Dondoo za mradi mkubwa wa kuchakata na kusindika gesi asilia - LNG

Dondoo za mradi mkubwa wa kuchakata na kusindika gesi asilia - LNG

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Hivi karibuni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini ya makubaliano ya awali ya mkataba wa mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia na kampuni za Equinor ya Norway na Shell ya Uingereza.

Rais Samia amesema mradi huo ni wa kimkakati kwa nchi ambao utakapokamilika utaingizia nchi mapato na kuinua uchumi. Mradi huu pia utazalisha ajira na kuchangia katika kujenga uwezo wa watanzania kupitia mafunzo, elimu, kuinua teknolojia na utafiti.

Dondoo za mradi huu:
Hadi kufikia mwezi Mei, 2022, jumla ya futi za ujazo trilioni 57.54 za gesi asilia ziligunduliwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini

Kati ya hizo, jumla ya futi za ujazo trilioni 47.13 ni katika vitalu vilivyopo katika kina cha bahari na futi za ujazo trilioni 10.41 ni katika maeneo ya nchi kavu, ugunduzi wa kiasi hiki kikubwa cha gesi asilia ulifanyika kwa ushirikiano wa Serikali na Makampuni.

Utekelezaji wa mradi huu katika Mkoa wa Lindi utafanyika sambamba na uendelezaji wa miundombinu kwenye mkondo wa juu ili kuwezesha kuvuna rasilimali hiyo. Mradi huu mkubwa utabadilisha sura na taswira ya uchumi wa nchi yetu.

Eneo ambalo mtambo utajengwa tayari limeshajulikana na kuwekwa katika miliki ya Serikali kwa kuwalipa fidia ya takriban Shilingi bilioni 5.71 wananchi 642 waliokuwa wakazi wa maeneo hayo.

Mradi huu unatarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi, kuiongezea Serikali mapato, kuongeza ajira na kuongeza uwezo wa Watanzania kitaaluma.

Kati ya miaka minne hadi sita ya ujenzi wa mradi huu kunatarajiwa kuwa na ajira 10,000 na baada ya kukamilika kwa ujenzi, ajira za kudumu zitakuwa 500.
 
Gesi nasikia ilishauzwa tayari. Tunachoambulia ni kodi tu kama wakituhurumia na kusema kuwa wamepata faida!
 
Tungekuwa na viongozi wenye akili na wazalendo wasio na tamaa na kuelemewa na ubinafsi uliopitiliza, kama Taifa tungekuwa na 1/4 ya jeuri ya Russia.
 
Gesi nasikia ilishauzwa tayari. Tunachoambulia ni kodi tu kama wakituhurumia na kusema kuwa wamepata faida!
Ndio mnavyodanganyana huko vijiweni?
Sasa kama ilishauzwa mkataba huu umesainiwa kwa mantiki ipi?
Wabongo muache ujuaji mwingi wakati ukweli kichwani ni Mambumbumbu..!
 
Back
Top Bottom