Dollar yaanza kushuka kwa kasi

Dollar yaanza kushuka kwa kasi

Ni kweli Dollar imeanza kushuka na shilingi ya kitanzania imeanza kuimarika hi kwa sababu kuu mbili
1. BOT ilikua na mnada wa hadhara wa dola na ilinunua dola za kutosha ili kukidhi manunuzi mbalimbali
2. Mapema mwezi 11 serikali ilianza kununua dhahabu ambayo itaiwezesha serikali kuuza na kupata pesa za kigeni moja kwa moja. Serikali kununua dhahabu ilitakiwa kuanza hili muda mrefu sana ili kupambana na upungufu wa pesa za kigeni, ila tunashukuru kwa kuchukua hatua

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
Yani umekaa serious unaandika uongo kabsa. So dunia nzima BOT ndio imefanya dola ishuke?
 
Hili tangazo ni la mwaka 2023?
Maelezo hayo ya benki hiyo yanakuja ikiwa ni siku nne tangu Tume ya Madini itangaze kuwa wachimbaji wakubwa na wauzaji wa dhahabu wanaotaka kuuza nje ya nchi wanatakiwa kutenga asilimia 20 ya madini hayo kwa ajili ya kuiuzia BoT.

Uamuzi huo ulifanywa na Serikali baada ya kufanyika maboresho katika Sheria ya Madini kufuatia kutungwa kwa Sheria ya Fedha ya mwaka 2024/25.
Mwaka huu bodi ya korosho ikitanganza kuanza mnada wa kununua korosho tafsiri yake mwaka Jana hawakununua koroshoa?

Ni kweli Dollar imeanza kushuka na shilingi ya kitanzania imeanza kuimarika hi kwa sababu kuu mbili
1. BOT ilikua na mnada wa hadhara wa dola na ilinunua dola za kutosha ili kukidhi manunuzi mbalimbali
2. Mapema mwezi 11 serikali ilianza kununua dhahabu ambayo itaiwezesha serikali kuuza na kupata pesa za kigeni moja kwa moja. Serikali kununua dhahabu ilitakiwa kuanza hili muda mrefu sana ili kupambana na upungufu wa pesa za kigeni, ila tunashukuru kwa kuchukua hatua

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
Ni kweli kabisa, hawa wakina mwigulu walilala sana, gold reserve inatakiwa iwe kubwa pale Bot Ili kuimarisha shilingi, mabalozi wote Duniani watafute masoko ya bidhaa zetu Ili kuongeza export. Raisi asiwachekee Wala rushwa kama anavyowalea sasa.
 
Nimeona hela nyingi kama zimeshuka natamani kupata uchambuzi kutoka kwa wanauchumi.
 
"Serikali kununua dhahabu ilitakiwa kuanza hili muda mrefu sana" KKumbuka hili alilifanya Ali hassan Mwinyi wakati akiwa Rais. Kwa bahati mbaya Mkapa akalifuta. Huenda hili likawa endelevu.
Biashara tuwaachie waliozaliwa kwenye biashara.
Uongo huu.

Mpango kwenye ulianza kwa mwinyi lakini ukafa kwa mwinyi pia(1994)

Sababu za huu mpango wa kununua gold kufeli ni baada ya kutokea udanganyifu mkubwa wakati wa kununua gold. Hivyo BOT ikapelekea kupata hasawa kubwa, wanunuzi wa serikali walikua wakishirikiana na watu wengine kununua gold isiyofaa tena kwa gharama kubwa. Mwisho huo mpango ukafeli mwinyi mwenyewe akiwepo
 
Hii comment sijaielewa. Nimekuambia mwaka Jana tulinunua pia gold, why dollar haikushuka? Hapa jibu straight maana ulichojibu sijaelewa
Wewe kununu gold kunashusha vip thamani ya dollar??? hivi mnajua mnachobishana nyie?? Semeni tumeuza dhahabu tumepata dollar ya kutosha... kununua kitu hakukuzi thamani yako ya pesa.
 
Taarifa yako Inaonesha kuwa Bot ilikuwa imefanikiwa kununua 418kg kwa almost mwaka
Lakina hapo chini nimekuletea taarifa ya mwezi oktoba tu walipofanikiwa kununua Zaid ya kg 800 Sasa kwahiyo unaposema mwaka jana Bot ilinunua dhahabu Zaid ya mwaka huu unataka kutuambia 400 na 800 ipi kubwa

Aidha, amesema kufuatia marekebisho ya sheria yaliyofanywa mwezi Julai na utekelezaji wake kuanza Oktoba mwaka huu, katika kipindi cha mwezi Oktoba 2024 peke yake, BoT iliweza kununua 872.05 kg na kuchangia hifadhi ya fedha za kigeni kwa $74.04 milioni.
 
