Uchumi haupimwi kwa bei ya dola mkuu.
China ina uchumi mkubwa na hela yake Yuan haina thamani sana, na China inapigana kila siku ili Yuan isipande thamani ibakie kuwa cheap, kwa sababu wanapiga mahesabu ya kufanya exports nyingi sana zitakazozibia thamani ya Yuan kuwa chini.
Wanafanya makusudi hela yao iwe na thamani ndogo kimkakati.
0Kwenye dola kushuka bei Tanzania, kwanza US Federal Reserve (Benki Kuu ya US) imepunguza interest rate. Benki Kuu ikipunguza interest rate, maana yake bei ya kukopa inapungua.Thamani ya dola inashuka.
Pia, kwenye msiba wa Mafuru, rais Samia alisema moja ya kazi kubwa alizofanya Mafuru hapa mwishoni wakati bei ya dola iko juu sana na dola haipatikani, Mafuru aliishauri serikali vitu vya kufanya ili dola ipatikane zaidi, na Samia alisema walifanikiwa. Hakutaja walifanya nini lakini inaonekana wameongeza dollar supply kwa mkupuo kiasi kwamba supply imekuwa kubwa sana kushinda demand na kiuchumi hilo linasababisha bei kushuka.