Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

Usiwapangie Watu kuamini waamuavyo.

Mungu anaweza kutenda mambo yote (hakuna jambo lolote linalomshinda) lakini hawezi kuzaliwa, ni akili hizo au matope?

Mungu kakuthibitishia kuzaliwa bila ya biological factors (sexual intercourse) za kibinadamu ili uone jinsi gani anaweza kufanya jambo lolote sababu NGUVU, UWEZO na MAMLAKA vina yeye na UKAMILIFU wake umepita fahamu za Binadamu, nyau wewe [emoji1]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Tukitumia logic hii hii inamaanisha hata wanaoabudu ng'ombe na wanyama wengine wapo sahihi maana Kwa imani yao Mungu amechukua umbile la huyo mnyama mfano wahindu.
 
Usiongee mambo ya utumishi wa Mungu bila kuwa na uhakika nayo.

Unaweza kuingia dhambi ya Kumkufuru Roho Mtakatifu.

Wewe una kipimo gani cha Kiroho kinacho watambua Watumishi wa Mungu ?

Kwanini wewe usiwe Mtumishi sahihi wa Mungu ?

Kumbuka hata Yesu pamoja na Ukamilifu wake alishawahi ambiwa kuwa ni Nabii wa Uwongo na baadhi ya watu.

Chunga Sana Ulimi Wako Unapofika Kuwasema Vibaya Watumishi wa Mungu.

Kuna maelfu ya watu wanaokoka kupitia mafundisho yao kwa hali yoyote wawavyo.
Tukija kwako unatumia nini kuwatambua watumishi wa Mungu? Na kwanini niamini kipimo chako kwamba ndiyo sahihi?
 

1 Tim 4:12 SUV​

Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

Lk 2:52 SUV​

Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.

Efe 6:11-18​

Efe 6:11-18 SUV​

Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.

Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.

Mit 8:17 SUV​

Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.
=======================
Haya wana wa Mungu twendeni kazi
👇🏻👇🏻👇🏻
Kwa sababu ni weekend
  1. ‭‭Zab‬ ‭104‬:‭14‬-‭15‬ ‭SUV‬ “Huyameesha majani kwa makundi, Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu; Ili atoe chakula katika nchi, Na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung’aze uso wake kwa mafuta, Na mkate umburudishe mtu moyo wake.”🍷🌾
  2. Mithali 31:6-7 (SUV) - “ Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini. Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake. 🍷💧
  3. Amosi 9:14 (BHN) - "Nitarekebisha hali ya watu wangu Waisraeli.Watajenga miji yao iliyoharibiwa na kuishi humo;watapanda mizabibu na kunywa divai yake;watalima mashamba na kula mazao yake." 🍇🍷

Take care guys. Don’t take it personal. Akili zangu changanya na zako. Tumia kiasi. 🥂
 
wakorinto nane inasema.....
walamimi yesu sikufia msarabani
mungu alininyakuwa kupitia wingu zito lililo tanda sehemu ile yamateso
akawawekea mwili mwingine ambao sio wangu wakautesa na kuuwa
kwahio Mimi sijafa Wala sijaondoka na zambi za yeyote
nasiku yamwisho nitarejea duniani ili nikionje kifo coz kilanafsi lazima itayaonja mauti

wale mnaoniona Mimi nimungu imekula kwenu Mimi sio mungu Bali ni nabii Kama manabii wengine
 
huyo shehe wako Mimi simjui.siwezi kukasirikia watu wamotoni mimi.hapanaandika huku nacheka Sanaa nikiona mnavyo chafukwa ka vifungu vyangu vinavyo wachoma
Humfahamu KIPOOZEO😅😅😅😅😅 MUULIZE FaizaFoxy anyejua dini wr kilaza tu
 
Mungu Hafurahii Waovu Kufa, anatuambia Kwa Upendo kabisa..."Ghairini ,ghairin mkaache njia mbayaaa ..mbona mnatala kufa????.


Ezekiel 33:11
Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu wovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini,ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli?
 
Yohana 3:16
[16]Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Yohana 3:36
[36]Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.

Yohana 5:24
[24]Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.

Yohana 6:35
[35]Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.

Yohana 6:40
[40]Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

Yohana 6:47
[47]Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye yuna uzima wa milele.

Yohana 11:25
[25]Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;

Yohana 20:30-31
[30]Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki.
[31]Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.

1 Timotheo 1:16
[16]Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristo audhihirishe uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini baadaye, wapate uzima wa milele.

1 Yohana 5:13
[13]Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu.

Warumi 8:1-2
[1]Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
[2]Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.


Isaya 28:16
[16]kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka.
 
Tukija kwako unatumia nini kuwatambua watumishi wa Mungu? Na kwanini niamini kipimo chako kwamba ndiyo sahihi?
Mimi sijasema chochote juu ya Usahihi au Uwongo wa watumishi wa Mungu.
Wewe ndio umewasema, ndio ninakuuliza umetumia kipimo gani cha Kiroho kuwapima na kuwasema hivyo ?
Hebu tuwekee hapa tafiti yako hadi ukahitimisha hitimisho lako juu yao.

Mnapenda sana kuwasema vibaya Watumishi wa Mungu kwa kubuni buni tu ili kuwadhalilisha bila sababu za msingi.
Kwanini wewe usiwe Mtumishi sahihi wa Mungu badala yao ?
 
Wagalatia 1:6 Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine.

7 Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo.

8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.

9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.
 
1 Petro 2:2
Kama watoto wachanga waliozaliwa,yatamanini maziwa ya akili yasiyo ghoshiwa ili Katika hayo mpate kuukulia wokovu.
 
Ayubu 14 :1
Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake si nyingi,naye hujaa taabu

Huu mstari huwa unanipa Sana muda wa kutafakari njia zangu.


Wafilipi 4:13
Ninayaweza Mambo yote Katika yeye anitiaye nguvu

Huu mstari unanipaga Sana ujasiri kupita nyakati zinazo onekana Ni ngumu kwangu
 
Back
Top Bottom