Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

Mithali 3:27-30

Mithali 4:23 - Linda sana moyo wako kuliko yote uyalindayo, maana ndiko zitokako chemichemi za uzima.

Mithali 4:13 - Mkamate sana elimu, wala usimuache aende zake, mshike maana yeye ni uzima wako
%E8%B6%85%E7%BA%A7%E6%88%AA%E5%B1%8F_20230305_010859.jpg
 
Mithali 6:1-11

Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa rafiki yako, Ikiwa wewe na mgeni mmepeana mikono, Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,

Sasa, mwanangu, fanya hivi ukajiokoe,

Kwa kuwa umejitia mkononi mwa jirani yako; Nenda ukanyenyekee, na kumsihi jirani yako. Usiache macho yako kupata usingizi, Wala kope za macho yako kusinzia. Ujiponye kama paa na mkono wa mwindaji, Na kama ndege katika mkono wa mtega mitego.

Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana kiongozi, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.

Ewe mvivu, utalala hadi lini? Utaondoka lini katika usingizi wako?

Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! Hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.
 
Mithali 6:16-19

Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.

Macho ya kiburi,

ulimi wa uongo,

Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;

Moyo uwazao mawazo mabaya;

Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;

Shahidi wa uongo asemaye uongo;

Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.
 
Mithali 10:12

Kuchukiana huondokesha fitina, bali kupendana husitiri makosa yote.

Mth 12 : Afadhali mtu anayedharauliwa, ikiwa ana mtumwa, Kuliko ajisifuye, ikiwa anahitaji chakula.

Mith 13 : Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe;
Bali yeye ampendaye humrudi mapema.
 
Mithali :14

Mtu masikini huchukiwa hata na marafiki zake, bali watu matajiri wanamarafiki wengi.

Yeye anayemdharau jirani yake hutenda dhambi,
bali amebarikiwa yeye aliye na huruma kwa mhitaji.

Mithali 18:11

Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu;
Ni kama ukuta mrefu katika mawazo yake.- (Mjenge jamani, Mungu anataka.mjenge)

Mithali 18:22

Apataye mke apata kitu chema;
Naye ajipatia kibali kwa BWANA.

Mithali 18:24

Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa maangamizi yake mwenyewe;
Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.
 
Zaburi ya daudi .....Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu. katika malisho ya majani mabichi hunilaza, kando ya maji ya utulivu huniongoza, huinuisha nafsi yangu na kuniongoza katika njia za haki Kwa ajiri ya jina lake......naam ni japopita kati ya bonde la uvuri WA mauti sitaogopa mabaya Kwa maana Yeye yupo pamoja Nami, gongo lako na fimbo yako vyani fariji ,waandaa meza mbele yangu machoni pa watesi wangu umenipaka mafuta kichwani pangu na kikombe changu kina furika hakika wema na fadhiri zitanifuata siku zote za maisha yangu.Nami nitakaa nyumbani mwa bwana milele
 
30 Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.
Yohana 3:30

31 Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yu juu ya yote.
Yohana 3:31
 
Pole San,Kila ninapousikia huu mstari huwa nakumbuka ibada ya mwisho ya dear mama😭😭.....huu mstari mzito sana

Ufu 14:13​

Ufu 14:13 SUV​

Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
 
Zaburi ya daudi .....Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu. katika malisho ya majani mabichi hunilaza, kando ya maji ya utulivu huniongoza, huinuisha nafsi yangu na kuniongoza katika njia za haki Kwa ajiri ya jina lake......naam ni japopita kati ya bonde la uvuri WA mauti sitaogopa mabaya Kwa maana Yeye yupo pamoja Nami, gongo lako na fimbo yako vyani fariji ,waandaa meza mbele yangu machoni pa watesi wangu umenipaka mafuta kichwani pangu na kikombe changu kina furika hakika wema na fadhiri zitanifuata siku zote za maisha yangu.Nami nitakaa nyumbani mwa bwana milele
Zaburi 23
 
Ukisoma kitabu cha Ayubu usome kwa uangalifu sana maana Ayubu aliyasema hayo alipokuwa hamjui Mungu ( alikuwa anasikia sikia tu habari za Mungu , akamtumikia kwa habari alizosikia)
Rekebisha kauli yako,Ayubu hajawahi kutomjua Mungu,maandiko yanaeleza wazi kabisa,

AYUBU 1:1
Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi,jina lake alikuwa akiitwa Ayubu,MTU huyo alikuwa mkamilifu n mwelekevu,Ni mmoja aliyemcha Mungu na kuepukana na uovu

Sasa kwa nini unasema alikuwa hamjui Mungu?
 
Back
Top Bottom