Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

Warumi 1
26 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;

27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.

28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.

Ndiyo hayo ya polisi wa zenji tunayashuhudia
Biblia imeongelea mambo mengi ambayo yalitokea, yametokea, yatatokea
 
Usiwapangie Watu kuamini waamuavyo.

Mungu anaweza kutenda mambo yote (hakuna jambo lolote linalomshinda) lakini hawezi kuzaliwa, ni akili hizo au matope?

Mungu kakuthibitishia kuzaliwa bila ya biological factors (sexual intercourse) za kibinadamu ili uone jinsi gani anaweza kufanya jambo lolote sababu NGUVU, UWEZO na MAMLAKA vina yeye na UKAMILIFU wake umepita fahamu za Binadamu, nyau wewe [emoji1]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
unajiona muelewa Kumbe kiazi tuu.mungu hazaliwi mbwa nyieeeee
 
Yohana 14:6​

Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
yes waislamu hatuta ingia peponi bila kufuata matendo ya mtume umeelewa wewe kiazi.

maana yake yesu alikuwa mtu mwema kwahio ukifata matendo yake utajiweka mahali salama.hio bibilia hata hamuielewi manyau nyie.
 
WIMBO ULIO BORA 4:7, 9

7. Tazama ulivyo mzuri ee mpenzi wangu,
wewe huna kasoro yoyote

9. Umefurahisha moyo wangu, dada yangu, bi arusi, umefurahisha moyo wangu,
kwa kunitupia jicho mara moja tu,
na kwa huo mkufu wako shingoni
 
yes waislamu hatuta ingia peponi bila kufuata matendo ya mtume umeelewa wewe kiazi.

maana yake yesu alikuwa mtu mwema kwahio ukifata matendo yake utajiweka mahali salama.hio bibilia hata hamuielewi manyau nyie.
Mkatom...be mabikira 72 🤣🤣🤣🤣🤣🤣 na mito ya POMBE

MMELOGWA
 
Mathayo 5:43
Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;

Mathayo 5:44
lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

Mathayo 5:45
ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

Mathayo 5:46
Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?

Mathayo 5:47
Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?

Mathayo 5:48
Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
 
Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasita-sita katikati ya mawazo mawili hata lini? Bwana akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno.

1 Wafalme 18:21
 
YOHANA 1:1-5.

Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.
 
YOHANA 1 :9....

9 Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.
10 Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.
11 Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.
12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
 
YOHANA 1:29.

29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!
 
Mathayo 28:16 Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu.

17 Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka.

18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.

19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
 
1 Yohana 4:1-3
********************************************************************************************
4 Wapendwa, msiamini kila roho bali zipimeni roho zote kwa makini muone kama zinatoka kwa Mungu. Kwa maana manabii wengi wa uongo wametokea duniani. 2 Na hivi ndivyo mtakavyomtambua Roho wa Mungu: kila roho inayokiri kuwa Yesu Kristo alikuja kama mwana damu, hiyo inatoka kwa Mungu. 3 Lakini roho yo yote ambayo haimkiri Kristo, si ya Mungu. Hii ndio roho ya mpinga-Kristo, ambayo mmekwisha kusikia kwamba inakuja, na sasa tayari iko duniani.
*******************************************************************************************
Hii mistari imeniumbusha kuhusu manabii wa uwongo waliotapakaa hapa nchini akiwaemo Geordevie na wengine kibao akina Mwamoosa, et al. Mungu atunusuru na hawa wapigaji wanaowakaanga masikini kwa jina la Yesu.
 
Isaiah 41:10
Don’t be afraid for I’m with you.
Don’t be discouraged for I’m your God. I will strengthen you and help you. I will hold you up with my victorious right hand!
Aaaamina [emoji2972]
 
1 Yohana 4:1-3
********************************************************************************************
4 Wapendwa, msiamini kila roho bali zipimeni roho zote kwa makini muone kama zinatoka kwa Mungu. Kwa maana manabii wengi wa uongo wametokea duniani. 2 Na hivi ndivyo mtakavyomtambua Roho wa Mungu: kila roho inayokiri kuwa Yesu Kristo alikuja kama mwana damu, hiyo inatoka kwa Mungu. 3 Lakini roho yo yote ambayo haimkiri Kristo, si ya Mungu. Hii ndio roho ya mpinga-Kristo, ambayo mmekwisha kusikia kwamba inakuja, na sasa tayari iko duniani.
*******************************************************************************************
Hii mistari imeniumbusha kuhusu manabii wa uwongo waliotapakaa hapa nchini akiwaemo Geordevie na wengine kibao akina Mwamoosa, et al. Mungu atunusuru na hawa wapigaji wanaowakaanga masikini kwa jina la Yesu.
Usiongee mambo ya utumishi wa Mungu bila kuwa na uhakika nayo.

Unaweza kuingia dhambi ya Kumkufuru Roho Mtakatifu.

Wewe una kipimo gani cha Kiroho kinacho watambua Watumishi wa Mungu ?

Kwanini wewe usiwe Mtumishi sahihi wa Mungu ?

Kumbuka hata Yesu pamoja na Ukamilifu wake alishawahi ambiwa kuwa ni Nabii wa Uwongo na baadhi ya watu.

Chunga Sana Ulimi Wako Unapofika Kuwasema Vibaya Watumishi wa Mungu.

Kuna maelfu ya watu wanaokoka kupitia mafundisho yao kwa hali yoyote wawavyo.
 
Yohana 4:23
“Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.”

Tumefika hii majira ya kumuabudu Mungu Baba na sio mwana tena. 1korintho 15:24-28
 
Back
Top Bottom