Domant phone numbers wanazogawiwa wateja wapya

Pole sana. Ulikuwa umeisajili kwa jina lako? Kama ndio hivyo ninaona bado tatizo halijaisha vizuri.
Labada nikairenew then niifunge niitupe
 
Nimeitupa mkuu hali haijawa shwari kabisa
Haya makampuni ya simu mawazo ya aina hii wanapaswa kufanyia kazi. Mwaka 2012 simu yangu iliibwa na laini ya Vodacom. Baada ya siku kumi kampuni hiyo ilimpa mteja wao namba kama ileile. Alichokipata yule dada Mungu anakijua. Nilielewa baada ya kufanya majaribio ya kuipiga namba ile ndipo dada alifunguka yaliyokuwa yakimsibu akipigiwa simu. 😂😂😂😂😂
 
Umejichanganya shabani kaoneka😂
 
Mimi ilinitokea, kuna watu wengi walikuwa wakinigia kutokea Lindi.
Kuna siku dada mmoja ikabidi niende naye sawa. Nikamuuliza, huyu unayemtafuta hauna namba yake nyingine? akasema namba nyingine sina, ila naweza kuipata maana watu wake wa karibu nawajua. Nikamwambia nitafutie hixo namba basi, akanitafutia na akanipa.
Baadaye sasa ikawa akipiga mtu simu, namwelekeza tu kwamba mtu unayemtaka anatumia namba fulani. Baada ya miezi kadhaa ishu ikaisha kabisa.
 
Sio bongo tu, hata mbele huko ukiacha kutumia lime ya simu baada ya muda anapewa mtu mwingine...
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji725]
 
Aisee pole sana
 
Dada yetu wa kazi anapigiwa simu kama Rosa Ree yule rapper wa Arusha. Mara nyingi tu anapigiwa na watangazaji wanataka interview, wengine wanataka kumpa deals, wengine kumsalimia. Huwa akiwaambia sio yeye wengine wanauliza Rosa Ree mwenyewe wanampataje na wengine wasumbufu hujua labda ni mtu wake wa karibu kashika simu, huwa wanajaribu tena
 
Mimi nilipewa namba alokua anatumia bwana Asenga, asee bibi babu, wajomba yani kalibia ndugu wote wanamlilia shida nadhanu ndo sababu akaitelekeza, kubwa kuluko yote ni ile miamala ya n m b, alafu ilikua kipindu cha watumisgu hewa,
 
Hiyo ni kawaida kwa mitandao yote. Line ikiwa dormant miezi mitatu wanapewa wateja wengine.
TIGO kwa hili nawasifu sana namba mpk kupewa mtu mwingine inaweza chukua hata mwaka au miaka 2
lkn AIRTEL na HALOTEL wapuuzi sana tena sana waweza kukuharibia biashara yako yani namba ishajulikana na wateja ss ikatokea tatizo ikawa haupo hewani kwa miezi kadhaa ebwanaee siku unaenda kuirenew unaambiwa kashapewa mtu mwingine unaweza ukampiga mtu ngumi

.kuna ndugu yangu alikuwa anaishi SOUTHAFRICA
sasa alikuja TANZANIA akakaa Kama miezi minne hivi sasa ile tayari anajiandaa kuondoka kurudi BONDENI ndo ikawa CORONA na mipak ikafungwaa
akabaki TANZANIA kwa mwaka mmoja zaidi mpk mpaka wa SOUTH ulivyofunguliwa
jumla alikaa TANZANIA mwaka 1 na miezi 6
siku anaondoka akasema mpk akifika nyumbani atatumia Simu ya mkewe kutujurisha kam amefika salama
mana tuliamini (kwa upuuzi tuliouzoea watanaznaia)kwa muda aliokaa ile lain itakuwa ishafungiwa pengine hata kupewa mtu mwingine
lkn cha kushangaza ike kutua tu OLIVA THAMBO akatucheck kwa namba ile ile na salio lake lilikuwa vile vile hakuongeza
yeye alishangaa hata sisi tulishangaa
kusema ukweli WENZETU upuuzi upuuzi hawana kabisa ndo mana wanazidi kufanikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…