Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

Mwanzo 3
1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu.

Wewe baki na werevu wako...

Mit 26:5 SUV​

Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake.
 
mungu hazaliwi wewe kiazi
Usiwapangie Watu kuamini waamuavyo.

Mungu anaweza kutenda mambo yote (hakuna jambo lolote linalomshinda) lakini hawezi kuzaliwa, ni akili hizo au matope?

Mungu kakuthibitishia kuzaliwa bila ya biological factors (sexual intercourse) za kibinadamu ili uone jinsi gani anaweza kufanya jambo lolote sababu NGUVU, UWEZO na MAMLAKA vina yeye na UKAMILIFU wake umepita fahamu za Binadamu, nyau wewe [emoji1]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo yako yote
Na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.

Waraka wa Yohana ngapi sijui
Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo yako yote
Na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.

Waraka wa Yohana ngapi sijui

3 Yoh 1:2 SUV​

Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
 
Mwanzo wa ndoa umenakiliwa katika Mwanzo 2:23-24:

“Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu na nyama katika nyama nyangu, basi ataitwa “mwanamke,” kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”

Mungu alimuumba mwanamume na kisha baadaye akamuumba mwanamke ili amkamilishe mwanamume.

Ndoa “iliwekwa” na Mungu kwa sababu kuwa “si vema huyo mtu awe peke yake” (Mwanzo 2:18).

Neno “msaidizi” limetumika kumwelezea Hawa katika Mwanzo 2:20 lamaanisha “kumzunguka, kumkinga, kumsaidia.” Hawa aliumbwa awe kando ya Adamu kama “nusu yake” awe msaidizi wake.

Mwanamume na mwanamke, wakati wameoana wanakuwa “mwili mmoja.”

Huu umoja umedhihirishwa mara nyingi katika tendo la ndoa. Agano Jipya inaongeza onyo kuhusu umoja huu.

“Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe” (Mathayo 19:6).

Kunayo nyaraka nyingi za mtume Paulo zenye zinahusu ndoa na jinsi Wakrito wanastahili kuwa katika ndoa. Ukurasa mmoja ni 1 Wakorintho 7, na mwingine ni Waefeso 5:22-33. Tulijifunza pamoja, hizi kurasa mbili zinatoa kanuni za kibibilia ambazo zinaunda mwongozo wa ndoa ambayo ni ya kumpendeza Mungu.

Ufahamu wa Waefeso hasa ndio wa uzito hasa kuhusu ndoa yenye ufanisi.

“Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili”
(Waefeso 5:22-23)

“Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake”
(Waefeso 5:25)

“Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa”
(Waefeso 5:28-29)

“Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mana yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja”
(Waefeso 5:31)
🤝🏻🤝🏻🤝🏻🙏🏼
 
hahahahahaaa mkuu tuwaache tuu Mana akilizao fyatu.mara wanasema oo yesu niroho.yani ujinga ujinga mwingi
Anzisha mada ya Allah😂😂 tuje tukuambie Jehamanu haitajaa hadi Allah aingize mguu wake
 
Usiwapangie Watu kuamini waamuavyo.

Mungu anaweza kutenda mambo yote (hakuna jambo lolote linalomshinda) lakini hawezi kuzaliwa, ni akili hizo au matope?

Mungu kakuthibitishia kuzaliwa bila ya biological factors (sexual intercourse) za kibinadamu ili uone jinsi gani anaweza kufanya jambo lolote sababu NGUVU, UWEZO na MAMLAKA vina yeye na UKAMILIFU wake umepita fahamu za Binadamu, nyau wewe [emoji1]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app

Mit 26:5 SUV​

Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake.
 
3 Yoh 1:2 SUV​

Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
 
Hosea 4:6
"Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;
kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa,
mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi;
kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako."
Asante sa na kwa nukuu sahihi WANAANGAMIZWA
 
Back
Top Bottom