Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

Hosea 4:6
"Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;
kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa,
mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi;
kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako."
 
Efe 1:7 Katika yeye huyo, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi sawasawa na wingi wa neema yake.
Tumekombolewa. In Eng it says we have been redeemed through his blood. Being redeemed is being saved.

Katika thesaurus kuwa saved ina visawe vingi. And kuwa saved, means kuokolewa, kutolewa katika hatari na kuwekwa katika usalama, kukabidhiwa mahali ama sehemu husika (delivered), kutolewa kwenye kifungo au utumwa (freed), kurudisha kile kilichokuwa kimepotea (recovered), kulindwa dhidi ya uvamizi au shambulio kutoka kwa adui (protect), kuwekwa huru kutoka kwenye zuio/kizuizi cha kisheria (emancipated).

So katika Kristo Yesu, tumefanyiwa haya yote, kwa njia ya Damu yake, sawasawa na wingi wa neema yake. Verse ni nyingi lakin hii ni mojawapo ya my best verse..so far.
 
Yoshua 24:15
"Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia: kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao. Lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana."
 
Mhuburi 9:11
"Nikarudi na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo, lakini wakati na bahati huwapata wote."
 
IMG_7223.jpg
 
"Mungu ni roho, na wote wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli"

huu mstari unapatikana kwenye kitabu cha YOHANA
 
Mathayo 24:24
24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.

Watu washaliwa mwamba anajenga mahotel na kununua mashamba ya maparachichi, nauliza nyinyi mmeleta posa kwetu je mwa m posa nani?
 
Wagalatia 5:26

"Muda na njaa sio rafiki wa mwanadamu."
 
Nikiwa mvulana kuna siku dingi akaniwakia wakati sikuwa na kosa lolote, nilikasirika, koromeo likawa linawaka moto kwa hasira; ghafla mstari huu ukanija moyoni na hasira yangu ikayeyuka mara. Ama kweli neno la Mungu ni dawa, likijaa ndani yako utayashinda majaribu mengi sana.

Vv
Mwamba Mungu wa Mbinguni akubariki sana😅😅😅
 

YOSHUA MWANA WA SIRA 22​


1Mvivu hufanana na jiwe litiwalo mavi,
Kila mtu atamfyonya katika aibu yake.
2Mvivu hufanana na uchafu wa jaani,
Kila augusaye atakung'uta mkono.

3Ni aibu ya baba kuzaa mwana aliye juha,
Na binti asiye na akili ni hasara yake.
4Binti mwenye busara ni tunu kwa mumewe;
Bali aletaye aibu ni huzuni ya mzazi wake.
5Aliye mtundu huwaaibisha baba na mume,
Naye atadharauliwa na wote wawili.
Du! Hii mbona haimo kwenye biblia mkuu?
 
~Zaburi 19:14

Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.
Halafu umenikumbusha kuna ka wimbo ka huu mstari, umefanya nimkumbuke my late Mother 🥹🥹
 
Back
Top Bottom