Tuchukulie mfano mmoja huu hapa wa hayo maombi ya Yanga.
View attachment 3364376
Hii barua imeandikwa August. Fainali ya FA ilifanyika June, yaani ndani ya miezi miwili kabla. Mshindi anatakiwa apewe pesa zake lini baada ya fainali? Je Yanga hawajawahi kutumia huu utaratibu wa kuwa na madeni na kuomba pesa zao mbalimbali zinazopitia huko TFF zitumike kupunguza au kulipia madeni hayo kama utaratibu ulio rafiki zaidi kwao?
Huyu hapa ni Festo Sanga, Mjumbe wa Bodi ya Singida BS ambaye pia ni Mbunge.
View attachment 3364379
Yanga wameamua kukinukisha na kuishambulia Bodi ya Ligi na TFF kutoka kila kona hata kwa habari ambazo wanajua siyo za kweli wakijua hii pressure inaweza kuwafanya TFF na Bodi ya Ligi kubadili msimamo wao kuhusu derby au wasitoe maamuzi makali dhidi ya Yanga kutokana na kutopeleka timu uwanjani 15/06.