIKALI imesema asilimia kubwa ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inawanufaisha wageni kutoka nje ya nchi kuliko wazawa.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema bungeni Dodoma kuwa sababu kubwa inayochangia hali hiyo ni uwezo mdogo wa makandarasi wa ndani wa kifedha, mitambo na wataalamu hivyo inakuwa vigumu kwao kushindana kwenye zabuni za kazi na makandarasi kutoka nje hasa kampuni za Kichina.

Bashungwa amesema hayo akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25 bungeni Dodoma jana. Alisema kwa mujibu wa takwimu za Bodi ya Usajili wa Makandarasi, kati ya miradi 36,839, wazawa walitekeleza miradi 35,351 sawa na asilimia 95.9 ya miradi hiyo.

Hata hivyo, Bashungwa amesema miradi iliyotekelezwa na wazawa ni midogomidogo yenye thamani ya Sh trilioni 23.749, sawa na asilimia 38.5 ya thamani ya miradi yote iliyosajiliwa na kutekelezwa katika kipindi hicho ambayo ni Sh trilioni 61.638.

“Hivyo, makandarasi wa nje ambao ni takribani asilimia 4.1 walitekeleza miradi michache yenye thamani kubwa (asilimia 61.5 ya thamani ya miradi yote),” amesema Bashungwa.

Kwa mujibu wake, kuna kampuni 14,800 za ndani za makandarasi, za ushauri wa wahandisi ni 252 na kampuni za wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi ni 461.

Chanzo: Habari Leo

My Take
Naunga mkono wazo la Bashungwa kuanza kuwaamini Wakandarasi Wazawa.Sheria hii isiishie Wizara ya Ujenzi pekee Bali Taasisi zote.Tanzania sio Mali ya Wachina pekee.
Sisiemu hoyeee....
 
Sawa kwa vile unashinda Jamii forum kusoma umbeya, ukitoka unaingia whatsApp kuangalia status, ukitoka hapo unaingia Youtube kuangalia video za Mwakatobe, ukitoka hapo unaingia tiktok na unamalizia facebook huwezi kuelewa ndiyo maana umeishia na jibu moja tu la muongo.
Mitandaoni kuna pesa nyingi sana shida mfumo wa upokeaji wa fedha. Kwa akili yako huwezi kuelewa kwasababu wewe ni msoma umbeya
Sema maliza ww ni Muongo. Toa ushahidi, watu wanashindwa kufanya kazi Mitandaoni shida dolla. Nyie watu wa dar mnaoishi kimara baruti na kupanda mwendokasi mnaona mnajua kila kitu nyie. Njoo na fact na sisi tuishio nzega tuje na zetu na kazi za mitandaoni.
 
Angekua anaonyesha njia usingekuja kulalamika huku
Fahamu kila kitu kipo chini ya ccm
Ndo maana nasemaga machawa hamnaga akili
Hivi unajua hii taarifa imetoka hewani Kwa sababu zipi? Ni baada ya Serikali ya Mama kuamua kubadili Hali mbovu ya awali na kuonesha wapi tunakwama.

Hilo la wakandarasi is over,Bado la kuzuia importation ya maziwa na Mafuta
 
Nimependa hoja yako, lakini sababu ya kupungukiwa ni sababu ya low seasonal inflow kutoka katika sekta hizo au kuna la zaidi?

Hivi inawezekana nchi ikawa na high inflow throughout the year?
Low and high seasonal inflow ni kweli zipo ila wanasiasa wetu wanatumia hiyo kama loophole ya kujitetea kwa kutowajibika
 
Ila hawa wakandarasi wa ndani ni shida kuna njia wametengeneza Dodoma basi ni mashimo tu na lami inapotea ukipita unaweza kusema lami ya miaka 30 nyuma kumbe hata mwaka bado. Kuna shida sana kwenye hili lakini naamini kama wataleta ushindani wa quality watafanya sana kazi. Vifaa pia changamoto kwa maana mitaji yao midogo. Lakini kubwa ubora wa kazi zao wanashida sana, sasa sijui kusudi ili wa save pesa au ndio uwezo wao umefika mwisho.
 
Sema maliza ww ni Muongo. Toa ushahidi, watu wanashindwa kufanya kazi Mitandaoni shida dolla. Nyie watu wa dar mnaoishi kimara baruti na kupanda mwendokasi mnaona mnajua kila kitu nyie. Njoo na fact na sisi tuishio nzega tuje na zetu na kazi za mitandaoni.
Siku nyingine usiwe una quote watu kudhihirisha ujinga ulionao. Una quote watu halafu hujui ulichoandika.
Endelea kusoma umbeya Jamii forum maana hata huelewi kuhusu making money online.
 
Back
Top Bottom