Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

Mkuu, usimtee sana Kamala na Democrats. Awamu yao imekuwa mbovu mno katika historia ya Marekani. Isitoshe, sera zao nyingi ni fedheha kupindukia.
 
Yes, ni kweli kabisa.

Joe Biden alipaswa atangaze angalau mwaka mmoja kabla ya mwaka wa uchaguzi kwamba hataweza kugombea tena kiti cha uRais ili kuwapa nafasi Wanachama wa Chama chake cha Democrats muda wa kutosha wa kumuandaa Mgombea mwingine badala yake.
 
Bila popular votes huwezi kupata electoral votes. Hizo zinategemeana kabisa. Unadhani kwa nini Trump amepata electoral votes 16 za jimbo la Florida?

Kwa sababu ameshinda jimbo hilo. Bila kushinda jimbo husika, unakosa electoral votes zake.
Sasa ina maana gani hii? Mbona ni kupoteza muda kusiko na maana yoyote.

Kama kushinda popular votes ndiyo kushinda electoral votes kwanini isiachwe tu hiyo popular votes?

Hillary Clinton alipogombea na Donald Trump, Hillary Clinton alimshinda Trump kwenye popular votes lakini Trump akamshinda Hillary Clinton kwenye electoral votes na kupelekea Trump kuwa Rais wa Marekani.

Sasa hoja yako ya kwamba popular votes na electoral votes zinaendana mbona kama haina uhalisi?
 
Ama walidhani Joe Biden angeweza kupiga muhula mwingine wa miaka 4, au walikuwa wanapoteza muda ili Kamala Harris asipitie ile michakato, ushindani na michujo chamani kwake.

Nadhani hii ya pili ndiyo sahihi zaidi, maana kila mtu alijua Joe Biden hangeweza tena kuwa rais.

Hatua yao ya kujaribu kumrahisishia njia Kamala ndiyo imewagharimu kukubwa.
 
Trump ameshinda katika ngome zote zenye upinzani mkali:
1. Georgia
2. North Carolina
3. Pennsylvania
4. Wisconsin

Bado 3
5. Arizona
6. Michigan
7. Nevada

Nimeamini huwezi kushinda uraisi wa Marekani bila kushinda jimbo la Pennsylvania!
Na hapo Pennsylvania si ndipo walipomchapa risasi? Kura za huruma probably ukizingatia electoral votes zipo za kutosha pale.
 
Ni rahisi na ungeelewa mifumo Yao ni mizuri sana
Kwani wananchi wakipiga kura moja kwa moja (popular votes) kuna shida gani?

Au nao ni wezi wa kura tu kama Afrika ndiyo maana hawawaamini wananchi wao kuwa na maamuzi ya mwisho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…