Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

Nimesema social media hapo ni x kwa media hakuna ni propaganda tu
Hata kwenye social meadia.

Ukiijua vizuri X utanielewa mkuu, kuna contents huwa zinafutwa kwa sababu za kisiasa ni vile haujawahi kuwa mwathirika kwenye hili.

Hata yeye mwenyewe Elon amekuwa akiitumia visivyo X yake angalia sakata la Venezuela na Brazil
 
Electoral votes, popular votes, majimbo...sijawahi kuelewa namna hawa jamaa wanavyohesabu kura.
Ukishinda jimbo lolote unachukua kura zote za wabunge (maseneta) wa eneo hilo hii wamefanya makusudi ili majimbo makubwa yasitokee yakaamua nani awe POTUS pekee
 
Imetangazwa dakika chache zilizopita na vyombo vya Habari

=====

Rais wa zamani Donald Trump kutoka chama cha Republican, ameshinda Uchaguzi wa Marekani.

View attachment 3144969
Chanzo: Spectator Index

Donald Trump ameoa mara tatu, Ivana na Marla Maples, mke wa kwanza na wa pili mtawalia ambao wote ametalikiana nao. Mke wake wa sasa ni Bi Melania.

Bwana Trump ana watoto watoto watano, watatu wa kiume Donald Trump Jr, Eric, Barron na watoto wawili wa kike Ivanka na Tiffany.

Rais huyo wa Zamani wa Marekani alizaliwa Juni 14 mwaka wa 1946, mjini New York, akiwa mtoto wa tano kati ya watoto sita.

Babake Fred alikuwa tajiri aliyemilki majumba na babu zake Trump walikua wahamiaji kutoka Ujerumani.

Mamake Mary alikuwa mzaliwa wa Scotland.


Tangu utotoni, Trump alikuwa mtundu na wazazi wake walimpeleka shule ya msingi iliyofadhiliwa na jeshi mjini New York.

Baadaye alifuzu kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania, kitivo cha elimu ya biashara mwaka wa 1968.

Alifanya kazi katika kampuni ya babake ambaye aliendesha biashara ya kuuza nyumba kwa raia wa kipato cha kadiri, viungani mwa New York.

Hata hivyo Donald Trump alikuwa na ndoto ya kufanya biashara nje ya makaazi ya Queens na Brooklyn.

Aliwekeza katika biashara kubwa ya ujenzi na kuweza kujenga mojawapo ya mijengo ya kifahari zaidi nchini Marekani. Alifanikiwa kutokana na sera ya kiuchumi iliyowekwa na utawala wa Reagan miaka wa 1980.

Yapo mahoteli, viwanja vya mchezo wa gofu, makazi ya kifahari, majumba ya kamari kutoka Carlifonia hadi Mumbai nembo yake ikiwa ni Trump.

Ameandika Riwaya kadhaa kuhusu biashara, huku umaarufu wake uking'aa zaidi katika makala yanayoelezea maisha halisi, "The Apprentice," katika runinga ya NBC. Hata hivyo alitupwa nje ya makala hayo baada ya kutoa kauli zilizowakera raia wa Mexico.
Muslim Brotherhood Wański *yea huko waliło; mass deportation
 
Chukulia kwa urahisi kabisa kwenye ligi za mpira;
-Sheria ni ukishinda unapata pointi tatu, droo point moja, ukifungwa hupati kitu.

-Ni system nzuri sana Iliwekwa kuhakikisha anaeshinda urais, ushindi wake uakisi uwakilishi wa majimbo yote yanayounda nchi ya marekani.

-Vinginevyo wanasiasa wahuni especially hao democrat wangekua wanawapa uraia wahamiaji haramu wengi kwenye majimbo ambayo wana advantage ili wapige kura nyingi wawawezeshe kushinda kama kigezo ingekua mshindi wa kura za nchi nzima ndo mshindi wa urais.

-Ni kama tu kwenye mpira, timu ikishinda 10-0 inapata point tatu sawa sawa na timu iloshinda 1-0
Ndiyo umeeleza nini sasa?

Sina uhakika hata kama wewe mwenyewe umeelewa ulichoandika.

Swali ni dogo sana, kwanini hawaachi kura za wananchi ndiyo zikawa kura za kuamua mshindi?

Kama ni demokrasia basi demokrasia nzuri na yenye uhalisia ni ile mamlaka ya uamuzi kuachiwa umma.

Sasa hii ina tofauti gani na China ambako tunaambiwa hakuna demokrasia ya kweli ambapo Rais anachaguliwa na bunge.
 
Tulisema humu watu wakatunanga. Hii inaita Reset Button
Dunia ilirudi kwenye mstari
Mungu ni mmoja
Imani kuu ya …… turudi kusali na kuabudu Mungu wa kweli!
Christmas itang’ara this time around.
 
Hiyo electrol vote naona ni km inabalance maamuzi ya majimbo yote
Huoni pia unaposema inabalance maana yake ni sawa na kuwanyima haki ya kumchagua Rais wamtakaye hao unaosema wapo wengi kwenye majimbo yao?

Kuna usemi usemao wengi wape sasa hapo mbona kama wengi wananyimwa?
 
Chukulia kwa urahisi kabisa kwenye ligi za mpira;
-Sheria ni ukishinda unapata pointi tatu, droo point moja, ukifungwa hupati kitu.

-Ni system nzuri sana Iliwekwa kuhakikisha anaeshinda urais, ushindi wake uakisi uwakilishi wa majimbo yote yanayounda nchi ya marekani.

-Vinginevyo wanasiasa wahuni especially hao democrat wangekua wanawapa uraia wahamiaji haramu wengi kwenye majimbo ambayo wana advantage ili wapige kura nyingi wawawezeshe kushinda kama kigezo ingekua mshindi wa kura za nchi nzima ndo mshindi wa urais.

-Ni kama tu kwenye mpira, timu ikishinda 10-0 inapata point tatu sawa sawa na timu iloshinda 1-0
Kwa tafsiri ya demokrasia ambayo wao wazungu ndiyo waanzilishi wa tafsiri na maana ya demokrasia basi wao ndiyo hukeuka hiyo dhana ya demokrasia.

Nimeambatanisha hapa nini tafsiri ya demokrasia na majibu ni kama haya.

Je, bado unataka tuamini kwenye uchaguzi wa Marekani kuna demokrasia?
 

Attachments

  • Screenshot_20241106_150851_ChatGPT.jpg
    Screenshot_20241106_150851_ChatGPT.jpg
    320.5 KB · Views: 3
Back
Top Bottom