Wewe kununu gold kunashusha vip thamani ya dollar??? hivi mnajua mnachobishana nyie?? Semeni tumeuza dhahabu tumepata dollar ya kutosha... kununua kitu hakukuzi thamani yako ya pesa.
Soma na uelewe usikurupuke. Kwa nn huwa hamsomi mnakimbilia kureply?????

Huyo amesema BOT walinunua gold mwezi wa 7 ndio umefanya dollar kushuka. Mm ndio nikamuuliza mbona mwaka jana BOT walinunua dollar lakini haikushuka. Hapo ndio tunabishana yeye anasema mwaka Jana BOT hawakununua dollar

Usikurupuke, muwe mnasoma kwanza
 
Bado hoja yangu iko pale pale.. Kununua dhahabu kule kununua dollar??? kipi ni kipi??
 
Dollar ilikua haipandi ila hela yenu ndio ilikua inashuka kwa speed nene na sasa hivi pia dollar haishiki ila hela yenu inajitahid kupanda
 
Taarifa yako Inaonesha kuwa Bot ilikuwa imefanikiwa kununua 418kg kwa almost mwaka
Lakina hapo chini nimekuletea taarifa ya mwezi oktoba tu walipofanikiwa kununua Zaid ya kg 800 Sasa kwahiyo unaposema mwaka jana Bot ilinunua dhahabu Zaid ya mwaka huu unataka kutuambia 400 na 800 ipi kubwa

Aidha, amesema kufuatia marekebisho ya sheria yaliyofanywa mwezi Julai na utekelezaji wake kuanza Oktoba mwaka huu, katika kipindi cha mwezi Oktoba 2024 peke yake, BoT iliweza kununua 872.05 kg na kuchangia hifadhi ya fedha za kigeni kwa $74.04 milioni.
Kwanza ulisema kununua tumeanza mwaka huu, hapo nadhani umejirekebisha mwenyewe maana ulianza kubisha.

Pili kuhusu kiasi kila taarifa Ina yake. Taarifa yangu ni kg 400+ , hiyo 360+

But haya yanaweza yasiwe mjadala. Mjadala wetu ni BOT ilianza kununua lini dollar. Tumeona ilianza mwaka jana tofauti na ulivyosema. So why mwaka Jana hakukua na poromoko la dollar dhidi ya TShs?

Kuhusu sheria mpya hiyo haihusiani kwenye huu mjadala sababu. Hata mwakani tunaweza Kuna na sheria nyingine lakini, hayo ni mabadiliko ya sheria ambayo hutokea mara kwa Mara. Ni sawa na sheria za ugavi kila Mara zinakuja lakini manunuzi hayajawahi kusimama
 
Sio mbaya..
Screenshot_20241211-163002_1.jpg
 
Hiki ulichoweka umekielewa kweli? Sijui umetoa wapi. Soma hiyo table na soma maelezo hapo mwanzo mwaka huu 15,000mil + from previous year 13,000mil+
Lakini kwenye table 2023 inaonyesha ni 7,000mil+

Anyway, kwa trend ya export hili anguko lingekuwepo toka miaka na miaka maana export huwa haisimami bali huongezeka kila mwaka(covid year excluded)
View attachment 3174499
Data za manunuzi zinapatikana Bot
Na hapo imewekwa kwa mwaka ila miaka ya kiserikali inaishia June.
 
Bado hoja yangu iko pale pale.. Kununua dhahabu kule kununua dollar??? kipi ni kipi??
Oyaa kuwa sasa kuelewa, hayo maswali unaniulizaje Mimi badala ya huyo aliyesema hayo? Mm mwenyewe namuhoji kwa nn aseme hivyo, alafu ww unanaiuliza tena mm? Ndio maana nakuambia acha kukurupuka soma kwa utulivu. Unachoniuliza mm ndio nachomuuliza huyo.
 
Data za manunuzi zinapatikana Bot
Na hapo imewekwa kwa mwaka ila miaka ya kiserikali inaishia June.
Unanieleza kitu ambacho nakijua. Hiyo link ya BOT umeweka sijaelewa. Nenda kwenye sehemu husika screenshot weka. Unaweka link ya jumla ambayo hata wewe huwezi kupitia kila kitu
 
Back
Top Bottom