Tatizo kubwa la Trump ni majivuno na kiburi chake.
Kilichomponza Trump ni ego yake. Kosa la kwanza la kumlipa mwanamke afiche siri siyo siyo crime, linakuwa crime tu kama lilifanyika ili kuficha kosa jingine. Sasa hapo kwenye ufichaji wa kosa jingine ndipo ego ya trump ilipompoza kwani iliwezekana kabisa kumlipa bila kuhusisha na uchaguzi ila akagtumia njia za kuwadharau waliokuwa wanamsaidia, na ndio waliomtosa.
Ukifuatia kosa la documents liliko mahakama ya Miami, nayo utagundua pia kuwa ni ego yake ndiyo iliyomletea matatizo. Idara ya kumbukumbu ilimwomba makaratasi matatu tu: (a) Barua aliyoachiwa na Obama (b) Barua aliyoandikiwa na Kim Jong Il (c) ramani iliyokuwa inatumika kuonyesha njia ya Hurricane Dorian. Lakini yeye kwa ego yake akawasumbua kwa zaidi ya mwaka mzima mpaka wakatumia amri ya mahakama na mwishowe kuvamia nyumbani kwa na kukuta document nyingi za serikali ambazo hakutakiwa kuwa nazo ambazo alikuwa anajitahidi sana kuzificha.
Baada ya kujikuta kuwa kosa lake dogo la ego limezaa tatizo kubwa kisheria, yeye anageuza kuwa la kisiasa na majuzi tu anasema kuwa Biden aliamuru FBI watumie deadly force kumkamata na kusahahu kuwa issue ilikuwa ni idara ya nyaraka za serikali.