John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Suala hili mbona Mimi binafsi nimeshawahi kuliongelea Mara nyingi sana kwenye mtandao huu wa JF. Soma post zangu za siku za nyuma utaona wewe mwenyewe kuhusu suala hili.Nje ya manda: Unaamini Idd Amin Dada ndiye aliyeivamia Tanzania au Ni Nyerere ndiye aliuemchokoza Amini? Ukijibu kwa ufasaha swali hili basi utakuwa na uoeo mkubwa WA kuangalia "other side of the story"
Msimamo wangu upo very clear kwamba Nyerere ndiye aliyeanzisha chokochoko dhidi ya Idd Amin, kwa kutaka kumrudisha madarakani huko Uganda rafiki yake Obote ambaye alipinduliwa na Idd Amin.
Aidha, Idd Amin hakuwa mwendawazimu kwa kuichagua Tanzania peke yake na kuivamia huku akiziacha nchi zingine nyingi ambazo zinapakana na Uganda. Kwa nini aliivamia Tz tu peke yake na kuziacha hizo nchi zingine??? Why only Tanzania but not Kenya, Zaire, Rwanda, or Sudan? Why???
Tz inapaswa kuacha kuingilia kati migogoro ya ndani isiyotuhusu iliyopo katika nchi zingine za majirani zetu. Mambo ya ngoswe aachiwe ngoswe mwenyewe!