Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

.
IMG_20230227_165052_885.jpg


Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Msifadhaike mioyoni mwenu bali mumwamini Mungu, nyumbani mwa baba mna makao, kama yasingekuwamo nimgaliwaambia.
 
Matendo ya Mitume 4:12
[12]Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
 
Hili fungu William Miller alikosea kulitafsiri akadhani lingetokea Duniani na hivyo kuwa mwisho wa dunia kumbe sivyo na badala yake lilikuwa likitokea ktk hekalu mbinguni
Hakuna book ya bible ninayo ikubali kama kitabu cha Daniel kilinifanya kuijua sana historia ya nyuma ya dunia. Hasa sura ya 11 ilinivutia sana na ikanipa mengi sana ambayo nilistaajabu moja ya binadamu ambao waliwahi pita nawa appreciate Daniel kwangu ni heshima.

Habari za miller hadi kukosea hesabu bila huyo nisingejua kabisa.
 

1 Tim 4:12 SUV​

Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

Lk 2:52 SUV​

Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.

Efe 6:11-18​

Efe 6:11-18 SUV​

Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.

Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.

Mit 8:17 SUV​

Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.
=======================
Haya wana wa Mungu twendeni kazi
👇🏻👇🏻👇🏻



~Zaburi 19:14

Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.
 
Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo yako yote
Na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.

Waraka wa Yohana ngapi sijui
 
Mwanzo wa ndoa umenakiliwa katika Mwanzo 2:23-24:

“Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu na nyama katika nyama nyangu, basi ataitwa “mwanamke,” kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”

Mungu alimuumba mwanamume na kisha baadaye akamuumba mwanamke ili amkamilishe mwanamume.

Ndoa “iliwekwa” na Mungu kwa sababu kuwa “si vema huyo mtu awe peke yake” (Mwanzo 2:18).

Neno “msaidizi” limetumika kumwelezea Hawa katika Mwanzo 2:20 lamaanisha “kumzunguka, kumkinga, kumsaidia.” Hawa aliumbwa awe kando ya Adamu kama “nusu yake” awe msaidizi wake.

Mwanamume na mwanamke, wakati wameoana wanakuwa “mwili mmoja.”

Huu umoja umedhihirishwa mara nyingi katika tendo la ndoa. Agano Jipya inaongeza onyo kuhusu umoja huu.

“Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe” (Mathayo 19:6).

Kunayo nyaraka nyingi za mtume Paulo zenye zinahusu ndoa na jinsi Wakrito wanastahili kuwa katika ndoa. Ukurasa mmoja ni 1 Wakorintho 7, na mwingine ni Waefeso 5:22-33. Tulijifunza pamoja, hizi kurasa mbili zinatoa kanuni za kibibilia ambazo zinaunda mwongozo wa ndoa ambayo ni ya kumpendeza Mungu.

Ufahamu wa Waefeso hasa ndio wa uzito hasa kuhusu ndoa yenye ufanisi.

“Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili”
(Waefeso 5:22-23)

“Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake”
(Waefeso 5:25)

“Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa”
(Waefeso 5:28-29)

“Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mana yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja”
(Waefeso 5:31)
 
1.Binafsi Kifungu cha Kwanza Nachopenda Ni Kile kifungu Kinaeleza Mungu Anapigana Na Yakobo Mungu Akashindwa.
Mwanzo 32:24

2.Pia Napenda Hivi vifungu viwili,Pale Yesu anapoeleza kuwa Yeye Ni mtu,Kama mimi na wewe
Yohana 8:40 pia Timotheo wa 1 2:5

3.Hichi kifungu Cha Kuwapiga nacho Kina mwamposa Na Wajinga wenzake Nakipenda Sana
Mathayo 24:24
 
Mathayo 7:7-8
"Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea, naye atafutaye huona, naye abishaye atafunguliwa."
 
Back
Top Bottom